Abiria wa mabus ya Hajees na Mtei wakamatwa

Kule Kenya, Abiria waliozidi/simama ndio wanaopigwa fine, wenyewe na huku huenda sheria inasema hivyo ngoja tusubirie watallam watujuze

Kweli tusubiri wataalam wa sheria watuwekee vifungu...
 
Nchi ilikuwa inakosa LAW enforcer, sasa sheria zote tutazijua. nenda Rwanda Raia wote wana adabu, na tanzania nako tufike mahali tuwe na adabu.
 
Busara itumike.., hali bado ni ngumu kuweza kukaa abiria wote, hasa daladala hapa dar
 
hii ni habari njema sana! Najua wenye mabasi watawajibika kwa sababu mara nyingi kama unasafiri watu wawili wanaweza kukatiwa siti moja hasa kama mnapandia vituo viwili tofauti!

Hii sheria ingerekebishwa ili wenye mabasi nao wachukuliwe hatua kwa kukwepa kodi kutokana na abiria wanaozidi hawapewi tickets, na kama watapewa tickets huwa ni fake, kwa maana hiyo wamiliki wa mabasi wanakwepa kodi
 
Abiria tusiwe kama nyumbu. Unaona gari limejaa, bado unaingia. Mbona magari yapo mengi sana? Haya mazoea ni Tanzania tu. Uganda au Kenya mabasi ya abiria au daladala zao hakuna kusimama. Hapa kwetu sijui kuna mdudu gani. Wakamatwe tu. Ustaarabu ni pamoja na abiria kuketi anaposafiri, hasa safari ndefu!

Sikubaliani nawe kabisa. Nilikuwa na kijana wangu anaenda shule Moshi kutokea Mwanza. Kasafiri na Bus la moja kwa moja toka Mwanza to Moshi na tiketi yake inasema hivyo. Lakini kufika Arusha wale abiria wa Moshi wakaambiwa bus lina matatizo hivyo wahamie lingine la kampuni hiyo hiyo kumalizia safari kwenda Moshi.
Kuingia kwenye Bus na linaondoka wakagundua kuwa wapo kadhaa wamekosa siti, jee wangefanyaje? Jee hapo wakati wanajiuliza cha kufanya ikitokea bus limekamatwa wanastahili kuadhibiwa? Hilo wewe kama Mwandishi wa habari za kiuchunguzi ulipaswa uje na majibu ya kueleweka sio kuja na majibu mepesi kama vile umetokea Malawi na hujui hujuma za wasafirishaji wa nchi hii.
 
Sijui unalaani nini, na unataka nini. Mosi, lile basi la awali wenye nalo walijua wana abiria wangapi. "Walipofaulisha", walijua watu wangapi wanaingia kujaza nafasi kwenye hilo basi la pili. Abiria wa basi bovu walipaswa wakatae usumbufu kwa kupewa gari jingine. Rejea kwenye sheria uone haki na wajibu wa abiria. Taratibu za kisheria ni kwamba kama gari limeharibika, kampuni inawajibika kuwapatia usafiri mwingine. Usafiri mwingine siyo kwamba wasimame katika mabasi mengine au wapandishwe kwenye malori! Abiria waliokuwa pamoja na mwanao walipaswa walalamike SUMATRA ili mmiliki wa kampuni hiyo yenye gari bovu awape usafiri mwingine, hata kama ni kwa kukodi gari. Abiria tukishajua haki na wajibu wetu, wallah malalamiko mepesi ya aina hii yatakoma. Wenye mabasi wanatusumbua na wanachekelea kwa sababu wanatambua kuwa sisi ni mbumbumbu wa haki zetu. Ebu wasiliana na SUMATRA wakupe somo vizuri. Ukishalipata, siku nyingine hutalalamika.
 
Sikubaliani nawe kabisa. Nilikuwa na kijana wangu anaenda shule Moshi kutokea Mwanza. Kasafiri na Bus la moja kwa moja toka Mwanza to Moshi na tiketi yake inasema hivyo. Lakini kufika Arusha wale abiria wa Moshi wakaambiwa bus lina matatizo hivyo wahamie lingine la kampuni hiyo hiyo kumalizia safari kwenda Moshi.
Kuingia kwenye Bus na linaondoka wakagundua kuwa wapo kadhaa wamekosa siti, jee wangefanyaje? Jee hapo wakati wanajiuliza cha kufanya ikitokea bus limekamatwa wanastahili kuadhibiwa? Hilo wewe kama Mwandishi wa habari za kiuchunguzi ulipaswa uje na majibu ya kueleweka sio kuja na majibu mepesi kama vile umetokea Malawi na hujui hujuma za wasafirishaji wa nchi hii.

Soma hapo kwenye bluu na nyekundu. Siyo mnakaa kulalamika tu wakati sheria za kuwalinda abiria zipo.
[h=2]Haki za Abiria[/h]HAKI ZA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA USAFIRI WA NCHI KAVU NA MAJINI KWA MUJIBU WA KANUNI ZA USAFIRISHAJI ZA MWAKA 2007 GN.218/2007

  1. Haki ya kurudishiwa nauli chombo cha usafiri kinapochelewa kuanza safari saa mbili baada ya muda uliopangwa kwenye ratiba na tiketi (Kanuni No. 21-(2) ).
  2. Haki ya kupewa tiketi ndani ya ofisi ya mtoa huduma ya usafiri husika na siyo vinginevyo (Kanuni ya 17-(1p) na ya 24-(1) ).
  3. Haki ya kutonyanyaswa kwa lugha za matusi au vitendo vyovyote kinyume na taratibu au kwa mujibu wa haki za binadamu iwe kwa abiria mtu mzima au mwanafunzi (Kanuni ya 18-(1a,g,h) ).
  4. Haki ya kufikishwa mwisho wa safari yaani kituo husika anakoelekea abiria (Kanuni ya 18-(1d) ).
  5. Haki ya kutosimamishwa ndani ya chombo cha usafiri (kwa mabasi ya mikoani) awapo safarini (Kanuni 17-1f) ).
  6. Haki ya kulipa nauli iliyoidhinishwa na Mamlaka ya SUMATRA na si zaidi ya kiwango husika (Kanuniya 34-1,2,3) ).
  7. Haki ya kutoendeshwa na dereva mmoja (kwa mabasi ya mikoani) zaidi ya saa nane (Kanuni ya 17-1g).
  8. haki ya kulindwa kwa mikanda ya usalama (Passengers seat belt) wakati wote wa safari (Kanuni ya 17-1i).
  9. Haki ya kupata huduma muhimu za usafi, afya na taarifa zinazohusiana na safari yake (Kanuni ya 17-1l,m,n).
  10. Haki ya kutolipia mzigo usiozidi kilogramu ishirini kwa mtu mzima na kilogramu kumi kwa mtoto (Kanuni ya 23-1,2).
  11. Haki ya kurudishiwa nauli yote abiria pale anapohailisha safari saa ishirini na nne au zaidi kabla ya muda wa safari wa chombo husika kama ilivyoainishwa kwenye tiketi na ratiba (Kanuni ya 24-1,2,3).
  12. Haki ya kuhifadhiwa/kutunziwa vifaa au mali ya abiria vinapothibitishwa kusahaulika ndani ya chombo cha usafiri husika (Kanuni ya 38).
  13. Haki ya kurudishiwa nauli pungufu ya asilimia kumi na tano tu ya kiasi alicholipa kama ilivyoainishwa kwenye tiketi endapo abiria atavunja safari ndani ya muda chini ya saa ishirini na nne kabla ya muda wa chombo cha usafiri kuanza safari (Kanuni ya 24-3).
 
Nairobi huwa kuna sheria hiyo na kuna watanzania waliwahi kukamawa kwenye Basi la spider wakitokea tazania kuelekea dar es salaam via Nairobi , watanzania hao walilala sero kwa kosa la kukutwa wamesimama .kwenye bas hilo.

Mkuu tazania kuelekeacdar es salaam ndio wapi huko mkuu?
 
Abiria tusiwe kama nyumbu. Unaona gari limejaa, bado unaingia. Mbona magari yapo mengi sana? Haya mazoea ni Tanzania tu. Uganda au Kenya mabasi ya abiria au daladala zao hakuna kusimama. Hapa kwetu sijui kuna mdudu gani. Wakamatwe tu. Ustaarabu ni pamoja na abiria kuketi anaposafiri, hasa safari ndefu!

KWA NINI SHERIA HIYO HAIFANYI KAZI DAR???
wATU WA KUTOKA KIMARA POST WANASIMAMA LAKINI HAWAKAMATWI
 
Nlipata bahat ya kutembelea nchi moja ambayo mabus yake ya route za mjini aka daladala ni makubwa ya gorofa. Ambayo abiria wanaruhusiwa kusimama floor ya chini ila wanaosimama wasizidi 20. Na wakishafikia capacity waliobaki lazima wasubiri bus lijalo. Ila kwa wenzetu ni sawa coz mabus yana ratiba na ratiba inafuatwa so mtu ana uhakika in 5 or 10 minutes anapata usafiri. Sisi hapa huwezi laumu sana abiria coz bus linalofuata linaweza kuja in two hours. Whether ni la mikoani au daladala. Coz foleni iko na kwa mikoani wanaweza simamishwa na traffic elfu kidogo mpaka kufika kwako ni muda mrefu. Mabadiliko yaanaza na sisi lakini pia system nzima ibadilike

Naona hiyo nchi moja itakua china.
 
Abiria tusiwe kama nyumbu. Unaona gari limejaa, bado unaingia. Mbona magari yapo mengi sana? Haya mazoea ni Tanzania tu. Uganda au Kenya mabasi ya abiria au daladala zao hakuna kusimama. Hapa kwetu sijui kuna mdudu gani. Wakamatwe tu. Ustaarabu ni pamoja na abiria kuketi anaposafiri, hasa safari ndefu!

Siku hizi maandishi yako yapo kibwana mdogo na kishabikishabiki sana.
Nimeanza kukudharau hata lile gazeti nilikuwa naliheshimu nimeacha kulinunua.
 
Hii sheria iko kenya. Umeona basi limejaa usipande subiri lingine.
 
Nairobi huwa kuna sheria hiyo na kuna watanzania waliwahi kukamawa kwenye Basi la spider wakitokea tazania kuelekea dar es salaam via Nairobi, watanzania hao walilala sero kwa kosa la kukutwa wamesimama kwenye bas hilo.

Ni kweli kabisa hii mambo iko Nai..assumption is umeona bus imejaaa haiko na siti..yet ukapanda.so thats your fault.
 
Abiria tusiwe kama nyumbu. Unaona gari limejaa, bado unaingia. Mbona magari yapo mengi sana? Haya mazoea ni Tanzania tu. Uganda au Kenya mabasi ya abiria au daladala zao hakuna kusimama. Hapa kwetu sijui kuna mdudu gani. Wakamatwe tu. Ustaarabu ni pamoja na abiria kuketi anaposafiri, hasa safari ndefu!

yako mengi kwa route ipi mdau
 
Soma hapo kwenye bluu na nyekundu. Siyo mnakaa kulalamika tu wakati sheria za kuwalinda abiria zipo.
Haki za Abiria

HAKI ZA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA USAFIRI WA NCHI KAVU NA MAJINI KWA MUJIBU WA KANUNI ZA USAFIRISHAJI ZA MWAKA 2007 GN.218/2007

  1. Haki ya kurudishiwa nauli chombo cha usafiri kinapochelewa kuanza safari saa mbili baada ya muda uliopangwa kwenye ratiba na tiketi (Kanuni No. 21-(2) ).
  2. Haki ya kupewa tiketi ndani ya ofisi ya mtoa huduma ya usafiri husika na siyo vinginevyo (Kanuni ya 17-(1p) na ya 24-(1) ).
  3. Haki ya kutonyanyaswa kwa lugha za matusi au vitendo vyovyote kinyume na taratibu au kwa mujibu wa haki za binadamu iwe kwa abiria mtu mzima au mwanafunzi (Kanuni ya 18-(1a,g,h) ).
  4. Haki ya kufikishwa mwisho wa safari yaani kituo husika anakoelekea abiria (Kanuni ya 18-(1d) ).
  5. Haki ya kutosimamishwa ndani ya chombo cha usafiri (kwa mabasi ya mikoani) awapo safarini (Kanuni 17-1f) ).
  6. Haki ya kulipa nauli iliyoidhinishwa na Mamlaka ya SUMATRA na si zaidi ya kiwango husika (Kanuniya 34-1,2,3) ).
  7. Haki ya kutoendeshwa na dereva mmoja (kwa mabasi ya mikoani) zaidi ya saa nane (Kanuni ya 17-1g).
  8. haki ya kulindwa kwa mikanda ya usalama (Passengers seat belt) wakati wote wa safari (Kanuni ya 17-1i).
  9. Haki ya kupata huduma muhimu za usafi, afya na taarifa zinazohusiana na safari yake (Kanuni ya 17-1l,m,n).
  10. Haki ya kutolipia mzigo usiozidi kilogramu ishirini kwa mtu mzima na kilogramu kumi kwa mtoto (Kanuni ya 23-1,2).
  11. Haki ya kurudishiwa nauli yote abiria pale anapohailisha safari saa ishirini na nne au zaidi kabla ya muda wa safari wa chombo husika kama ilivyoainishwa kwenye tiketi na ratiba (Kanuni ya 24-1,2,3).
  12. Haki ya kuhifadhiwa/kutunziwa vifaa au mali ya abiria vinapothibitishwa kusahaulika ndani ya chombo cha usafiri husika (Kanuni ya 38).
  13. Haki ya kurudishiwa nauli pungufu ya asilimia kumi na tano tu ya kiasi alicholipa kama ilivyoainishwa kwenye tiketi endapo abiria atavunja safari ndani ya muda chini ya saa ishirini na nne kabla ya muda wa chombo cha usafiri kuanza safari (Kanuni ya 24-3).
Napata mashaka na weledi wako. Nimeuliza nini nawe unajibu nini? Suala hapo ni abiria kuhamishiwa ndani ya gari lingine na akiwa ndani na tayari anagundua hakuna siti kisha polisi wanakamata gari na yeye anahukumiwa.
 
Abiria tusiwe kama nyumbu. Unaona gari limejaa, bado unaingia. Mbona magari yapo mengi sana? Haya mazoea ni Tanzania tu. Uganda au Kenya mabasi ya abiria au daladala zao hakuna kusimama. Hapa kwetu sijui kuna mdudu gani. Wakamatwe tu. Ustaarabu ni pamoja na abiria kuketi anaposafiri, hasa safari ndefu!

Hakuna daladala inayosimamisha
 
Napata mashaka na weledi wako. Nimeuliza nini nawe unajibu nini? Suala hapo ni abiria kuhamishiwa ndani ya gari lingine na akiwa ndani na tayari anagundua hakuna siti kisha polisi wanakamata gari na yeye anahukumiwa.

Ndiyo maana nilianza kusema abiria tusiwe kama nyumbu! Unahamishiwa kwenye gari jingine, unakosa kiti, halafu unabaki humo humo? Kama alikubali kusimama, kwanini asikamatwe? Vinginevyo unataka kusema kondakta na dereva walimteka huyo abiria wako? Umedai kuwa ni mtoto, mtoto anaweza kusafiri mwenyewe bila uangalizi wa mtu mzima? Unasafirisha mtoto kama kifurushi? Kama alishindwa kutambua kosa alilofanyiwa; udhaifu hapo ni wa nani? Nasisitiza, Polisi walikuwa sahihi. Next time huyo mwanao atakuwa amepata akili kuwa kusimama katika basi la abiri kwa safari ndefu ni kosa lenye kustahili adhabu. Watanzania lazima tuyajue haya mambo, na siyo kulalamika tu.
 
mkuu nilishapita hiyo barabara haki ya Mungu nilisali sana na kila mara niliwa na wasi wasi na maisha yangu.

Wezetu wamasai wamejaa kwenye hizo gari then nawakuta na silaa yaani ikuki na mapanga wanayo sasa unaiuliza ikitokea wkipat ajali itakuwaje
 
Hakuna daladala inayosimamisha

Kanuni za Usafirishaji za mwaka 2007 zinazuia magari yanayosafiri kati ya mji na mji kusimamisha abiria. Daladala hakuna zuio, na hata kwenye mradi wa mabasi yaendayo kasi utashuhudia wengi wakiwa wamesimama.
 
Back
Top Bottom