Abiria wa mabus ya Hajees na Mtei wakamatwa

Abiria wa mabus ya Hajees na Mtei wakamatwa

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,760
Mabus ya Mtei na Hajees ( T 122 BZU) yanayofanya safari ya Arusha to Kiteto yamekamatwa kwa kosa la kuzidisha abiria, mbaya zaidi ambacho kimenisukuma kuleta hapa jukwaani ni kutaka kujua kama sheria hii ya kukamata abiria wote waliokuwa wamesimama na kuhukumiwa na polisi je ipo?

Ikumbukwe bus la Hajees namba limekamatwa tangu Jana je nani anawajibu wa kuwahudumia abiria mfano chakula, maji na wale waliokuwa wamekata ticket za kuunganisha bila shaka watakuwa wamechelewa nani anawajibika hata kwa abiria wengine ambao hawana hatia kisa tu Gari, Dereva, konda na abiria waliokuwa wamesimama wamekamatwa.
 
Huko manyara abiria waliozidi kwenye gari wamehukumiwa kifungo cha nje.Ni miezi 6.
 
Abiria tusiwe kama nyumbu. Unaona gari limejaa, bado unaingia. Mbona magari yapo mengi sana? Haya mazoea ni Tanzania tu. Uganda au Kenya mabasi ya abiria au daladala zao hakuna kusimama. Hapa kwetu sijui kuna mdudu gani. Wakamatwe tu. Ustaarabu ni pamoja na abiria kuketi anaposafiri, hasa safari ndefu!
 
hii ni habari njema sana! Najua wenye mabasi watawajibika kwa sababu mara nyingi kama unasafiri watu wawili wanaweza kukatiwa siti moja hasa kama mnapandia vituo viwili tofauti!
 
Nairobi huwa kuna sheria hiyo na kuna watanzania waliwahi kukamawa kwenye Basi la spider wakitokea tazania kuelekea dar es salaam via Nairobi, watanzania hao walilala sero kwa kosa la kukutwa wamesimama kwenye bas hilo.
 
Abiria tusiwe kama nyumbu. Unaona gari limejaa, bado unaingia. Mbona magari yapo mengi sana? Haya mazoea ni Tanzania tu. Uganda au Kenya mabasi ya abiria au daladala zao hakuna kusimama. Hapa kwetu sijui kuna mdudu gani. Wakamatwe tu. Ustaarabu ni pamoja na abiria kuketi anaposafiri, hasa safari ndefu!

Sheria hiyo IPO...
 
Nlipata bahat ya kutembelea nchi moja ambayo mabus yake ya route za mjini aka daladala ni makubwa ya gorofa. Ambayo abiria wanaruhusiwa kusimama floor ya chini ila wanaosimama wasizidi 20. Na wakishafikia capacity waliobaki lazima wasubiri bus lijalo. Ila kwa wenzetu ni sawa coz mabus yana ratiba na ratiba inafuatwa so mtu ana uhakika in 5 or 10 minutes anapata usafiri. Sisi hapa huwezi laumu sana abiria coz bus linalofuata linaweza kuja in two hours. Whether ni la mikoani au daladala. Coz foleni iko na kwa mikoani wanaweza simamishwa na traffic elfu kidogo mpaka kufika kwako ni muda mrefu. Mabadiliko yaanaza na sisi lakini pia system nzima ibadilike
 
Kumbe sheria zipo lakini wasimamizi walizifumbia macho!?
Basi wangelitumia 'busara' ya wakati wa Lyatonga Mrema ya kutoa siku saba angalau wananchi wasio na hatia wajiandae. Kumbuka hawa abiria sio wahujumu uchumi.
 
Watahudumiwa na mmiliki wa gari ila mpaka wawe na ticket halali ya basi hilo.
Hongereni sana Jeshi la polisi
 
Kutokujua sheria hakukuondolei kosa, hongereni trafiki kwa kutimiza wajibu
 
Kwani walilazimishwa kupanda gari hilo?

Ili tuheshim sheria watandikwe faini iwaume ili kesho waheshim utaratibu wa level seat. Maana watu wamezoea kuambiwa na makondo chuchumaeni mbele kuna traffic officer ili tusichelewe, na kondoo kama kawa wanakaliana ili ionekane ni level seat
 
Kule Kenya, Abiria waliozidi/simama ndio wanaopigwa fine, wenyewe na huku huenda sheria inasema hivyo ngoja tusubirie watallam watujuze
 
Back
Top Bottom