Abiria unachelewaje Ndege (check-in) Airport?

Abiria unachelewaje Ndege (check-in) Airport?

Mi nshaachwa na ndege ka mara mbili...ya kwanza ni transportation ilisumbua coz nilitoka mji tofauti kwenda mji mwengine airport ikiisha sehem yenyewe mi mgeni halafu ucku kabla nilikesha harusini na nilitakiwa nirudi nxt day niripoti kazini na hakuna wakunisindikiza kila mtu na hangover zake siku nililaani hio maana ndege ilikuwa haijatake off lkn wakanigomea kabisa ila baadae nilipokuja kuwaeleza kazini kilichojiri walicheka mnooo na pole nyingi!! Kipindi naenda harusini sasa mabegi yote hayakufika ontime sijui waliyakwamisha wapi dah na miparo yote iko mabegini yaani safari ile ilikuwa gundu tupu.Siku nyingine tena ilikuwa ka nuksi zimepandikizana si muda mrefu baada ya trip ya mwanzo nikachanganya masaa nikasoma lisaa limoja nyuma tofauti na muda sahihi....again nikafika airport ndege ipo lkn wakanigomea kucheck in coz ilikuwa boarding time...hii inatokea sana!
 
Mkuu viwanja vya wenzetu kutoka terminal moja kwenda nyingine ni umbali mrefu sana. Sasa ukiwa mgeni unaweza kujikuta unatakiwa ucheck in terminal 3 halafu wewe ukaenda terminal 2. Ukija kushtuka umeachwa. Sometimes upo in the right terminal ila sasa hujui ni counter gani unatakiwa ucheck in na wala hujui ni GATE gani? Wengi pia hujikuta wakiachwa transit kwenye kubadili ndege! Au ukute kuna zile electronic check in mashine , mwenzangu na mie umetoka "sitimbi" huna ujualo na kila mtu yuko busy halafu lugha ni gongana hata ukisemeshwa kile kingereza cha mbali na wale wasaidizi huelewi. Mpaka ukija kamilisha taratibu zote ndege imeshakuacha
ha ha ha loool lkn kweli teh.....
 
kwani foleni zimeanza leo??unasahauje passport??kuna vitu vingine huwez kumwambia mtu akakuelewa..eti nimesahau
 
halafu pia unakuta mtu ana mizigo mingi utadhani kabeba sayari...lazma uachwe tu
 
Mpaka sasa sijaona aliyetoa sababu ya maana ya kuchelewa airport zaidi ya uzembe. Eti umesahau passport, huo tuuiteje?
 
Siku ya kwanza kupanda ndege ,wale maafisa wanaokaaga kwenye chumba cha pembeni hapa baada ya kupigiwa mhuri kwenye passport,waliniita na kuanza kuniuliza maswali ,ilikua kidogo nichelewe.kumbe walikua wanataka hela, dooh!! Nikatoa ef kumi nikawapa,wakaniambia haya nenda.
 
Jamaa wa immigration pale airport/JNIA wana njaa sijapata kuona
 
Luna haka ya kufundishana name kupeana uzoefu kwa mlio pata fursa ya kutumia viwanja vikubwa vya kimataifa haswa vya nchi za magharibi mzee Wangu husafiri Mara kadhaa hutueleza namna uwanja wa Amsterdam ulivyo mkubwa na busy sana. Hapo nasikia possibility ya kupotea name kuachwa na ndege in kubwa sana pana hitaji umakini sana na kutoona aibu katika kuuliza. Tunaomba darasa kwa wazoefu
 
ukiona noma kuuliza imekula kwako
mfano Dubai unakuta services provider wao wakwanza kukuuliza
 
Hujui kuchelewa ndege ni mojanya style za maisha .

Watu wengine huchelewa Ndege maksudi ....
 
sawa sawa kabisa.......hasa hao wanaotoa boarding pass bila gate no.......halafu ukalitafutie mbele huko.......kama hujawahi kusafiri utafurahi.......hii kweli ni sababu madhubuti ya kuachwa na ndege...........

Preta, I think these days all international flight wanaweka kabisa gate no once you check in either in person or online lakini kama ni hizi local, then hapo ndio balaa. Mie nadhani ni uzembe tu ndio huwa unatusumbua!
 
Luna haka ya kufundishana name kupeana uzoefu kwa mlio pata fursa ya kutumia viwanja vikubwa vya kimataifa haswa vya nchi za magharibi mzee Wangu husafiri Mara kadhaa hutueleza namna uwanja wa Amsterdam ulivyo mkubwa na busy sana. Hapo nasikia possibility ya kupotea name kuachwa na ndege in kubwa sana pana hitaji umakini sana na kutoona aibu katika kuuliza. Tunaomba darasa kwa wazoefu

Mkuu siku hizi ni vigumu sana kupotea unless hujui kusoma, kwanza kwenye ticket yako inakuonyesha gate yako na ukifika tu airport kuna screen kibaao zinaonyesha status za ndege zote and where to board from, pia kuna maelekezo kibao on how to get from one gate to the other.
 
Kama umeshacheck-in kuachwa ni ngumu (kwa baadhi ya Airport) watakutafuta mpaka upatikane
 
Preta, I think these days all international flight wanaweka kabisa gate no once you check in

Ni kweli mkuu lakini kitu kama hiki nilikutana nacho KIA.........ndio maana nikatoa mchango huo............
 
KIA nako mtu unahitaji namba ya gate kwani zipo ngapi?
 
Mwingine anakwambia anaenda kupanda ndege hivyo hawezi kupanda boda. Ukienda airport shurt upande tax.

..afuu hamna usafiri rahisi wa kudash in a rush to airport kama boda boda yaani!, tena tusiobebaga vifurushi wala misanduku huwa tunagongelea dk 10 za mwisho, siku hizi bila pressure yaani nachagua boxer namuelekeza kabisa hamna haja ya kukuruka barabarani ananiacha BP pale natembea tu kama naenda kupiga picha JNIA kumbe ndio nasepa hivyo.
 
Mkuu viwanja vya wenzetu kutoka terminal moja kwenda nyingine ni umbali mrefu sana. Sasa ukiwa mgeni unaweza kujikuta unatakiwa ucheck in terminal 3 halafu wewe ukaenda terminal 2. Ukija kushtuka umeachwa. Sometimes upo in the right terminal ila sasa hujui ni counter gani unatakiwa ucheck in na wala hujui ni GATE gani? Wengi pia hujikuta wakiachwa transit kwenye kubadili ndege! Au ukute kuna zile electronic check in mashine , mwenzangu na mie umetoka "sitimbi" huna ujualo na kila mtu yuko busy halafu lugha ni gongana hata ukisemeshwa kile kingereza cha mbali na wale wasaidizi huelewi. Mpaka ukija kamilisha taratibu zote ndege imeshakuacha
Hii inaweza kutokea ila viwanja vingi vya ndege vya kimataifa kama unajua kiingereza sehemu nyingi zinajieleza vizuri kabisa. Ni vigumu sana kupotea kwa kweli labda kama hujui kusoma na kuuliza (Hapa wengi pia wanaangukia maana ujuaji mwingi hawataki kuonesha ushamba). Kwa mfano mimi kwa mara ya kwanza niliposafiri kwenda nje ya nchi nilikuwa nauliza kila kitu na sikupotea kwa kweli.
 
Back
Top Bottom