BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Leo Novemba 28, 2023 sisi Wakazi hasa wa Kigamboni tumepata changamoto ya Kivuko.
Yaani leo kivuko kinachofanya kazi ni MV Kazi tu, kingine wanasema ni kibovu, watu wanachelewa makazini, Azam ameleta kivuko kidogo kimoja nacho ni kama kinazidiwa kutokana na idadi ya watu wanaohitaji kuvuka.
Najiuliza kwa nini wasimruhusu Azam aweke vyote viwili kisha MV Kazi ipakie magari tu?
Hali hii ikiendelea hivi, ikifika jioni tutakaokuwa tunavuka kutoka Kivukoni kwenda Kigamboni hapo ndipo shughuli itakuwa kubwa.
Changamoto kama hizi zimekuwepo kwa muda mrefu tangu kuanza kwa mwaka huu, ile pantoni nyingine ikienda kwenye matengenezo kunakuwa na usumbufu mkubwa, foleni za magari zinakuwa ndefu, kwa ufupi ni kero juu ya kero.