Kivukoni - Kigamboni maamuzi magumu yafanyike; Wakazi watafute mbadala wa kutumia Kivuko maana kinafanya kazi kimoja

Bayebe

Senior Member
Jan 31, 2014
152
198
MH. RAIS SAMIA ANAHITAJI WATENDAJI WA DHATI KIVUKONI KIGAMBONI NA MANISPAA KWA UJUMLA

Umati ni mkubwa.

Kivuko kimoja tu ndio kinachofanya kazi

Muda wa kusubiri ni zaidi ya Saa moja
 
Ndugu zangu wa Kigamboni, kama unataka kuja mjini asubuhi hii ni bora ukapitia darajani mana hapa ferry kuna panton moja tu ndo inayofanya kazi
 
Hawa watu hapo Kivukoni tushasema hawako serious. Siku chache zilizopita nilisikia wamefukuzwa watu hapo kwa uzembe. Leo nimesikia redioni kuwa kulikuwa na pantoni moja ndogo tu inavusha watu hakuna magari kuvuka! Mpaka watu wapoteze maisha ndio hatua za maana zitachukuliwa.
 
shida hapo panashibisha matumbo ya watu ndo maana watu wananufaika kupitia shida za wananchi.. wangeweka hata floating bridge kama ya lukonimombasa ila wstakosa ulaji.. floating bridge kwa ajili y a wapita miguu na baiskeli..linafunga na kufunguka meli zinapopita.. cause hapo ni less than 2km walk
 
Back
Top Bottom