Huyu baba amenisikitisha sana juzi, Private wanazozungumzia ni zipi? Maana ninao ushahidi wapo watoto wa vigogo wengi wanasoma Private then wanakuja kuramba 100% ya Loan! Nchi hii haitaisha double standard Ng'oooo hasa kwa sababu mwenye mamlaka makubwa ndiye anaongoza hiyo double standard!!!
Bodi ya mikopo na Serikali inapaswa kuondoa hicho kigezo na ibaki na sifa ya ufaulu wa mwanafunzi kulingana na fani anayoenda kusomea. Uasili wa mtoto katokea wapi, hautusaidii kama nchi, tunapaswa kulenga ufaulu kama sifa watoto wapige kitabu...labda wa Serikali wapewe kigezo maalum kama kushushiwa sifa ya kigezo cha ufaulu...kama private A basi wao iwe B. Ila kimwacha Mtoto kwenda chuo Kikuu na kapata AAA kwa kuwa tuu katoka private school ....ni kichaaa na dunia itatushangaaa...kweli kweli....akili inasakwa duniani kuliko dhahabu....
Tatizo ni watu kufikiria kuwa watu wanawapeleka watoto shule za private kwa kuwa wana pesa nyingi. Hawajui kuwa kuna wazazi wanajinyima sana ili kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata elimu nzuri. Shule za serikali zimetuangusha. Kila mtu anajua na Rais anajua.
Anyway, hii ya kuja na affirmative action Tanzania ni kichekesho cha mwaka!! Ni nani anataka kuclaim kuwa kulikuwa na disadvantaged group siku za nyuma hapa Tanzania tena baada ya Uhuru!? It doesn't make sense!!
wa "Kama ulisoma shule ya binafsi hupati mkopo" ili wazazi wajipange mapema na wajue kuwa mtoto akisoma private school hapati mkopo kutoka bodi ya mikopo.
Kama kafilisika au kafariki kinachohitajika ni uthibitisho wa mamlaka husika. Tatizo liko wapi? Kwanza ni kwa faida ya mwanafunzi mwenyewe kwani atawajibika kuulipa huo mkopo plus interest ndani ya miaka 3 baada ya kuhitimu.
Hoja ya kuwanyima mkopo wanafunzi waliosoma private schools ni hoja ya ovyo. Ningeelewa wangesema wananyimwa stipend. Mkopo ni stahiki ya kila mmoja.
Kingine: Kwani mtu kubadilika toka kuwa mtoto (tegemezi) hadi mtu mzima (anayejitegemea) huwa ni miaka mingapi? Nilidhani mzazi ana jukumu la kisheria kum-support mtoto wake; na sio baada ya hapo.
Kumbuka kwa private sec schools,unapolipa say,mil 2 kwa term moja i.e.4 mil kwa mwaka, hiyo ina-cover gharama zote za chakula,mavazi,usafiri,tuition fee etc.
Mkuu usijitoe ufahamu, hiyo 1.5 ya chuo ni ada (school tuition fee) pekee bado madudu mengine kibao pesa kama hiyo au zaidi.
mkosoe Nondo ktk siasa zake zingine ila sio kwa hili la mikopo. dogo yupo sahihi kabisa.
hali ya kiuchumi hubadilika. Kuna kupunguzwa kazini, kampuni yako au uliyo ajiliwa kufilisika, kuugua n.k. vinaweza kupelekea mzazi kushindwa kuendelea kumlipia mtoto elimu ya juu kam private.
Pia ieleweke huu ni mkopo atakae kopeshwa atalipa, na wazazi wote wanalipa kodi ubaguzi uwe kwenye vigezo vya kupata admission na vipengele vingine. Tuache mawazo ya kichawi chawi.
Ujinga (nitafsiriwe kuwa situkani) hauwezi kutuisha watz. Ukishindwa kusoma na kuelewa andiko fupi kama hili hata unakuja na hoja dhaifu hivi ni nini tena kama si ujinga? Soma na uielewe hoja ya mwandishi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini (TSNP) Abdul Nondo amefunguka na kusema kuwa kigezo cha bodi ya mikopo kutoa mikopo kwa kuzingatia tu wanafunzi waliosoma shule za serikali na kuwabagua wale waliosoma shule za private si sawa kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwakosesha haki watu kusoma.
Abdul Nondo amesema hayo siku moja baada ya kauli ya Rais Magufuli kusema kuwa bodi ya mikopo haiwezi kutoa mikopo kwa wanafunzi ambao awali walionekana kusoma katika shule za binafsi na kudai kuwa watu hao wanauwezo hata wa kusomesha na wazazi wao ndiyo maana waliweza kusomeshwa katika shule binafsi walipokuwa wakisoma.
"Mara ya kwanza kabisa, niliwahi sikia kauli ya namna hiyo kwa Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarishi akisema kama umesoma private school hupati mkopo. Kauli hii tuliipinga vikali, kipindi hicho na tukasema sio fair sababu gharama za chuo ni kubwa (Ada, hela ya kula ,copy, usafiri,hela ya malazi, hela ya mafunzo kwa vitendo field). Ni tofauti kabisa na fedha ya ada shule ya private laki 8, au mil 1 ambayo pia watu husoma kwa ada hiyo private. Kuwanyima mkopo ni kuwakatishia ndoto zao kabisa"
Nondo aliendelea kusema kuwa sababu nyingine ni kuwa uwezo wa mzazi unaweza kubadilika badilika inawezekana kipindi cha nyuma alikuwa na uwezo wa kulipia gharama lakini kipindi mtoto anaingia chuo labda mzazi amepatwa na magonjwa ya kudumu, uchumi umeyumba kiasi cha kushindwa kumudu gharama hizo jambo ambalo linapelekea wanafunzi wengine kukosa haki ya kusoma elimu ya juu.
"Mfano kipindi mtoto akiwa anasoma 'private' mzazi alikuwa na uwezo wa kulipa, kipindi mtoto anaingia chuo baba au mzazi amepata magonjwa, ameparalyze, amefilisika, kumnyima mkopo mtoto huyu ni kumkatishia malengo yake. Pia tulihoji juu ya kama mtoto amesoma kwa kudhaminiwa inakuwaje, kuna wanaodhaminiwa kusoma private schools na mashirika binafsi, watu binafsi, na husomeshwa shule tuu sio chuo, baadaye hutelekezwa chuo wajitegemee. Hii bodi ya mikopo walisema wataweka kipengele kuambatanisha vielelezo vya udhamini ila huwa ni geresha tuu huwa hawatoi hata uambatanishe ndio maana sio sahihi kutoa mkopo kwa kigezo cha u private schools, au u government schools siyo haki"
"Tulihoji pia wapo waliosoma kwa kurUdia mitihani kutafuta 'credits' mara nyingi hawa huwekwa katika kundi la private schools, wapo QT (qualified Tests), wapo diploma wote hawa huwa termed as private schools. Kuwanyima mkopo kwa vigezo hivi ni kupoteza ndoto zao. Kigezo cha kutoa au kutotoa mkopo kwa kuangalia ulisoma private au government sio kigezo sahihi. Kime katisha ndoto za wanafunzi wengi saana sababu hakitoi majibu halisi ya uwezo wa mwanafunzi kustahimili gharama"
Mbali na hilo Abdul Nondo amesema bodi ya mikopo sasa imekuwa ikikusanya marejesho ya mikopo kuliko kipindi chote kama ambavyo wao wenyewe wamekuwa wakisema hilo hivyo amewaomba kigezo hicho cha kuangalia mwanafunzi alisoma shule gani na kumpa mkopo huku wengine wakikosa mkopo kutokana na shule walizowahi kusoma siyo haki na kuwa kitendo hicho ni kukatisha ndoto za watu kusoma elimu ya juu.
"Hakuna kipindi bodi ya mikopo wanakusanya makusanyo na marejesho Kama kipindi hiki, tuwasii bodi ya mikopo hiki kigezo hakifai. Kama bodi ya mikopo wataamua kukitumia kama kigezo cha kukosa mkopo, basi tunawaomba waandike katika muongozo wao wa 2018/2019 .Wakiongeze kuwa "Kama ulisoma shule ya binafsi hupati mkopo" ili wazazi wajipange mapema na wajue kuwa mtoto akisoma private school hapati mkopo kutoka bodi ya mikopo. Itasaidia ikifafanuliwa hivyo"
Hoja kubwa kubwa mikopo hiyo inatokana na kodi za wananchi bila kujali nani kalipa. Kama ndivyo serikali isiwatoze kodi yoyote wazazi wenye watoto wanaosoma private.
Chuo ishu siyo ada peke yake ila gharama za maisha kila siku ndio tabu. Meals and accomodation, stationery , field and research and many more. Wawakopeshe hizo gharama nyingine za kila siku ada tutawalipia
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.