Abdul Nondo afunguka kuhusu bodi ya mikopo

Abdul Nondo afunguka kuhusu bodi ya mikopo

Nachojua watu wengi waliokulia kwenye Dimbwi la umasikini wanakua na roho mbaya sana pale wao wanapopata nafasi ya kutoa ili wengine wafanikiwe kama wao ni ngumu wanataka wote wapitie maisha aliyopita yeye ..Mbeki alisema umasikini ni ugonjwa kama magonjwa mengine tuukomeze kwa kutoa Elimu ndio itakayowaponya alipingwa sana sana na Bunge... Maana walijua Elimu watapewa watu weusi na ndio wengi hawana Elimu...sasa Bongo mtu anajisifia kujenga Reli na kuacha kusomesha kabisa akili za wapi hizo...
 
Ila tuongee ukweli kama umeweza kulipa zaidi ya 2.5 kwa miaka 7 ongeza 4 ongeza 2 halafu leo 1.5 ya chuo itakushindaje miaka 3
Sidhani kama unawaza sawasawa, kuna factors kibao zinazoweza kumfanya mzazi/mlezi kushindwa kumsomesha mtoto
ie kifo, kustaafu, kutokuwa tena ktk ajira, kipato kupungua au kufa kwa biashara etc, lkn kwa mtu anaewaza kama wewe huwezi kuona hayo.
 
Ila tuongee ukweli kama umeweza kulipa zaidi ya 2.5 kwa miaka 7 ongeza 4 ongeza 2 halafu leo 1.5 ya chuo itakushindaje miaka 3
Inaonekana ulishawahi dumbukia kisimani yaani watu tukonyumbani kisa mikopo wee unaongea hivi acha utani na maisha ya watu
 
Nadhani tunachanganya mambo. Kijana anayeingia Chuo Kikuu ni mtu mzima tayari, ana walau miaka 18. Hawezi akaendelea kuwa tegemezi kwa mzazi wake. Anawajibika kujiendeleza, anao umri wa kutosha kumshitaki na kushitaki. Kufikia umri huo mzazi hana tena majukumu na mtoto huyo. Kama alikuwa na kipato, mzazi atakuwa amekaribia kuchoka na anastahili kustaafu na kuonja maisha yake.
Sera inayotengenezwa hapa Tanzania ni kinyume kabisa na kinachofanyika mataifa mengine. Yumkini baada ya miaka 18, anastahili kupewa nyumba na serikali kama upo utaratibu wa kusaidia wananchi, kupewa kazi au kuchukua mkopo akasome. Tunachokifanya ni kuwalundika mibaba na mimama iliyopevuka kwa wazazi wao ambao muda umeshaisha kwa maana ya uwezo wa kifedha.
Ni bahati mbaya sana kuwabagua wale ambao waliosoma private (tena mara nyingi kwa shida kweli, wakirudishwa mara kwa mara kwa kukosa ada). Ni kama ile sera ya kibaguzi kuwanyima wavulana nafasi ya kuendelea masomo chuo kikuu mara baada ya form 6 kwa kuwa tu wavulana wa zamani walikuwa wengi katika shule kuliko wasichana. Huyu unayembagua hahusiki, kila kitu kinapaswa kuangaliwa kwa uhalisia wake!

">miaka 18". Yes, ni mtu mzima! serikali iwawezeshe, kupitia kodi zetu na si jukumu tena la mzazi!
 
Kijana ana mawazo mazuri kuliko yule jamaa mwenye PHD.



Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini (TSNP) Abdul Nondo amefunguka na kusema kuwa kigezo cha bodi ya mikopo kutoa mikopo kwa kuzingatia tu wanafunzi waliosoma shule za serikali na kuwabagua wale waliosoma shule za private si sawa kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwakosesha haki watu kusoma.

Abdul Nondo amesema hayo siku moja baada ya kauli ya Rais Magufuli kusema kuwa bodi ya mikopo haiwezi kutoa mikopo kwa wanafunzi ambao awali walionekana kusoma katika shule za binafsi na kudai kuwa watu hao wanauwezo hata wa kusomesha na wazazi wao ndiyo maana waliweza kusomeshwa katika shule binafsi walipokuwa wakisoma.

"Mara ya kwanza kabisa, niliwahi sikia kauli ya namna hiyo kwa Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarishi akisema kama umesoma private school hupati mkopo. Kauli hii tuliipinga vikali, kipindi hicho na tukasema sio fair sababu gharama za chuo ni kubwa (Ada, hela ya kula ,copy, usafiri,hela ya malazi, hela ya mafunzo kwa vitendo field). Ni tofauti kabisa na fedha ya ada shule ya private laki 8, au mil 1 ambayo pia watu husoma kwa ada hiyo private. Kuwanyima mkopo ni kuwakatishia ndoto zao kabisa"

Nondo aliendelea kusema kuwa sababu nyingine ni kuwa uwezo wa mzazi unaweza kubadilika badilika inawezekana kipindi cha nyuma alikuwa na uwezo wa kulipia gharama lakini kipindi mtoto anaingia chuo labda mzazi amepatwa na magonjwa ya kudumu, uchumi umeyumba kiasi cha kushindwa kumudu gharama hizo jambo ambalo linapelekea wanafunzi wengine kukosa haki ya kusoma elimu ya juu.

"Mfano kipindi mtoto akiwa anasoma 'private' mzazi alikuwa na uwezo wa kulipa, kipindi mtoto anaingia chuo baba au mzazi amepata magonjwa, ameparalyze, amefilisika, kumnyima mkopo mtoto huyu ni kumkatishia malengo yake. Pia tulihoji juu ya kama mtoto amesoma kwa kudhaminiwa inakuwaje, kuna wanaodhaminiwa kusoma private schools na mashirika binafsi, watu binafsi, na husomeshwa shule tuu sio chuo, baadaye hutelekezwa chuo wajitegemee. Hii bodi ya mikopo walisema wataweka kipengele kuambatanisha vielelezo vya udhamini ila huwa ni geresha tuu huwa hawatoi hata uambatanishe ndio maana sio sahihi kutoa mkopo kwa kigezo cha u private schools, au u government schools siyo haki"

"Tulihoji pia wapo waliosoma kwa kurUdia mitihani kutafuta 'credits' mara nyingi hawa huwekwa katika kundi la private schools, wapo QT (qualified Tests), wapo diploma wote hawa huwa termed as private schools. Kuwanyima mkopo kwa vigezo hivi ni kupoteza ndoto zao. Kigezo cha kutoa au kutotoa mkopo kwa kuangalia ulisoma private au government sio kigezo sahihi. Kime katisha ndoto za wanafunzi wengi saana sababu hakitoi majibu halisi ya uwezo wa mwanafunzi kustahimili gharama"

Mbali na hilo Abdul Nondo amesema bodi ya mikopo sasa imekuwa ikikusanya marejesho ya mikopo kuliko kipindi chote kama ambavyo wao wenyewe wamekuwa wakisema hilo hivyo amewaomba kigezo hicho cha kuangalia mwanafunzi alisoma shule gani na kumpa mkopo huku wengine wakikosa mkopo kutokana na shule walizowahi kusoma siyo haki na kuwa kitendo hicho ni kukatisha ndoto za watu kusoma elimu ya juu.

"Hakuna kipindi bodi ya mikopo wanakusanya makusanyo na marejesho Kama kipindi hiki, tuwasii bodi ya mikopo hiki kigezo hakifai. Kama bodi ya mikopo wataamua kukitumia kama kigezo cha kukosa mkopo, basi tunawaomba waandike katika muongozo wao wa 2018/2019 .Wakiongeze kuwa "Kama ulisoma shule ya binafsi hupati mkopo" ili wazazi wajipange mapema na wajue kuwa mtoto akisoma private school hapati mkopo kutoka bodi ya mikopo. Itasaidia ikifafanuliwa hivyo"
 
Dogo unapoint. Ila kumbuka unayejibizana naye sio JK. Atakupelekwa ka GF wako tena. Shaur ako

tapatalk_1519827230709.jpeg
 
Ila tuongee ukweli kama umeweza kulipa zaidi ya 2.5 kwa miaka 7 ongeza 4 ongeza 2 halafu leo 1.5 ya chuo itakushindaje miaka 3

mkuu kumbuka kuna kustahafu,magonjwa,kufilisika na umauti kwa mzazi/mlezi kwa mustakabali huo vipi hapo mkuu...??
mtoto akose haki ya msingi hata kama ana vigezo vya kupata mkopo...??... wasomi wetu wanafikirije jamani..kwa uchache huo jamani...??
 
Ila tuongee ukweli kama umeweza kulipa zaidi ya 2.5 kwa miaka 7 ongeza 4 ongeza 2 halafu leo 1.5 ya chuo itakushindaje miaka 3
utakuta anaeongea hivi ni darasa la saba kama Musukuma au form four failure tu!!!! KAMA UMEFIKA CHUO KIKUU HUWEZI KUPOST KAMASI KAMA HIZI HUMU.
 
Ila tuongee ukweli kama umeweza kulipa zaidi ya 2.5 kwa miaka 7 ongeza 4 ongeza 2 halafu leo 1.5 ya chuo itakushindaje miaka 3
MTOCHORO :
  1. Uwezo wa mtu kulipia gharama unaweza kukomea popote, na sababu za kushindwa zimetajwa kama uchumi kuyumba (kuharibikiwa biashara, kilimo, kazi nk), magonjwa ya kudumu, kifo cha mzazi/wazazi.
  2. Kumbuka anayepewa mkopo ni mtoto, siyo mzazi. Huko private mtoto alisomeshwa na mzazi, katika university mtoto anajisomesha kwa mkopo ambao ataurejesha
  3. La kuzingatia sana, hii pesa haitolewi bure, ni mkopo tena wenye riba (wameipa majina tofauti lakini ni riba tu) kubwa sana.
 
MTOCHORO.
Ki ukweli anachosema Nondo ni kweli kwa mfano Mzuri mdogo wangu leo hii anafanya mtihani wa form six private na form four kasoma private ila sasa ukweli ni kwamba anayemsomesha kastaafa kitambo sema aliongezewa mda wa kazini kutokana na mahitaji na mafao alishalipwaga.
pili kuna jamaa yangu wa karibu sana alifiwa na Wazazi wake ndani wote ndani ya miaka 2 ambao ndio nguvu lakini watoto before death walisoma shule za private lakini leo hii hata hela ya ada yao ya A level ni shida.
kwahiyo wa ndugu life can change any time
 
Ila tuongee ukweli kama umeweza kulipa zaidi ya 2.5 kwa miaka 7 ongeza 4 ongeza 2 halafu leo 1.5 ya chuo itakushindaje miaka 3
Nahisi hutambui kuwa hata wewe huijui kesho yako, kuna kustaafu na mafao kuchelewa, kuna kutumbuliwa kimakosa, kuna kuvunjiwa mjengo wako bila fidia na hivyo kuuawa kiuchumi n.k
IMG_20180507_070912_135.jpg
 
Ila tuongee ukweli kama umeweza kulipa zaidi ya 2.5 kwa miaka 7 ongeza 4 ongeza 2 halafu leo 1.5 ya chuo itakushindaje miaka 3
Mbona majibu ya swali lako ameyatoa bwana Nondo au hujasoma.

Kama wazazi wamefilisika, wanaumwa, alisomeshwa kwa ufadhili, waliorudia mitihani, waliotoka diploma.
 
Porojo tupu wenye uwezo wanajulikana tu kwa historia ya toka Primary
Na mwenye uwezo hawezi kupigania mkopo, wakina sie ndio tunalia lia.

Muda mwingine uchoshe ubongo wako kwa kuufikirisha zaidi.
 
Kama shule za umma ni mbaya au hazikidhi viwango acha na pesa zao ziwe mbaya tu.kopeni kwingineko bhana.
 
Ila tuongee ukweli kama umeweza kulipa zaidi ya 2.5 kwa miaka 7 ongeza 4 ongeza 2 halafu leo 1.5 ya chuo itakushindaje miaka 3
Hakuna kitu ninacho kipenda kama ukweli na uhalisia.Mm ni mwlm mdogo wangu alpo maliza drs la saba nikaona shule ya kata hataambulia chochote,nikampeleka private school ada sh laki nane day mpaka form four.Sasa ukiniambia mm nina hela ya kulipia gharama ya chuo kikuu ada,pesa ya kula,marazi,field ,stationary na nauli za hapa na pale utauwa uongo.Tuacha ushabiki tutumie akili zetu vzr na mungu atuongoze katka kufikiri.Tuwe na huruma kwa binadam wenzetu maisha ni mafupi mnoo kuliko kitu chochote.
 
Back
Top Bottom