Chuo ishu siyo ada peke yake ila gharama za maisha kila siku ndio tabu. Meals and accomodation, stationery , field and research and many more. Wawakopeshe hizo gharama nyingine za kila siku ada tutawalipia
kusomesha mtoto private si kwamba unauwezo mkubwa wa kifedha wengine hali zao ni ngumu lakini dhamira na malengo yao mtoto apate elimu bora.
mfano kuna mama shughuli yake ilikua ususi hakua na mume, mtoto wake akafaulu shule flani ya kata ambayo tangu kuanzishwa kwake wanafunzi waliofaulu sana nidiv4 tena m1 au wawili yani ni ziro tupu. na yote iyo inachangiwa na uhaba wa walimu mazingira mabovu ya shule na changamoto nyingine nyingi, izi shule zingekua na mazira rafiki kwa mwanafunzi wazazi wachache wangepeleka watoto prvt
alifatilia uhamisho bila mafanikio alitafuta pesa, alijima mengi yule mama adi kula nyumbani ilikua inasumbua ili kijana apate shule. zilipatikana pesa yule kijana akapata shule private akamaliza na kupata dvsn1, ambapo ndio lilikua lengo la uyo mama na ndoto zake zikawa kweli.
je kijana uyo akifika chuo kikuu alafu akakosa mkopo kwa kigezo cha kusoma prive itakua sawa? huoni serikali ilikua na jukumu la kumsaidia uyo mama ambapo malazi, chakula na stationer gharama kubwa kuliko ada.
Nadhani tunachanganya mambo. Kijana anayeingia Chuo Kikuu ni mtu mzima tayari, ana walau miaka 18. Hawezi akaendelea kuwa tegemezi kwa mzazi wake. Anawajibika kujiendeleza, anao umri wa kutosha kumshitaki na kushitaki. Kufikia umri huo mzazi hana tena majukumu na mtoto huyo. Kama alikuwa na kipato, mzazi atakuwa amekaribia kuchoka na anastahili kustaafu na kuonja maisha yake.
Sera inayotengenezwa hapa Tanzania ni kinyume kabisa na kinachofanyika mataifa mengine. Yumkini baada ya miaka 18, anastahili kupewa nyumba na serikali kama upo utaratibu wa kusaidia wananchi, kupewa kazi au kuchukua mkopo akasome. Tunachokifanya ni kuwalundika mibaba na mimama iliyopevuka kwa wazazi wao ambao muda umeshaisha kwa maana ya uwezo wa kifedha.
Ni bahati mbaya sana kuwabagua wale ambao waliosoma private (tena mara nyingi kwa shida kweli, wakirudishwa mara kwa mara kwa kukosa ada). Ni kama ile sera ya kibaguzi kuwanyima wavulana nafasi ya kuendelea masomo chuo kikuu mara baada ya form 6 kwa kuwa tu wavulana wa zamani walikuwa wengi katika shule kuliko wasichana. Huyu unayembagua hahusiki, kila kitu kinapaswa kuangaliwa kwa uhalisia wake!
stroke Yale niliyokwambia Jana ...ndio Yale Yale aliyo yaongea nondo leo "" naweza kusema kuwa kama Jamaa ni member wa JF basiii alichukua mawazo yangu baada ya kupitia ule Uzi kisha akaongezea na Mawazo yake ili kutengeneza hoja iliyoshiba zaidi ....."" Jana nilikwambia hoja za msingi mnooo...moja wapo ikiwa nihiyo ya uwezekano wa kufilisika kwa wazazi "" waliokuwa wana wasomesha Watoto wao shule za private "" pia niligusia mpak wazazi waliofariki "" wazazi ambao wakati walipokuwa hai walikuwa wanawasomesha Watoto wao shule za private "" baada ya wazazi kufikwa na mauti Watoto wamejikuta hawawezi kuendlea na shule hzo kutokana na ukuu wa gharama wa shule husika....
lakini ukaleta u UVCCM nakupinga...nashukuru Mungu hii hoja imekuja tena mezani ."" haya tirilika nayo ...hahaa
kusomesha mtoto private si kwamba unauwezo mkubwa wa kifedha wengine hali zao ni ngumu lakini dhamira na malengo yao mtoto apate elimu bora.
mfano kuna mama shughuli yake ilikua ususi hakua na mume, mtoto wake akafaulu shule flani ya kata ambayo tangu kuanzishwa kwake wanafunzi waliofaulu sana nidiv4 tena m1 au wawili yani ni ziro tupu. na yote iyo inachangiwa na uhaba wa walimu mazingira mabovu ya shule na changamoto nyingine nyingi, izi shule zingekua na mazira rafiki kwa mwanafunzi wazazi wachache wangepeleka watoto prvt
alifatilia uhamisho bila mafanikio alitafuta pesa, alijima mengi yule mama adi kula nyumbani ilikua inasumbua ili kijana apate shule. zilipatikana pesa yule kijana akapata shule private akamaliza na kupata dvsn1, ambapo ndio lilikua lengo la uyo mama na ndoto zake zikawa kweli.
je kijana uyo akifika chuo kikuu alafu akakosa mkopo kwa kigezo cha kusoma prive itakua sawa? huoni serikali ilikua na jukumu la kumsaidia uyo mama ambapo malazi, chakula na stationer gharama kubwa kuliko ada.
stroke Yale niliyokwambia Jana ...ndio Yale Yale aliyo yaongea nondo leo "" naweza kusema kuwa kama Jamaa ni member wa JF basiii alichukua mawazo yangu baada ya kupitia ule Uzi kisha akaongezea na Mawazo yake ili kutengeneza hoja iliyoshiba zaidi ....."" Jana nilikwambia hoja za msingi mnooo...moja wapo ikiwa nihiyo ya uwezekano wa kufilisika kwa wazazi "" waliokuwa wana wasomesha Watoto wao shule za private "" pia niligusia mpak wazazi waliofariki "" wazazi ambao wakati walipokuwa hai walikuwa wanawasomesha Watoto wao shule za private "" baada ya wazazi kufikwa na mauti Watoto wamejikuta hawawezi kuendlea na shule hzo kutokana na ukuu wa gharama wa shule husika....
lakini ukaleta u UVCCM nakupinga...nashukuru Mungu hii hoja imekuja tena mezani ."" haya tirilika nayo ...hahaa
hahaa hapana mkuu "" siye mimi "" anyway " niliyaona Yale majibu yako " ijapokuwa kwa serikali hii sidhani kama kuna wakuwa na mawazo kama yle yakwako""na kama wapo naimani watakwama kwenye utekelezaji
Ni kweli lakini alipokuwa analipa kiasi hicho alikuwa anaongeza au anapunguza! Mtu anaweza kuwa amejipanga na kudunduliza kiasi hicho kwa kujinyima. Hivyo siyo vyema kutoa mkopo kwa kigezo cha shule aliyosoma mhusika.
hao mapopoma achana nao ...kuna watu wana amua kujidhiki kusomesha Watoto wao private ili wapate elimu bora "" wakiwa O LEVEL .A.LEVEL wanakubali kusurubika katika kipindi chote cha miaka 6 wakiwa na imani kuwa Watoto wao wakifika chuo serikali itaaapokea kijiti kwa kuwapatia mikopo "" halafu leo serikali inakuja nakuali hii kwa wananchi wake niwazi serikali itakuwa inafurahi mnooo pindi inapoona wananchi wake wakiwa wanaishi kwenye hali ya msongo wa Mawazo " mwisho wasiku wanakufa kwa magonjwa ya hovyo ""
ndio maana hii nchi IPo kwenye top list yazile nchi ambazo wananchi wake hawana furaha ....manina wallahi nitalikimbia hili taifa ""
huku wafnyakazi hawaongezewi mishahara..huku bunge halionyeshwi live " huku kamata kamata ya viongozi wa vyama pinzani " huku kutoweka kwa watu ghafla kama azory na Ben saa8...huku maiti zimeokotwa kwenye fukwe zikiwa kwenye viroba..Mara mwanafunzi wa NIT kapigwa risasi ..huku " lissu kapigwa risasi ..Mara CAG aseme trillion 1.5 hazijulikani zilivyotumika .Mara watu wa kubiti 380 hawajulikani walipo " huku watu wamevunjiwa makazi yao kutoka Kimara .Mbezi mpka kibamba"" sasa hivi limeibuka hili la mikopo ""
.......kwa minajili hii tujiandae kukosa furaha daima
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini (TSNP) Abdul Nondo amefunguka na kusema kuwa kigezo cha bodi ya mikopo kutoa mikopo kwa kuzingatia tu wanafunzi waliosoma shule za serikali na kuwabagua wale waliosoma shule za private si sawa kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwakosesha haki watu kusoma.
Abdul Nondo amesema hayo siku moja baada ya kauli ya Rais Magufuli kusema kuwa bodi ya mikopo haiwezi kutoa mikopo kwa wanafunzi ambao awali walionekana kusoma katika shule za binafsi na kudai kuwa watu hao wanauwezo hata wa kusomesha na wazazi wao ndiyo maana waliweza kusomeshwa katika shule binafsi walipokuwa wakisoma.
"Mara ya kwanza kabisa, niliwahi sikia kauli ya namna hiyo kwa Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarishi akisema kama umesoma private school hupati mkopo. Kauli hii tuliipinga vikali, kipindi hicho na tukasema sio fair sababu gharama za chuo ni kubwa (Ada, hela ya kula ,copy, usafiri,hela ya malazi, hela ya mafunzo kwa vitendo field). Ni tofauti kabisa na fedha ya ada shule ya private laki 8, au mil 1 ambayo pia watu husoma kwa ada hiyo private. Kuwanyima mkopo ni kuwakatishia ndoto zao kabisa"
Nondo aliendelea kusema kuwa sababu nyingine ni kuwa uwezo wa mzazi unaweza kubadilika badilika inawezekana kipindi cha nyuma alikuwa na uwezo wa kulipia gharama lakini kipindi mtoto anaingia chuo labda mzazi amepatwa na magonjwa ya kudumu, uchumi umeyumba kiasi cha kushindwa kumudu gharama hizo jambo ambalo linapelekea wanafunzi wengine kukosa haki ya kusoma elimu ya juu.
"Mfano kipindi mtoto akiwa anasoma 'private' mzazi alikuwa na uwezo wa kulipa, kipindi mtoto anaingia chuo baba au mzazi amepata magonjwa, ameparalyze, amefilisika, kumnyima mkopo mtoto huyu ni kumkatishia malengo yake. Pia tulihoji juu ya kama mtoto amesoma kwa kudhaminiwa inakuwaje, kuna wanaodhaminiwa kusoma private schools na mashirika binafsi, watu binafsi, na husomeshwa shule tuu sio chuo, baadaye hutelekezwa chuo wajitegemee. Hii bodi ya mikopo walisema wataweka kipengele kuambatanisha vielelezo vya udhamini ila huwa ni geresha tuu huwa hawatoi hata uambatanishe ndio maana sio sahihi kutoa mkopo kwa kigezo cha u private schools, au u government schools siyo haki"
"Tulihoji pia wapo waliosoma kwa kurUdia mitihani kutafuta 'credits' mara nyingi hawa huwekwa katika kundi la private schools, wapo QT (qualified Tests), wapo diploma wote hawa huwa termed as private schools. Kuwanyima mkopo kwa vigezo hivi ni kupoteza ndoto zao. Kigezo cha kutoa au kutotoa mkopo kwa kuangalia ulisoma private au government sio kigezo sahihi. Kime katisha ndoto za wanafunzi wengi saana sababu hakitoi majibu halisi ya uwezo wa mwanafunzi kustahimili gharama"
Mbali na hilo Abdul Nondo amesema bodi ya mikopo sasa imekuwa ikikusanya marejesho ya mikopo kuliko kipindi chote kama ambavyo wao wenyewe wamekuwa wakisema hilo hivyo amewaomba kigezo hicho cha kuangalia mwanafunzi alisoma shule gani na kumpa mkopo huku wengine wakikosa mkopo kutokana na shule walizowahi kusoma siyo haki na kuwa kitendo hicho ni kukatisha ndoto za watu kusoma elimu ya juu.
"Hakuna kipindi bodi ya mikopo wanakusanya makusanyo na marejesho Kama kipindi hiki, tuwasii bodi ya mikopo hiki kigezo hakifai. Kama bodi ya mikopo wataamua kukitumia kama kigezo cha kukosa mkopo, basi tunawaomba waandike katika muongozo wao wa 2018/2019 .Wakiongeze kuwa "Kama ulisoma shule ya binafsi hupati mkopo" ili wazazi wajipange mapema na wajue kuwa mtoto akisoma private school hapati mkopo kutoka bodi ya mikopo. Itasaidia ikifafanuliwa hivyo"
Hongera sana Abdul Nondo, hoja yako imekaa vizuri, ila hata mimi kama ninauwezo wangu hakuna sababu mwanangu asome kwa mkopo. Wapo watu ambao kiukweli wanashida. Hawa wapewe kipaumbele hata kama wamesoma private. Kipengele hicho kiondolewe, ila elimu iendelee kutolewa kwa wazazi na wanafunzi wenyewe wasikimbilie mkopo kama sio lazima.
mtoto alipokuwa primary na sekondari mzazi alikuwa na ajira lkn anapofika chuo kikuu mzazi anakuwa keshastaafu Nondo yuko sawa, serikali afikirie upya kwani kusomesha private siyo lazima uwe tajiri.
Thinking outside the box: Hivi hawa ambao watoto wao wanakataliwa kupewa mikopo, siyo kwamba ndio wazazi wao ni walipa kodi wakubwa kwa nchi hii?? So this is what they get in return? Kweli Afrika linaweza kura bara hatari sana kuishi.
Nchi ya wajinga ndio huweka watu kwa matabaka .hao watoto wanaoitwa wa masikini ndio wepi hao ,utakuta baba zao wako baa kila siku ,ucone watu wanalipa ada za private ukadhani wanazo pesa wameacha kwenda baa hawana nyumba ndogo .tuwatafute hao wanaoitwa masikini tuone, wameoa wanawake wawili mpaka watatu ,ndio vidume kwenye baa ,ana wtoto tisa mpaka kumi mie ambaye nasomesha mtoto private nina watoto wawili na mke mmoja ,baa siendagi hivi nani masikini kati ya hawa watu ,Namwomba huyou mheshimiwa abadili mawazo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.