Si kila Mchungaji, Nabii au Mtume anayetumia Biblia kufundisha ni Mkristo, wengine ni matapeli

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Jan 3, 2018
1,816
5,151
Kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaojiita Mitume, Manabii au Wachungaji ambao wamekuwa wakiwakonfyuzi watu hasa wale ambao si waumini wa Dini ya Kikristo.

Kitu kibaya zaidi hao Viongozi wa madhehebu hayo wamekuwa wakitumia Biblia kama njia ya kufanya huo utapeli wao ukaonekana ni ukweli, Watanzania wengi wamejikuta wananaswa kwenye mtego huo kwakuwa kama tujuavyo Watanzania na kusoma vitabu ni kama paka na panya.

Watu wengi kutokusoma Biblia ndiyo imekuwa mtaji mkubwa wa hao matapeli kwasababu wanafahamu hao wanaojiita Wakristo hawaielewi Biblia kwa ufasaha.

Biblia ni kitabu kilicho wazi kabisa kwa wafuasi wa Kristo na hakina mambo mengi kama watu wanavyodhani. Kwakuwa wafuasi wengi wanaojiita "Wakristo" hawapendi kuisoma ndipo hao matapeli wamejipatia huo mwanya wa kuwadanganya.

Neno "Wakristo" lilipatikana kwa mara ya kwanza pale kwenye Mji wa Antiokia, na hii ni baada ya wafuasi wa Yesu kukutana huko kwa muda wa mwaka mmoja na kuungana katika mambo ya kufundishana yale yote ambayo Yesu Kristo aliwafundisha kabla hajapaa.

Hii utaipata katika kitabu cha Matendo ya Mitume 11 : 26

Hivyo neno "Wakristo" kwa kifupi ni watu wanao muamini Yesu Kristo, kuiamini imani yake na yale aliyoyafundisha.

Maswali amabayo Nabii, Mtume au Mchungaji hawezi yajibu;

1. Ni wapi katika Biblia imesema watu wafunge hadi wafe ili waende mbinguni?

2. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka gari uende ukaombewe?

Msingi wa kupata gari ni kufanya kazi, na maandiko yako wazi. "Fanya kazi siku sita na siku ya saba pumzika. Mungu ataibariki kazi ya mikono yako."

3. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka mchumba (mume/mke) upakwe maji au mafuta ya upako?

4. Ni wapi katika Biblia imesema ukiumwa UKIMWI uende kanisani uombewe UKIMWI uondoke?

Kupata UKIMWI ni matokeo ya dhambi, hivyo Mungu kwa uaminifu kabisa anaweza kukusamehe dhambi ila UKIMWI ukaendelea kuishi nao hadi unakuingiza kaburini.

Msipoielewa Biblia hakika mtafia dhambini.

5. Ni wapi katika Biblia imesema biashara yako ikiyumba ukachukue mafuta na maji ya upako uweke kwenye biashara yako?

Fanya biashara kwa uaminifu, fuata taratibu zote za kibiashara, mfanye Mungu awe wa kwanza katika biashara zako hakika utafanikiwa tu. Achaneni na hao matapeli watawaumiza sana tu.

6. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka kumuona Mtume au Nabii ni lazima ulipe fedha?

7. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka kuombewa na mtumishi wa Mungu ulipe fedha?

8. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka mtoto ukapewe mafuta na maji ya upako utumie ili uzae?

Wakristo ni watu wa maandiko (scriptures), ukiona unaingia mkenge kwa hao wapiga ramli wanaojiita Manabii na Mitume tambua wewe si Mkristo bali ni muunga tela la wapagani.

Mtaibiwa na kutapeliwa sana, kibaya zaidi mtakoseshwa na uzima wa milele kwa madanganyo ya matapeli hao.
 
Kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaojiita Mitume,Manabii au wachungaji ambao wamekuwa wakiwakonfyuzi watu hasa wale ambao si waumini wa Dini ya Kikristo.

Kitu kibaya zaidi hao Viongozi wa madhehebu hayo wamekuwa wakitumia Biblia kama njia ya kufanya huo utapeli wao ukaonekana ni ukweli,watanzania wengi wamejikuta wananaswa kwenye mtego huo kwakuwa kama tujuavyo watanzania na kusoma vitabu ni kama PAKA na PANYA.Watu wengi kutokusoma Biblia ndiyo imekuwa mtaji mkubwa wa hao matapeli kwasababu wanafahamu hao wanaojiita Wakristo hawaielewi Biblia kwa ufasaha.

Biblia ni kitabu kilicho wazi kabisa kwa wafuasi wa Kristo na hakina mambo mengi kama watu wanavyodhani.Kwakuwa wafuasi wengi wanaojiita "WAKRISTO" hawapendi kuisoma ndipo hao matapeli wamejipatia huo mwanya wa kuwadanganya.

Neno "WAKRISTO " lilipatikana kwa mara ya kwanza Pale kwenye Mji wa Antiokia,na hii ni baada ya wafuasi wa Yesu kukutanika huko kwa muda wa mwaka mmoja na kuungana katika mambo ya kufundishana yale yote ambayo YESU KRISTO aliwafundisha kabla hajapaa.

Hii utaipata katika kitabu cha MATENDO YA MITUME 11 : 26

Hivyo neno " WAKRISTO" kwa kifupi ni watu wanao muamini YESU KRISTO,kuiamini imani yake na yale aliyoyafundisha.

Maswali amabayo NABII,MTUME au MCHUNGAJI hawezi yajibu.

1.Ni wapi katika Biblia imesema watu wafunge hadi wafe ili waende mbinguni?

2.Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka gari uende ukaombewe?

-Msingi wa kupata gari ni kufanya kazi,na maandiko yako wazi. "Fanya kazi siku sita na siku ya saba pumzika"

"Mungu ataibariki kazi ya mikono yako"

3.Ni wapi Katika Biblia imesema ukitaka mchumba(Mume/Mke) upakwe maji au mafuta ya upako?

4.Ni wapi katika Biblia imesema ukiumwa UKIMWI uende kanisani uombewe UKIMWI uondoke?

-Kupata UKIMWI ni matokeo ya Dhambi,Hivyo Mungu kwa uaminifu kabisa anaweza kukusamehe Dhambi ila UKIMWI ukaendelea kuishi nao hadi unakuingiza kaburini.

Msipoielewa Biblia hakika mtafia Dhambini.

5.Ni wapi katika Biblia imesema biashara yako ikiyumba ukachukue mafuta na maji ya upako uweke kwenye biashara yako?

-Fanya biashara kwa uaminifu,fuata prosija zote za kibiashara,Mfanye Mungu awe wa kwanza katika Biashara zako hakika utafanikiwa tu,achaneni na hao matapeli watawaumiza sana tu.

6.Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka kumuona Mtume au Nabii ni lazima ulipe fedha?

7.Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka kuombewa na mtumishi wa Mungu ulipe fedha?

8.Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka Mtoto ukapewe mafuta na maji ya upako utumie ili uzae?

WAKRISTO NI WATU WA MAANDIKO(SCRIPTURES),UKIONA UNAINGIA MKENGE KWA HAO WAPIGA RAMLI WANAOJIITA MANABII NA MITUME TAMBUA WEWE SI MKRISTO BALI NI MUUNGA TELA LA WAPAGANI.

Mtaibiwa na kutapeliwa sana,kibaya zaidi mtakoseshwa na uzima wa milele kwa madanganyo ya matapeli hao.
Hosea 4:6 Watu wangu wa wanaangamizwa kwa kukosa MAARIFA, kwakuwa wewe umeyakataa MAARIFA, Mimi Mami nitakukataa wewe usiwe Kuhani kwangu Mimi, kwakuwa umeisahau Sheria ya MUNGU wako Mimi nami nitawasahau watoto wako" mwisho wa kunukuu maandiko matakatifu.
Unaweza kuta katika hao waliokufa 60% of them hawajui hata biblia takatifu ina vitabu vingapi in both old and new testament
Na ikumbkwe this is not African problem only,we have seen this in industrialized Europe and USA,in late 1979, Jimmy Johnstone, alikua cult leader wa people's Temple,aliua wafuasi wake Zaidi ya 1000, kwa kile kinachojulikana kama Johnstone massacre of 1979.
 
Actually haya mambo yalishatabiriwa mapema ukisoma Kitabu Cha Petro wa Pili,Yuda hata Ufunuo pia vinathibitisha uwepo wa Waalimu wa Uongo na manabii wa Uongo

But I like the Bible kwamba imeshakuweka aware chaguo ni lako uzima au kupotea
 
Kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaojiita Mitume, Manabii au Wachungaji ambao wamekuwa wakiwakonfyuzi watu hasa wale ambao si waumini wa Dini ya Kikristo.

Kitu kibaya zaidi hao Viongozi wa madhehebu hayo wamekuwa wakitumia Biblia kama njia ya kufanya huo utapeli wao ukaonekana ni ukweli, Watanzania wengi wamejikuta wananaswa kwenye mtego huo kwakuwa kama tujuavyo Watanzania na kusoma vitabu ni kama paka na panya.

Watu wengi kutokusoma Biblia ndiyo imekuwa mtaji mkubwa wa hao matapeli kwasababu wanafahamu hao wanaojiita Wakristo hawaielewi Biblia kwa ufasaha.

Biblia ni kitabu kilicho wazi kabisa kwa wafuasi wa Kristo na hakina mambo mengi kama watu wanavyodhani. Kwakuwa wafuasi wengi wanaojiita "Wakristo" hawapendi kuisoma ndipo hao matapeli wamejipatia huo mwanya wa kuwadanganya.

Neno "Wakristo" lilipatikana kwa mara ya kwanza pale kwenye Mji wa Antiokia, na hii ni baada ya wafuasi wa Yesu kukutana huko kwa muda wa mwaka mmoja na kuungana katika mambo ya kufundishana yale yote ambayo Yesu Kristo aliwafundisha kabla hajapaa.

Hii utaipata katika kitabu cha Matendo ya Mitume 11 : 26

Hivyo neno "Wakristo" kwa kifupi ni watu wanao muamini Yesu Kristo, kuiamini imani yake na yale aliyoyafundisha.

Maswali amabayo Nabii, Mtume au Mchungaji hawezi yajibu;

1. Ni wapi katika Biblia imesema watu wafunge hadi wafe ili waende mbinguni?

2. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka gari uende ukaombewe?

Msingi wa kupata gari ni kufanya kazi, na maandiko yako wazi. "Fanya kazi siku sita na siku ya saba pumzika. Mungu ataibariki kazi ya mikono yako."

3. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka mchumba (mume/mke) upakwe maji au mafuta ya upako?

4. Ni wapi katika Biblia imesema ukiumwa UKIMWI uende kanisani uombewe UKIMWI uondoke?

Kupata UKIMWI ni matokeo ya dhambi, hivyo Mungu kwa uaminifu kabisa anaweza kukusamehe dhambi ila UKIMWI ukaendelea kuishi nao hadi unakuingiza kaburini.

Msipoielewa Biblia hakika mtafia dhambini.

5. Ni wapi katika Biblia imesema biashara yako ikiyumba ukachukue mafuta na maji ya upako uweke kwenye biashara yako?

Fanya biashara kwa uaminifu, fuata taratibu zote za kibiashara, mfanye Mungu awe wa kwanza katika biashara zako hakika utafanikiwa tu. Achaneni na hao matapeli watawaumiza sana tu.

6. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka kumuona Mtume au Nabii ni lazima ulipe fedha?

7. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka kuombewa na mtumishi wa Mungu ulipe fedha?

8. Ni wapi katika Biblia imesema ukitaka mtoto ukapewe mafuta na maji ya upako utumie ili uzae?

Wakristo ni watu wa maandiko (scriptures), ukiona unaingia mkenge kwa hao wapiga ramli wanaojiita Manabii na Mitume tambua wewe si Mkristo bali ni muunga tela la wapagani.

Mtaibiwa na kutapeliwa sana, kibaya zaidi mtakoseshwa na uzima wa milele kwa madanganyo ya matapeli hao.

Maandiko yanatufundisha kuzitambua roho

Kumbukumbu La Torati 13:1-4

1. “Akitokea nabii au mtabiri wa ndoto miongoni mwenu, akawaahidi na kuwapa ishara au maajabu fulani,

2. halafu ishara au maajabu hayo yatokee, kisha aseme: ‘Tufuate miungu mingine na kuitumikia, (miungu ambayo hamjapata kuijua)’,

3. msisikilize maneno yake nabii huyo au mtabiri wa ndoto, kwa maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawatumia wao kuwajaribu, ili ajue kama mnampenda yeye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote.

4. Mfuateni na kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kushika amri zake na kuitii sauti yake; mtumikieni na kuambatana naye.
 
Mko bize na wachungaji na manabii ila Waganga na washirika wao mnawaruka .
Hawa ndio wanafanya uharibu Grade one Kila Kona na hamuwazingatii.

Shetani anawatumikisha kupingana na yeye wanaendelea kutamba

Rc ni matapeli pia
unaweza kutubu kwa binadamu mwenzio

1 Wakorintho 3:4-6

4 Mmoja wenu anasema, “Mimi ninamfuata Paulo,” na mwingine anasema, “Ninamfuata Apolo.” Mnaposema mambo kama haya, mnaenenda kama watu wa ulimwengu.

5 Je, Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Apolo na mimi si watumishi tu ambao Mungu alitutumia ili mmwamini Yesu Kristo. Kila mmoja wetu alifanya kazi aliyopewa na Bwana. 6 Nilipanda mbegu na Apolo akamwagilia maji. Lakini Mungu ndiye aliyeiotesha na kuikuza.
 
Kwa kifupi tu ni kwamba dini zote ni Utapeli mtupu, ila Walokole ndio wamepotea zaidi.

Poleee

... WENGI NI MATAPELI

TAFUTA KUIJUA KWELI UTAPATA MAARIFA

HOSEA 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
 
MKUU KWANI WAKRISTO WAKO NA DHAMBI WAKATI TUNABATIZWA NA HAPO HAPO YESU ALIKIFA MSALABANI ILI TUOKOKE NA DHAMBI
 
MKUU KWANI WAKRISTO WAKO NA DHAMBI WAKATI TUNABATIZWA NA HAPO HAPO YESU ALIKIFA MSALABANI ILI TUOKOKE NA DHAMBI

Rudi kajifunze Ubatizo na maana yake
Halafu ujue pia Yesu hakufa, aliyekufa ni Kristo
Ukiuelewa ukristo utaelewa

Yesu ni Mungu
 
Mambo ya manabii ya uongo sio mapya,yalishatabiriwa kitambo tunachokiona Sasa ni utimilifu wa maandiko.

Uko sahihi

WAEFESO 4:11-13
Naye alitoa wengine kuwa
mitume,
na wengine kuwa manabii;
na wengine kuwa wainjilisti
na wengine kuwa wachungaji
na waalimu;
kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo

Mungu hana mipaka
 
Jamani kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake waacheni watu wale.....Wasipokuwepo waumini watafunga huduma zao lakini wanao wengi na kila siku wanaongezeka
Watu wengi hawataki kazi wala kufuata utaratibu wanataka miujiza
Mtu anapaka mafuta ya nabii sehemu za siri ili atakayemuingilia amuoe jamani....

INSTAGRAM @dollrubii_decors
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom