Hii thread imenipa maswali mapya.
Kwa mara ya kwanza nilitoka nje ya DSM nikiwa naenda Moshi kwa ajili ya masomo ya A-level katika shule moja ya boys,,nikiwa kidato cha 6 tulialikwa kwenya mahafali katika shule ya wasichana ya Ashira.sijawahi kufika tangu nizaliwe lakini nilikuwa mwenyeji wa yale mazingira,ata nilioenda nao walishangaa nilipowaambia sijawahi kufika maana ndio nilikuwa nawaelekeza njia mpaka tunafika.Tukiwa njiani nilikutana na mzee mmoja ambaye alionekana kushtuka aliponiona na alikuwa kama mtu anayetaka kuniuliza kitu,haikuwa sura ngeni,ni sura niliyoizoea lakini sikumbuki niliiona wapi.
Nilipomaliza mitihani niliamua kurudi tena mwenyewe,niliizunguka Marangu kwa miguu,nikafika mahali ambapo sijawahi kukanyaga tangu nizaliwe lakini sikuwa mgeni,napafahamu..Mwishowe niliamua kujijibu labda paliwahi kuja ndotoni sababu tangu naenda Moshi kidato cha 5 Marangu ndio sehemu niliyokuwa natamani kufika