A living reincarnation, rebirth..!

Nimeshindwa kupata neno zuri la kichwa cha habari kitakachoendana na maudhui hivyo nimeamua kutumia hicho cha kiingereza.... Naomba radhi kwa watakaokwazika...!!!
Kabla sijaendelea naomba nitoe tafsiri ya reincarnation lakini pia nitoe na tafsiri ya rebirth (hizi zote kwa kiswahili ni kuzaliwa tena, ama kuzaliwa mara ya pili )

REINCARNATION ni mchakato wa kuzaliwa tena katika umbo la kiumbe hai kingine kutokana na matendo yako ya nyuma baada ya kufa.... Hii wanaitumia sana waamini wasioamini katika Mungu mmoja bali miungu... Kwao hakuna neno MSAMAHA... ukitenda baya utalipwa baya... Ukitenda jema utalipwa jema... Na hii hutokea ukiwa hai ama ukizaliwa TENA....!!!

REBIRTH ni mchakato wa kuzaliwa mara ya PILI lakini katika mwili ule ule ila likiwa ni tendo la kiroho zaidi... Hii hutumiwa sana na waamini wanaoamini katika Mungu mmoja na maisha ya peponi baada ya kifo kama ukitubu na maisha ya jehanum kama usipotubu na kuungama madhambi yako... Rebirth ni tendo la kuokoka kiroho....
Yote kwa yote kuna mstari mwembamba sana kati ya tafsiri hizi mbili rebirth na reincarnation... Moja ikiwa ni kuzaliwa tena na nyingine ikiwa ni kuzaliwa mara ya pili.... Moja ikiwa ni tendo la kiroho zaidi na nyingine ikiwa ni tendo la kimwili pamoja na kiroho....
Mfanano wao ni kwamba zote ni imani

Turejee kwenye mada yetu sasa
Kuna usemi maarufu duniani kuwa dunia wawili wawili... Kwamba kuna watu wa kaliba tofauti kabisa.. Nchi tofauti kabisa au maeneo tofauti kabisa lakini wamefanana kama mayai... Naamini umeshawahi kusikia mtu akikwambia kuwa nimemuona mtu anafanana na wewe kabisa... Hii ndio living reincarnation ninayotaka kuijadili hapa

Swala la matunzo ya watoto waliotelekezwa na wazazi wa kiume pamoja na kwamba limekuwa la kisiasa zaidi.. Lakini kiroho lina tafsiri yake pana sana... Tafsiri ya kwamba hapa duniani sura yako si yako pekee mtatofautiana vingine kama kabila umri eneo nk lakini sura ni ile ile.... Kitendo kilichofanywa na baadhi kutaka kuthibitisha madai yao ni kuweka sura za watoto na wababa wanaotuhumiwa kuwa hao ni watoto wao....
Hiki ni kichekesho kwakuwa wengi hawajui kuhusu living reincarnation or rather rebirth... Kwamba kipimo pekee kinachoweza kuthibitisha uhusiano wa mzazi wa kiume na mtoto ni kipimo cha kupima damu cha DNA....!!! hiki ndio kipimo pekee chenye majibu sahihi vingine vyote ni vya kufikirika na kuhisi zaidi kuliko uhalisia....
Lakini vile vile ni marangapi huwa tunahisi kuwa sehemu ambayo wala hatujawahi kufika... Saa nyingine tumeona kwenye luninga, gazeti au mitandaoni... Au unafika mahali kwa mara ya kwanza lakini unakuwa na hisia kamili kuwa hapo mahali unapafahamu.....
Roho zetu ni kitu kikubwa mno na kilicho huru.. Ni roho zetu hizi hutuhama nje ya ufahamu wetu na kwenda kuzurura kwenye ulimwengu wa roho na hata kuweza kuingia kwenye majumba roho ya mili mingine ama kupita sehemu ambazo hubeba kumbukumbu zake na kurudi nazo kwenye mwili asili...
Kumbukumbu hizo zikihifadhiwa kwenye ubongo hubaki na kutengeneza picha ya uhalisia usio timilifu... Hii hali hupelekea yafuatayo
. kukutana na mtu kwa mara ya kwanza lakini unahisi kabisa si mara yenu ya kwanza kukutana.. Basi huishia kusema tu nimekufananisha.
. kufika eneo kwa mara ya kwanza lakini ukiwa na fikra kuwa si mara ya kwanza... Jua roho ilikutoroka na kwenda yenyewe.
. kufananishwa na mtu ambaye hamfahamiani kabisa na mko mbalimbali
. kuwa na fikra ya kukaribia kutokea kitu fulani ambacho kiuhalisia hakijawahi kukutokea
. kufanya kitu kipya kabisa huku fikra zikikukumbusha kukifanya kitu hichohicho lakini bila kumbukumbu kamili

Ulimwengu wa roho ni timilifu na huweza kufanya vitu nje ya utashi wa kawaida wa binadamu na kutuletea Kumbukumbu zisisotimia.... Na hii ndio living reincarnation au living rebirth katika uhalisia wake......
Mimi sina mtoto wa kusingiziwa.... Mkioneshwa yeyote tunafanana hata vitabia jueni tu ya kwamba hiyo ni michezo ya roho katika kuvinjari kwake
Kuna hii movie ya Kihindi inaitwa KaranArjun ukiicheki somo lako la leo la reincarnation litaeleweka saaana.
Screenshot_20180412-133054.jpg
 
Mku

Mkuu mshana mm nina swali dogo tu kwenye maada hii hasa kipengele cha roho kutoka na kisha kurudi na kumbukumbu kikawaida tunajua ubongo una sehemu maalum ya kuhifadhi kumbu kumbu (hypocampus) au kwa lugha rahisi ni kuwa kumbu kumbu huhifadhiwa kwenye ubongo sasa tunavyoelewa kutokana na mafunzo ya kidini ni kuwa roho huwa haina physical body yaani yenyewe ni sawa na pumzi tu bali wengine husema huwa ina taswira na umbile sawa na physical body yake sasa kama ni hivyo that means huwa haiwezi kushikika wala kuonekana na kama ni hivyo ina maaana haiwezi kuwa na sehemu ya kuhifadhia kumbukumbu kwa sasa hizo memory inazorudisha kwenye mwili huwa ina bebea wapi? Mkuu?
 
Uko sahihi lakini pia naomba nikuulize hizo kumbukumbu ni physical au ni invisible?
 
Mkuu sipo deep sanaaa katika maswala ya neuroscience ila nitakujibu kadiri ya uwezo wangu ni kuwa katika ubongo kuna system(mfumo) maalum unaohusika katika maswala ya kumbukumbu ambayo kiujumla huitwa LIMBIC SYSTEM ambapo katika lymbic system kumegawanyika sehemu nyingi ila mfano wa hizo ni ( olfactory bulbs, hippocampus, amygdala, anterior thalamic nuclei, fornix n.k) sehemu hizi kama ilivyo kawaida zina mfumo wa neurone kama tunavyojua ubongo una neurons nyingi ambazo zenyewe ndo huwa kama njia ya kusafiririsha tarifa kwa njia ya umeme(electrical impulse) sasa turudi kwenye swali lako ni kuwa katika mfumo huo wa kumbu kumbu huwa kuna kitu wanakiita sensory processor (mchanganuo hisishi) ambao wenyewe huwa unapokea taarifa kwa mfumo wa kemikali(chemicals) au physical vibrations (mawimbi mtikiso) yaani utakapoona tukio ili lihifadhiwe na kwa kumbu kumbu basi mfumo huo utapokea either mabadiliko ya ki kemikali eneo hilo au utapokea mtikisiko maalum ambao utahifadhiwa kipawa chake katika hyppocampus na baada ya hapo kama utakuja kuona tukio hilo hilo basi tukio hilo husababisha utumwaji wa taarifa kama ya awali yenye kipimo (intesity) sawa na kile cha awali basi hapo ubongo wako huweza kupima kiwango cha taarifa kama ni sawa na kile cha awali hii husababisha wewe kupata kumbukumbu:
Mimi ndo hujua hivyo mkuu kwa hiyo kumbu kumbu si invisible bali ni STIMULI ambayo inahifadhiwa kwa mfumo wa chemical change au physical vibrations kwenye ubongo .
 
Asante sana kwa ufafanuzi... Lakini huu bado ni ufafanuzi wa kisayansi zaidi kuliko kiroho... Sayansi ina maelezo mazuri sana lakini inapokuja kama ukiwa wa kiroho utaendelea kuhoji na kuhoji na mwisho wa siku tutarudi kwenye nishati roho (spiritual energy) kama kisababishi cha kila kitu
Sasa iko hivi mfumo mzima wa kitendo ambacho automatically huanzia kwenye fikra, mchakato wake mpaka kufikia kuwa kumbukumbu, ukiachana na kile kitendo halisi mengine yote ni invisible
Kumbukumbu hugeuza visible tu pale unapoziwakilisha kwa maandishi, picha michoro ana kitu... Kwa mfano linatokea tukio la mauaji mtaani.. Halafu kwenye upelelezi polisi wanakuja na picha ya mtuhumiwa... Inatokea ulimuona mtu wa namna hiyo... Hapa sasa unavuta kumbukumbu.. Kitu kilichokuwa visible kilichanyatwa na kuwa invisible na sasa unajaribu kukigeuza visible tena kwa kutoa maelezo na kusaidiwa kuchora picha yake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom