A living reincarnation, rebirth..!

Mshana ninawezaje kuipa nguvu roho yangu,kwa maana ya nguvu ya machale,kupata ndoto za mambo yajayo na kadhalika.
 
Nimeshindwa kupata neno zuri la kichwa cha habari kitakachoendana na maudhui hivyo nimeamua kutumia hicho cha kiingereza.... Naomba radhi kwa watakaokwazika...!!!


Kabla sijaendelea naomba nitoe tafsiri ya reincarnation lakini pia nitoe na tafsiri ya rebirth (hizi zote kwa kiswahili ni kuzaliwa tena, ama kuzaliwa mara ya pili)

REINCARNATION ni mchakato wa kuzaliwa tena katika umbo la kiumbe hai kingine kutokana na matendo yako ya nyuma baada ya kufa.... Hii wanaitumia sana waamini wasioamini katika Mungu mmoja bali miungu... Kwao hakuna neno MSAMAHA... ukitenda baya utalipwa baya... Ukitenda jema utalipwa jema... Na hii hutokea ukiwa hai ama ukizaliwa TENA....!!!

REBIRTH ni mchakato wa kuzaliwa mara ya PILI lakini katika mwili ule ule ila likiwa ni tendo la kiroho zaidi... Hii hutumiwa sana na waamini wanaoamini katika Mungu mmoja na maisha ya peponi baada ya kifo kama ukitubu na maisha ya jehanum kama usipotubu na kuungama madhambi yako... Rebirth ni tendo la kuokoka kiroho....

Yote kwa yote kuna mstari mwembamba sana kati ya tafsiri hizi mbili rebirth na reincarnation... Moja ikiwa ni kuzaliwa tena na nyingine ikiwa ni kuzaliwa mara ya pili.... Moja ikiwa ni tendo la kiroho zaidi na nyingine ikiwa ni tendo la kimwili pamoja na kiroho... Mfanano wao ni kwamba zote ni imani!

Turejee kwenye mada yetu sasa..

Kuna usemi maarufu duniani kuwa dunia wawili wawili... Kwamba kuna watu wa kaliba tofauti kabisa.. Nchi tofauti kabisa au maeneo tofauti kabisa lakini wamefanana kama mayai... Naamini umeshawahi kusikia mtu akikwambia kuwa nimemuona mtu anafanana na wewe kabisa... Hii ndio living reincarnation ninayotaka kuijadili hapa

Swala la matunzo ya watoto waliotelekezwa na wazazi wa kiume pamoja na kwamba limekuwa la kisiasa zaidi.. Lakini kiroho lina tafsiri yake pana sana... Tafsiri ya kwamba hapa duniani sura yako si yako pekee mtatofautiana vingine kama kabila umri eneo nk lakini sura ni ile ile.... Kitendo kilichofanywa na baadhi kutaka kuthibitisha madai yao ni kuweka sura za watoto na wababa wanaotuhumiwa kuwa hao ni watoto wao....

Hiki ni kichekesho kwakuwa wengi hawajui kuhusu living reincarnation or rather rebirth... Kwamba kipimo pekee kinachoweza kuthibitisha uhusiano wa mzazi wa kiume na mtoto ni kipimo cha kupima damu cha DNA....!!! hiki ndio kipimo pekee chenye majibu sahihi vingine vyote ni vya kufikirika na kuhisi zaidi kuliko uhalisia....

Lakini vile vile ni mara ngapi huwa tunahisi kuwa sehemu ambayo wala hatujawahi kufika... Saa nyingine tumeona kwenye luninga, gazeti au mitandaoni... Au unafika mahali kwa mara ya kwanza lakini unakuwa na hisia kamili kuwa hapo mahali unapafahamu..

Roho zetu ni kitu kikubwa mno na kilicho huru.. Ni roho zetu hizi hutuhama nje ya ufahamu wetu na kwenda kuzurura kwenye ulimwengu wa roho na hata kuweza kuingia kwenye majumba roho ya mili mingine ama kupita sehemu ambazo hubeba kumbukumbu zake na kurudi nazo kwenye mwili asili..

Kumbukumbu hizo zikihifadhiwa kwenye ubongo hubaki na kutengeneza picha ya uhalisia usio timilifu... Hii hali hupelekea yafuatayo;
  • Kukutana na mtu kwa mara ya kwanza lakini unahis kabisa si mara yenu ya kwanza kukutana.. Basi huishia kusema tu nimekufananisha.
  • Kufika eneo kwa mara ya kwanza lakini ukiwa na fikra kuwa si mara ya kwanza... Jua roho ilikutoroka na kwenda yenyewe.
  • Kufananishwa na mtu ambaye hamfahamiani kabisa na mko mbalimbali
  • Kuwa na fikra ya kukaribia kutokea kitu fulani ambacho kiuhalisia hakijawahi kukutokea
  • Kufanya kitu kipya kabisa huku fikra zikikukumbusha kukifanya kitu hichohicho lakini bila kumbukumbu kamili
Ulimwengu wa roho ni timilifu na huweza kufanya vitu nje ya utashi wa kawaida wa binadamu na kutuletea Kumbukumbu zisisotimia.... Na hii ndio living reincarnation au living rebirth katika uhalisia wake..

Mimi sina mtoto wa kusingiziwa.... Mkioneshwa yeyote tunafanana hata vitabia jueni tu ya kwamba hiyo ni michezo ya roho katika kuvinjari kwake!

Licha technology kukua kupita kiasi tumeshindwa kujua haya mambo

Real nature of the earth
- Mungu ni kiumbe hakisi/ au ni roho au ni uwepo
- hii dunia itakuja kuishia wapi my after bill years nn kitaikumba dunia

-Maisha baada ya kifo
-Kuna njia yeyote ya kutokomeza kifo


Mungu alitokea wapi(swali hili nasikia ni vibaya sana kujiuliza unaweza anguka na kufa papo hapo). Mshara
narudisha microphone kwako
 
Licha technology kukua kupita kiasi tumeshindwa kujua haya mambo

Real nature of the earth
- Mungu ni kiumbe hakisi/ au ni roho au ni uwepo
- hii dunia itakuja kuishia wapi my after bill years nn kitaikumba dunia

-Maisha baada ya kifo
-Kuna njia yeyote ya kutokomeza kifo


Mungu alitokea wapi(swali hili nasikia ni vibaya sana kujiuliza unaweza anguka na kufa papo hapo). Mshara
narudisha microphone kwako
Hayo kamwe hayawezi kuja kujulikana katika ulimwengu wa technology kwakuwa huu ni ulimwengu hatua ya pili secondary stage.. Wakati ulimwengu wa roho ndio msingi wa kila kitu primary stage
 
Tunapata ujumbe gani hapa!? Angalia kushoto kuna nini na kulia kuna nini... Angalia chini kuna nini... Vipi kuhusu juu!?

Mkuu, turudi hapo kwenye hiyo Circle
Tukijaaliwa kuamka salama.... Tukutane kwa ajili ya uchambuzi na ufafanuzi wa kina zaidi.... Dhana ya kuzaliwa tena na kuzaliwa mara ya pili... Dhana ya kumbukumbu ya mahali tusipowahi kufika kabla na matukio yake.... Dhana ya kufanana na kufananishwa View attachment 741786View attachment 741806
 
Tunapata ujumbe gani hapa!? Angalia kushoto kuna nini na kulia kuna nini... Angalia chini kuna nini... Vipi kuhusu juu!?
Tukijaaliwa kuamka salama.... Tukutane kwa ajili ya uchambuzi na ufafanuzi wa kina zaidi.... Dhana ya kuzaliwa tena na kuzaliwa mara ya pili... Dhana ya kumbukumbu ya mahali tusipowahi kufika kabla na matukio yake.... Dhana ya kufanana na kufananishwa View attachment 741786View attachment 741806
Mkuu, turudi kwenye hiyo Circle hapo juu
 
Asanteeee sana kwa bandiko zuri mkuu
Kuna vingi vya kujifunza
Nipo hapa nairudia rudia nikuulize tu swali tuwili tutatu hivi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom