Nimeshindwa kupata neno zuri la kichwa cha habari kitakachoendana na maudhui hivyo nimeamua kutumia hicho cha kiingereza.... Naomba radhi kwa watakaokwazika...!!!
Kabla sijaendelea naomba nitoe tafsiri ya reincarnation lakini pia nitoe na tafsiri ya rebirth (hizi zote kwa kiswahili ni kuzaliwa tena, ama kuzaliwa mara ya pili)
REINCARNATION ni mchakato wa kuzaliwa tena katika umbo la kiumbe hai kingine kutokana na matendo yako ya nyuma baada ya kufa.... Hii wanaitumia sana waamini wasioamini katika Mungu mmoja bali miungu... Kwao hakuna neno MSAMAHA... ukitenda baya utalipwa baya... Ukitenda jema utalipwa jema... Na hii hutokea ukiwa hai ama ukizaliwa TENA....!!!
REBIRTH ni mchakato wa kuzaliwa mara ya PILI lakini katika mwili ule ule ila likiwa ni tendo la kiroho zaidi... Hii hutumiwa sana na waamini wanaoamini katika Mungu mmoja na maisha ya peponi baada ya kifo kama ukitubu na maisha ya jehanum kama usipotubu na kuungama madhambi yako... Rebirth ni tendo la kuokoka kiroho....
Yote kwa yote kuna mstari mwembamba sana kati ya tafsiri hizi mbili rebirth na reincarnation... Moja ikiwa ni kuzaliwa tena na nyingine ikiwa ni kuzaliwa mara ya pili.... Moja ikiwa ni tendo la kiroho zaidi na nyingine ikiwa ni tendo la kimwili pamoja na kiroho... Mfanano wao ni kwamba zote ni imani!
Turejee kwenye mada yetu sasa..
Kuna usemi maarufu duniani kuwa dunia wawili wawili... Kwamba kuna watu wa kaliba tofauti kabisa.. Nchi tofauti kabisa au maeneo tofauti kabisa lakini wamefanana kama mayai... Naamini umeshawahi kusikia mtu akikwambia kuwa nimemuona mtu anafanana na wewe kabisa... Hii ndio living reincarnation ninayotaka kuijadili hapa
Swala la matunzo ya watoto waliotelekezwa na wazazi wa kiume pamoja na kwamba limekuwa la kisiasa zaidi.. Lakini kiroho lina tafsiri yake pana sana... Tafsiri ya kwamba hapa duniani sura yako si yako pekee mtatofautiana vingine kama kabila umri eneo nk lakini sura ni ile ile.... Kitendo kilichofanywa na baadhi kutaka kuthibitisha madai yao ni kuweka sura za watoto na wababa wanaotuhumiwa kuwa hao ni watoto wao....
Hiki ni kichekesho kwakuwa wengi hawajui kuhusu living reincarnation or rather rebirth... Kwamba kipimo pekee kinachoweza kuthibitisha uhusiano wa mzazi wa kiume na mtoto ni kipimo cha kupima damu cha DNA....!!! hiki ndio kipimo pekee chenye majibu sahihi vingine vyote ni vya kufikirika na kuhisi zaidi kuliko uhalisia....
Lakini vile vile ni mara ngapi huwa tunahisi kuwa sehemu ambayo wala hatujawahi kufika... Saa nyingine tumeona kwenye luninga, gazeti au mitandaoni... Au unafika mahali kwa mara ya kwanza lakini unakuwa na hisia kamili kuwa hapo mahali unapafahamu..
Roho zetu ni kitu kikubwa mno na kilicho huru.. Ni roho zetu hizi hutuhama nje ya ufahamu wetu na kwenda kuzurura kwenye ulimwengu wa roho na hata kuweza kuingia kwenye majumba roho ya mili mingine ama kupita sehemu ambazo hubeba kumbukumbu zake na kurudi nazo kwenye mwili asili..
Kumbukumbu hizo zikihifadhiwa kwenye ubongo hubaki na kutengeneza picha ya uhalisia usio timilifu... Hii hali hupelekea yafuatayo;
- Kukutana na mtu kwa mara ya kwanza lakini unahis kabisa si mara yenu ya kwanza kukutana.. Basi huishia kusema tu nimekufananisha.
- Kufika eneo kwa mara ya kwanza lakini ukiwa na fikra kuwa si mara ya kwanza... Jua roho ilikutoroka na kwenda yenyewe.
- Kufananishwa na mtu ambaye hamfahamiani kabisa na mko mbalimbali
- Kuwa na fikra ya kukaribia kutokea kitu fulani ambacho kiuhalisia hakijawahi kukutokea
- Kufanya kitu kipya kabisa huku fikra zikikukumbusha kukifanya kitu hichohicho lakini bila kumbukumbu kamili
Ulimwengu wa roho ni timilifu na huweza kufanya vitu nje ya utashi wa kawaida wa binadamu na kutuletea Kumbukumbu zisisotimia.... Na hii ndio living reincarnation au living rebirth katika uhalisia wake..
Mimi sina mtoto wa kusingiziwa.... Mkioneshwa yeyote tunafanana hata vitabia jueni tu ya kwamba hiyo ni michezo ya roho katika kuvinjari kwake!
Dhana ya 'Utwaaji Upya Mwili' yaani 'Reincarnation' kwa lugha ya kiingereza -- na tena kulingana na imani, maarifa ya kimapokeo na dini -- kama vile Uhindu, Ujaini, Ubuddha n.k; huenda si 'ukweli kamili' juu ya 'kuishi' na 'maisha ya mtu'.
Kwa namna yake, Utwaaji upya mwili, huenda ilikuwa ni tafsiri nyepesi juu ya ukweli wa jambo fulani lililo pana na tata kuhususiana na 'uzima' na 'miili'. Hii ilikuja na 'maona', 'manabii' na 'watu wakuu kiroho'. Kwa maana hawa wote-- iwe kutokea mashariki ama magharibu -- wametuletea nasibu ya habari na visomo kuhusiana na 'mtu','mataifa/kabila/staarabu', 'matukio', 'wakati' na 'hatma' zake.
Yesu, kutokea nchi ya zamani kule Mashariki ya Kati -- kwa mfano, amenukulishwa katika vitabu vya dini, imani na mapokeo kupata kusema "siku za mwisho, maarifa yataongezeka duniani...". Kwamba, yale anayoyafanya, watu wengi wataweza kuyafanya pia hata na zaidi... Sasa, siku za mwisho kwa mfano, ni zipi? Ikiwa mengi aliyopata kuyasema tunayakubali -- na kwa kiasi fulani kushangazwa, ni kwa namna gani aliweza kujua "Mambo ya mbele ya wakati"(?)... Maarifa kuongezeka, Vita na Mabadiliko ya Nchi...
Ni KWELI YESU ALIKUWA NI MWENYE KUWEZA KUONA MATUKIO hata nje ya mzingo wa fahamu zake za mwili wa nyama. Watu wengi tu wamepata kuwa hivyo hivyo; kuwa na 'Jicho la Tatu' -- yeye Yesu, kunukuliwa hili linawezekana pale 'mbili inapofanywa kuwa moja'... Lakini, Je, kuona nje ya mzingo wa wakati ndiyo 'kuwa na maarifa' kama yote? SI LAZIMA... Na hapa tunaweza kutumia kesi hiyo hiyo ya Yesu, kuanza kukadirisha yumkini ya ukweli wa jambo...
Japo kuna 'kanuni ya msababishano' wa vitu na matukio; ndani ya 'mapana ya yote',
wakati waweza 'kuchezeshwa' na basi hata kuwa kana 'mwisho wa dunia' usiwe ni 'mwisho' wa dunia... Tunaweza kunasibu kesho iliyo ni tofauti na 'jaala' zetu. Kwenye dini, huzungumzwa 'unafsishi' wa 'Mungu Muweza yote'... Kwamba 'utu' ama 'umma' wenye 'nyoyo safi' na 'Kuishi katika Yeye' huo waweza 'kuepushwa' na lolote 'ovu'... HII NI KWELI; lakini 'Mungu' ni fumbo la Imani...
Katika siku za leo, tunayonafasi ya kujua mambo ilivyo bora kuliko siku za nyuma zilizotuletea dini na mapokeo yanayotawala wengi duniani.
Kati ya vitu ambavyo tutavijua ama kuviandea vyema ili kujua ni 'fumbo la Mungu'; lakini sasa--tunaelekea kujua ukweli kwamba hakuna 'Mungu' hasa, ila kuna 'Uungu'... Vitu vyote, ni 'sifa', 'ishara' na 'utukufu' wa 'kweli' moja iliyo ni 'Mungu'. Lakini ni pale tu tunapoimaizi ama kujinasibu na 'kweli' katika muktadha wa 'Uungu' ndipo tunaweza kujilingania uwezo wa 'kufanyika moja na mawezekano yaliyo makuu'... Ikiwemo kutawala 'Mambo ya Nyakati' na kukadirisha 'Sheria za Madhahirisho' si tu hapa duniani ila ulimwenguni pote. Labda mapokeo ya kidini yangetaja hili kana kusema: 'kuwa Warithi wa Ufalme wa Mbingu -- Mbingu na Nchi'... Ndivyo Yesu alivyoita hasa; kusema baada ya 'Mtu kuzaliwa mara pili'... Mtume Paulo kusema; kuwa 'Mtu Mpya' mwenye nasibu ya 'Nchi Mpya'...
Mshana, 'kweli' ni si hasa --- ama tuseme, haipatikani katika stori stori ama visa vya ajabu ajabu... Kweli ni 'Taji la Imani na Taa' katika ufahamu na katika mtu. Labda mtu mwenye kuiishi njia ya imani ya namna hii anaweza kuwa ni 'mtu wa maarifa'--lakini ikiwa ni hivi, mtu huyu atanasibika 'hekima' na 'busara'. Lakini pia, maarifa si lazima iwe ni maneno... Hata katika ukimya, mapenzi na utumishi, roho ya 'kweli na uzima' inatenda -- wakati wowote na popote; kupitiliza hata 'matukio katika Nyakati'... Watu wa haya ni 'Waamuzi' katika yote yatendekayo--leo, hata kesho katika leo. Katika Uungu hakuna mwanzo wala mwisho, hakuna 'mipaka' wala 'kiasi'...
Basi, humu JF sasa, kipo kizazi cha chipkizi wenye kiu na hamu ya 'kuijua kweli'... Hawa, ndiyo huanza na udadisi, wengine watahoji kuhusu dini na mapokeo, wengine watavutika na mambo yanaonekana kupitiliza kawaida, wengine watakuwa wakanushaji wa yote yaliyoletwa na dini na kuja kuonekana ni kizingiti kwa utanuzi wa fikra, maarifa na upeo. Yote haya ni kheri, Labda pamoja tutajenga 'Hema jipya la Makutanio' katika 'Hesabu' ya watu wa Leo... 'Walawi wa leo' wanamuhitaji Musa wa vilemba vingi -- mkufunzi wa fikizia za kikwantumu, mtaasisi wa maendeleo--mipango na usimamizi, mvumbuzi, mzazi, ndugu na rafiki katika 'safari ya kuhama'; toka kwenye 'utumwa wa kimafikara' kuielekea lulu ya 'uzima na habari za ulele'.
Hmmm.