A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

Ndo maana huwa nasema kuwa nchi hii haina kiongozi serikalini. Kumpiga mtu wanadhani ndo kutatua matatizo? The end is nearer than ever!
 
Hilo nakubaliana na wewe, huwezi ukataka kumuua mtu just because anadai haki yake ya kimsingi..serikali imeshindwa kuwatetea wananchi ambao ndio waliowapigia kura. CCM AND THE GOVERNMENT kama wanahusika inabidi wajiuzulu. Na mataifa ya nje waache kutoa misaada hapa tanzania mpaka tuwe na uchaguzi mkuu.
 
Mimi hapo penye red ndo panaponifanya nishangae sana juu ya hii skendo. Hata kwenye ile thread nyingine nilijikuta nashindwa kuamini kama serikali imehusika.

Swali langu ni kuwa "Ulimboka alitekwa peke yake, na baada ya kuokotwa alikuwa hana fahamu na hawezi kuongea. Je, haya yaliyomtokea kayasema nani?

Hawa ndio watanzania ndugu yangu likishatokea jambo kila mmoja anatengeneza story yake. Hakuna tofauti na hekaya ya Abunuasi
 
Watanzania wenzangu tukubali kuwa kila binadam alizaliwa na atakufa sitakuwa mimi wala wewe ambaye unasoma haya machache ninayoandika hii picha ya dr ulimboka ni trela ya yale ambayo yatafanywa na hawa watu waliobeba dhamana zetu naumia sana na nimepata ujasili wa yale yatakayotokea mbele sina uhakika kama majambaz wanaweza kufanya upuuzi huu ndugu zangu tufunge mikanda,tujiandae na hawa wauaji naumia dr uli mungu yu nawe. Haki aiombwi inachukuliwa
 
Sasa rais ajiuzulu kwa kipi hasa?

Mimi nadhani ingekuwa busara mheshimiwa kiongozi wa madaktari Dr Ulimboka ajiuzulu mara moja kwa sababu wakati anafanya mazungumzo na hao jamaa kama alizungumza nao kama mwakilishi wa madaktari bila kupata idhini ya chama cha madaktari ni makosa makubwa!!

MSITU WA PANDE UMEKUWA UKITUMIWA USALAMA WA TAIFA PIA ZOMBE ALIFANYA MAUAJI UKO, APO NAAMINI WAHUSIKA NI WALE TULOWAPA KURA KWA KISHINDO, WAO WANANGUVU SIE TUNA MUNGU, OH MOLA WETU MWEMA, MSSIMAMIE, MSAIDIE PIA MPE AFYA NJEMA JEMEDARI WETU DR ULIMBOKA RIL HAJATENDEWA HAKI, Amin
 
Hivi kama kumuua dr. Ulimboka ni ufumbuzi wa kudumu wa tatizo lililopo kwa nini wasiwakamate madaktari wote nchini wawapeleke gas chamber wawaue kama Adolf Hitler alivyowafanyia wayahudi?! damu ya Ulimboka iliyovuja itakuwa chachu ya mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Ewe Mwenyezi Mungu inusuru Tanzania yetu isibadilike na kuwa "A man eat man society" kama nchi fulani hapa afrika mashariki!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kuna kauli iliwahi kutolewa na waswahili mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!
 
Mimi hapo penye red ndo panaponifanya nishangae sana juu ya hii skendo. Hata kwenye ile thread nyingine nilijikuta nashindwa kuamini kama serikali imehusika.

Swali langu ni kuwa "Ulimboka alitekwa peke yake, na baada ya kuokotwa alikuwa hana fahamu na hawezi kuongea. Je, haya yaliyomtokea kayasema nani?

Hii ni JF, unajuaje wahusika wenyewe nao wamo humu? Nangojea watakapoweka picha ya tukio lenyewe.
 
Kutokana na vitendo alivyo fanyiwa mpigania Haki Dr. Uli nashawishika vita ya Haki inakaribia kushinda dhidi ya mkoloni mweusi aliye tutawala miaka 50 toka tupate Uhuru kwa mkoloni mweusi.
 
Kama hili ni lakweli na haya yaliyotokea ni kweli basi ndugu inueni vichwa vyenu! Maana Watekaji wenu wapowaziwazi. Hii si dalili inayoashiria heri ......wala si kitu cha kushabikia ........wala si swala la kusifia......wala si habari ya kupenda isikike tena.....wala haivutii bali kuhuzunisha........!!!!
 
Sasa rais ajiuzulu kwa kipi hasa?

Mimi nadhani ingekuwa busara mheshimiwa kiongozi wa madaktari Dr Ulimboka ajiuzulu mara moja kwa sababu wakati anafanya mazungumzo na hao jamaa kama alizungumza nao kama mwakilishi wa madaktari bila kupata idhini ya chama cha madaktari ni makosa makubwa!!

Acha ukuwadi huna huruma kabisa MCHUMIA TUMBO KAMA CCM WENZAKO MWOGOPE MUNGU!! aNGEKUWA NDUGUYO NDO KAPIGWA HIVYO UNGETOA HIZO pumba unazotoa !!!!!!
 
Yan haya ni mauaji kbisa na tunahitaji tamko la serikali kwa hili.

Kumbe ndio maana ya msemo wa liwalo na liwe.

Kwa Mungu roho ya Mtu Masikini na Roho ya Mtu tajiri ni SAWA, Kwanini Roho ya ULI iwe ya pekee kiasi kwamba inahitaji maandamano ya nchi Nzima???????????????????????. Drsssssssss, mmetanguliza masilahi yenu mbele kwa kugharimu roho wa Watanzania maskini, Leo yanampata kiongozi wa migomo, mnajifanya kutaka kuiondoa SRk madarakani. Roho ipi inathamani, Ya huyo mmoja au Roho zisizo naidadi zinazopotea pale MOI????????????????????.
 
Ndugu zetu wangapi wamepoteza maisha katika mgomo wa kwanza mbona hukusema kitu, leo Uli unajifanya kuongea sana, acha unafiki wa mawazo.
 
Back
Top Bottom