A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

mi binafsi nawapongeza madaktar kwa mgomo wao, ila wanachonikela kama wamegoma kutuhudumia wananchi kwa nini wanamuhudumia ulimboka? Na yeye wangegoma tukajua kweli kuna mgomo. Leo hii mnagoma kuwahudumia wakina mama wajawazito wanaotaka kujifungua, na ndugu zetu wote anahudumiwa mtu mmoja huo ni uungwana au ubinafsi? Mnatunyanyasa watu tusiokuwa na hatia wala sio hiyo serikali. Tukimbilie wapi sisi? Na nyie mnaoshabikia mgomo usiombe kupata ajari ghafla ukaenda hospitali na kugomewa kupewa huduma. Utakufa unajiona. So bad.
 
Kwa hiki kilichomtokea Dr. Ulimboka,Rais Kiwete hakupashwa kwenda kumpa pole kabisa. Hii ni kudhihirisha UDHAIFU wake mwingine. Yeye Kiwete ndiyo chanzo cha JARIBIO LA MAUAJI YA DR. ULIMBOKA AMBALO HALIKUFANIKIWA.Sasa anaenda kumwona ili iweje? Kujikosha? Unafiki? Kupoteza lengo au nini hasa? Maana huu mgogoro umeingia mwaka wa pili na hakuna ufumbuzi. Kama ameshindwa kutatua matatizo ya Madaktari kwa muda wote huu hafai kuwa RAIS!!
 
wanagoma na mwisho wa mwezi wanaenda na ATM kudraw Bank fedha zetu walipa kodi huku wagonjwa wetu wanakufa hospitali. hii ni halali? kwanini waendelee kulipwa mwezi huu? kwanini serikali haigomi kuwalipa kwa kususa kwao? hawatendi haki hata kidogo.

wewe mzima unawasaidiaje wagonjwa wetu wanaokufa kwa adhari za mgomo huo... nadhani ungesema kesho nitagoma kula kushinikiza madai ya madr kutimiza ili ndugu zetu watibiwe vizuri .. kama hauko tayari badi nyamaza kwani wagonjwa wenyewe wako tayari kufa ili ma dr watimiziwe madai yao ili kuweza kusaidia kizazi kijacho... wewe mbugiri tulia na anza ku judge nani amekosea na nani hajakosea kwanza usiongelee hela zetu sie ndo walipa kodi wakilipwa mishahara sio hela za serikali ni zetu .... na sie ndo tunao amua waongezewe au wasiongezewe mshahara... kwa kufa au kwa kunyamaza kimya .... wewe inawezekana hata ni mkwepa kodi kwa hiyo nyamaza tu kimya la sivyo tutaanza kukufuatilia...
 
kama anaendelea sawa jina la bwana lihimidiwe, wanafki siku zpte huumbuka kama alivyoumbuka yule shushushu pale m2
 


Hali ya dr Ulimboka kwasasa ni kama unavyo muona hapo! Mungu mbariki apate afya njema!
 

elungata,
hivi ni sababu gani ilikuwa inasababisha hao madaktari wawe wanaiba hizo dripwater na madawa na kwenda kuuza uswahilini?
 

Wasichukue kwani hawalipi kodi?
Unazijua aina za kodi na jinsi zivyolipwa?
Usikurupuke!
 

Umekaa ukajiuliza kwa nini wanaiba / kuomba rushwa? hivi anaekula akashiba sa ngapi atafikiria kuiba / kuomba rushwa?.....wanafanya yote hayo vile maslahi yao ni duni.....boresheni maslahi yao muone kama wataiba / kuomba rushwa......sitetei anaeiba / kuomba rushwa ila kabla hujamuhukumu kwa kuiba jaribu kujiuliza kwanza.....mbona wabunge hawana wanachofanya bungeni lakini wanalipwa vizuri kuliko hao madaktari?
 

Kumbe wewe unawahafamu wafanyakazi wa afya ambao wanatenda yasiyopaswa namengine maovu alafu unachelewa kuwatolea ripoti police maana unaneemeka nayo kwakukulipia ada nahela yako yakula eee!SHEM ON YU!
 
JK hawezi kwenda kumuona shujaa anemkosesha usingizi maan madai yao ni ya msingi sana na aibu kwa rais! CT Scan ni 250m tsh wanashindwa kununua kila hosp kubwa hapa tanzania ila wanaiba 3bil pesa za kuzurulia rais!

Aibu sana wala hana haja ya kwenda atafute nchi ambayo hajaenda siku nyingi aende akaombe dawa ya ngao maana vyandarua alivyoenda kuomba marekani vimeisha dawa yake!!.......asije akaulizwa kwa nini nchi yako ina ugonjwa wa malaria?

Asije akajibu "kwani mimi mbu?waulizwe mbu"
 
Mother theresa na mwenzake nighngale wakifufuka leo hii WATAKUFA KWA KIHORO...
>swtlj...binadamu angekua anatosheka na pesa wale mafisadi wangeshatosheka.
>wewe unaesema nitoe taarifa polise,ALIEKWAMBIA POLISI NI MALAIKA NI NANI?WEWE MWENYEWE SI AJABU NI DAKTARI NA UNAFANYA MAMBO HAYO KAMA KAWA.
 
tusisukumwe na hisia juu ya kipigo cha dr.ulimboka and eventually reaching to a sanctity statement that the government has afrontly commited a crime to dr.ulimboka without making critical analyisis about event.


Yawezekana kabisa serikali kushiriki katika tukio hilo haramu ili kuzima nguvu ya kiongozi huyo katika kuongoza migomo ya madaktari hao.lakin swali la kujiuliza ni kwamba ni serikali gani iso na akili ikafanya uovu huo dhahiri? Kwani serikali imeashiwa mbinu za kum abduct mtu? Evi mara ngapi tumesikia fulani amepotea,amekfa katika mazingira tatanishi?


Pia,yawezekana watu wasioitakia serikali kuhusika tukio ili kudhihirisha udhaufu wake nahivyo kujiimarisha kisiasa ama kikanda na hatimaye kuchukuwa nchi 2015 kama inavyondotewa.kwa mfano ikumbukwe ter.12,january,2011 kipo chama kilisema wazi kuwa,kitahakikish kinatumia kila aina yavitimbi ili kuhakikisha nchi haitawaliki.je chama hicho hakiwezi kuwaziwa kwa tukio hili kama ni mbinu kutekeleza mkakati?



Aidha,migomo ya madaktari ilisababisha baadhi ya mawaziri kutupwa nje pale raisi alipotengua baraza na kuunda lingine.je hamuoni ka hawa wanaweza kufanya hivyo kwa aidha kulipiza kisasi au kumkomoa rais kwa kuwatupa nje?


Vilevile ifahamike kuwa,migomo ya madakatari inasababisha vifo vya watu waso na hatia.je hamuwezi kuona kuwa hizi ni hasira za wananchi wanaopoteza ndugu zao kwa migomo ya madaktari?


Lakini pia,juzi tu tumeshuhudia askofu mmoja akitamka kuwa,ccm ijiandae kuaga ikulu mwaka 2015.je hamuwezi kuona kuwa,haya ni maandalizi ya kufikia lengo hilo la askofu hoyo?


Mwisho napenda kusema kuwa, tusiharakie kuishtumu serikali kuhusika na tukio hilo bali tuachie tume kufanya uchunguzi kwani mchawi atapatikana tu.


Naomba kuwasilisha wanajamii





 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…