Kwa staili ya uongozi wa JK, yeye binafsi sidhani kama anahusika, kwa kuwa watendajhi wake hukosa busara mara nyingi sana na kwa kuwa hana tabia ya kumlinda mtu, au kumpa mtu maelekezo ya nini cha kufanya, mpaka ashindwe ndio anaingilia kati (rejea swala la katiba, rejea mgomo uliopita vongozi wa kada mbalimbali waliropokwa wee mwinsho wakaumbulia na maamuzi na msimamo tofauti) Kuna Maswali muhimu ya kujiuliza ambayo yanasaidia kutafakari:
1. Je, haiwezekani ikawa ni chombo fulani cha dola au taasisi ya serikali (au kiongozi wake) kimeona kitengo chake kinadhalilishwa kwa kushindwa kuzuia vuguvugu hili na wanaona wajichukulie hatu wanazo ona wao ili kulinda kitengo na nafasi walizonazo? Hasa hasa ukizingatia watu wanavyopoteza kazi serikalini kwa kushindwa kusimamia maeneo yao ya kazi (yani hakuna garantee ya post uliyonayo). wako tayari hata kumshauri waziri mkuu vibaya kama walivyofanya kipindi kilichopita.
2. je kutokana na kuongezeka kwa uadui wa kisiasa (wa ndani au/na nje ya CCM), haiwezekani ikawa madui wametake advantage ya situation ku-set more fire? Na kuhakikisha wanafanya kitu ambacho kitaimarisha mgomo na kuifanya serikali ionekane dhaifu na inatumia mbinu chafu? Na hivyo kupelekea watu wa rika la kati (midle class) ambao ndio chachu hasa ya mapinduzi, ingawa sasa hawashiriki kikamilifu katika siasa kwani wako busy na uzalishaji mali.
3. Je watakuwa ni baadhi ya wale waliothiriwa kwa njia moja au nyingine na migomo hii?
Je hawadhani JK angependa busara itumike zaidi kuliko nguvu na maneno ya kejeli? Au kutaka kuonyesha mabavu kwa watu ambao serikali hii ni yao na si yenu nyinyi mlioko madarakani ambao ni dhamana tu mmepewa na haohao wanaolalamika?