99.9% ya Wananchi wanamkubali Rais Samia Suluh Hassan

99.9% ya Wananchi wanamkubali Rais Samia Suluh Hassan

Uchaguzi ukifanyika leo hata waibe kura samia atapigwa chini
Hata mpewe usimamazi wa uchaguzi bado hamuwezi kupita maana hamuwezi kupata kura za wananchi, Nani awape kura? Kwa Sera na ajenda zipi mlizonazo? Mh Rais wetu Mama Samia Hana mpinzani Wala mtu wakuweza kushindana Naye kutoka huko upinzani
 
Acha kupotosha umma, soma comment zilizopo hapa maana sisi ni robo sehemu ya watanzania ulinganishe na Uzi uliouanzisha.
Takwimu kama hizi za kukubalika kwa Rais inapendeza zikatoka kwa Taasisi zinazojielewa
 
Punguza kuota mchana
Huo ndio ukweli,na ukweli,huwa unauma,Mh Rais anakubalika 99.9%.Nilisema humu kuhusu Ruto anavyokubalika Kenya,na matokeo yameonekana,mpaka mahakamani ameshinda.Wapo walionipinga,sasa hawana hoja.
 
Mama Hana mpinzani anayeweza ingia Naye uwanjani, mama Ni habari nyingine, kila Eneo utakalogusa utakuta mama kaweka baraka zake, Ni kazi juu ya kazi, Ni mwendo wa kutimiza ahadi, Ni mwendo wa kuwatumikia watanzania kwa utumishi ulio tukuka na wenye kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti
Umeelezea vizuri sana,na unazidi kuwaumiza moyo,wasiojelewa.
 
Nimekwambia acha matusi, Mimi siwezi kukutukana maana ninamheshimu kila mtu bila kujari tunatofautiana kwa kiasi kipi, tunaweza tukatofautiana na bado tukaheshimiana tu bila shida yoyote Ile,

mh Rais wetu anaendelea kututoa kimasomaso watanzania, Nchi kwa Sasa ipo mikononi mwetu watanzania ndio maana unaona watanzania tukishirikishwa katika ujenzi wa Taifa letu pendwa,

Maendeleo tunayaona na kazi ya mh Rais wetu inaonekana na kugusa maisha ya watanzania
Hawana hoja,ndio maana wanabaki kutukana
 
Data nyingi Sana zilitolewa na serikali yetu pendwa majuzi tu hapo, Hivyo zipo tu Ni suala la mtu kujionea ukweli huo Kama vile ujenzi wa vituo vya Afya 234 kutokana na tozo zetu watanzania, mama yupo kazini na ametufikia na kuwafikia watanzania, kazi iendelee
Umeelezea vizuri.
 
Lucas mwashambwa nakubaliana na wewe kabisa....tena kwa sasa ni asilimia 100. Hakuna anayepinga. Halafu pia usisahau kuweka na zile data tulikubaliana kuzisambaza. Safi sana... Tuwazime hawa wapinzani....

Zile tulizopewa juzi juzi hapa Lumumba umezisahau? Na IDs sasa uwe unachagua moja....maana unatumia zote kiasi sometimes tutaonekana tunachanganya Kikwajuni One .mi huwa nashauri unaamua week hii unatumia Id hii nyingine id nyingine.
Huna hoja.
 
Nimetembea sehemu nyingi sana Tanzania, kwenye mikusanyiko ya watu wanampongeza Rais Samia kwa kuwa na uongozi thabiti. Mpaka jana, kulikuwa na maonyesha ya biashara ya kina mama wa kila kabila, kila dini na wa kila rangi. Maonyesho hayo yanaoitwa Women Galla.

Wanawake walileta mpaka vyakula wanavyouza mitaani(mama ntilie, huku wanaiwata mama lishe) na bidhaa mbalimbali nk. waliniambia tumefanya biashara tunamshukru Mungu, na tunamshukuru Mh. Rais Samia. Kina mama wajasiriamali waliniambia wapo hapo jana ikiwa ni siku 4 na pia wakamshukuru sana Meya wa mji huo kwa kuandaa tamasha hilo.

Na wakazi wa mji huo pia walifurahi nakusema ni ubinifu haujawahi kutokea, na kuwaletea wasanii wa Mama Kimbo, waliniambia huu ni ubunifu wa hali ya juu hasa kufanyika katikati ya mji. Vijana wengi pia walishukuru kwa kupata kazi ya usalama wa eneo husika, walipata ajira.

Pia vijana wa bodaboda, bajaji, guta ya pikipiki kwa wingi wao walishukuru sana kwa kupata abiria. Wenye maguta walikuwa wakipata bidhaa za wafanyabiashara. Bila kuwasahau wenye biashara ndogo ndogo na wenye michezo ya watoto kama magari ya watoto, mabembea nk. nao walishukuru sana.
Pamoja na.mapungufu ya kila mwanadamu mmoja mmoja kwangu mimi bado tu naimani na nina mkubali Raisi wetu Mhe Samia Suluhu Hassan. Mungu azidi kumlinda na kumpa maono na utulivu zaidi. Kwa maendeleo ya Tanzania yetu🙏🏻🙏🏻
 
Hana mpinzani kabisaa, yoyote atakaye jitokeza kushindana Naye hakika atavuna aibu ya karne, maana kwa Sasa mh Rais wetu mpendwa anakubalika na kuungwa mkono na watanzania kila Kona itakayopita kutokana na utendaji kazi wake uliogusa maisha ya watanzania
Hakika.
 
Hapo bado hujaongelea kilimo ambako huko ndiko hutwambii kitu sisi wakulima ambao kwetu kilimo ndio pumzi yetu, mh Rais wetu ametoa billioni Mia moja hamsini Kama Ruzuku na kupelekea kushuka kwa mbolea na kwa Sasa mbolea inapatikana kwa elfu sabini wakati awali ilikuwa inauzwa kwa shilingi laki moja na 40
Wananchi tunaona maendeleo.Nani kama Mama.
 
Hata mpewe usimamazi wa uchaguzi bado hamuwezi kupita maana hamuwezi kupata kura za wananchi, Nani awape kura? Kwa Sera na ajenda zipi mlizonazo? Mh Rais wetu Mama Samia Hana mpinzani Wala mtu wakuweza kushindana Naye kutoka huko upinzani
Huu ndio ukweli.
 
Back
Top Bottom