99.9% ya Wananchi wanamkubali Rais Samia Suluh Hassan

Kazi za mama zipo wazi na zinaonekana wazi kwa mtu asiyejipa ukipofu, kazi za mama zimegusa maisha ya wengi, Angalia namna suala la mbolea za Ruzuku namna zilivyogusa wakulima secta ambayo imeajiri mamillioni ya watanzania nchini

Angalia Ni kundi gani ambalo ukienda utakuta halijaguswa kiutendaji na mh Rais wetu? Kila sehemu mh Rais wetu kafanya kazi inayoonekana na kugusa na kubadilisha au kurahisishia maisha ya watanzania, mfano usogezaji wa huduma za Afya Elimu maji na hata umeme kumempunguzia adha mwananchi wa kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma

pia ukienda katika Elimu unakuta kafanya kazi kubwa ambapo hata mtoto aliyetokea familia maskini anao uhakika wakupata Elimu, maana kwa Sasa jukumu la Ada mpaka kidato Cha sita lipo mikononi mwa mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani
Umefafanua vizuri.
 
Nimetembea sehemu nyingi sana Tanzania, kwenye mikusanyiko ya watu wanampongeza Rais Samia kwa kuwa na uongozi thabiti. Mpaka jana, kulikuwa na maonyesha ya biashara ya kina mama wa kila kabila, kila dini na wa kila rangi. Maonyesho hayo yanaoitwa Women Galla.

Wanawake walileta mpaka vyakula wanavyouza mitaani(mama ntilie, huku wanaiwata mama lishe) na bidhaa mbalimbali nk. waliniambia tumefanya biashara tunamshukru Mungu, na tunamshukuru Mh. Rais Samia. Kina mama wajasiriamali waliniambia wapo hapo jana ikiwa ni siku 4 na pia wakamshukuru sana Meya wa mji huo kwa kuandaa tamasha hilo.

Na wakazi wa mji huo pia walifurahi nakusema ni ubinifu haujawahi kutokea, na kuwaletea wasanii wa Mama Kimbo, waliniambia huu ni ubunifu wa hali ya juu hasa kufanyika katikati ya mji. Vijana wengi pia walishukuru kwa kupata kazi ya usalama wa eneo husika, walipata ajira.

Pia vijana wa bodaboda, bajaji, guta ya pikipiki kwa wingi wao walishukuru sana kwa kupata abiria. Wenye maguta walikuwa wakipata bidhaa za wafanyabiashara. Bila kuwasahau wenye biashara ndogo ndogo na wenye michezo ya watoto kama magari ya watoto, mabembea nk. nao walishukuru sana.
Katika hao watu uliowahoji,uliwawahoji wamachingq na mama ntilie ndio ukaja na hizi habari au umekaa na kutuletea habari ya kutunga,MTATUMIKA MPAKA LINI?
 
Nimetembea sehemu nyingi sana Tanzania, kwenye mikusanyiko ya watu wanampongeza Rais Samia kwa kuwa na uongozi thabiti. Mpaka jana, kulikuwa na maonyesha ya biashara ya kina mama wa kila kabila, kila dini na wa kila rangi. Maonyesho hayo yanaoitwa Women Galla.

Wanawake walileta mpaka vyakula wanavyouza mitaani(mama ntilie, huku wanaiwata mama lishe) na bidhaa mbalimbali nk. waliniambia tumefanya biashara tunamshukru Mungu, na tunamshukuru Mh. Rais Samia. Kina mama wajasiriamali waliniambia wapo hapo jana ikiwa ni siku 4 na pia wakamshukuru sana Meya wa mji huo kwa kuandaa tamasha hilo.

Na wakazi wa mji huo pia walifurahi nakusema ni ubinifu haujawahi kutokea, na kuwaletea wasanii wa Mama Kimbo, waliniambia huu ni ubunifu wa hali ya juu hasa kufanyika katikati ya mji. Vijana wengi pia walishukuru kwa kupata kazi ya usalama wa eneo husika, walipata ajira.

Pia vijana wa bodaboda, bajaji, guta ya pikipiki kwa wingi wao walishukuru sana kwa kupata abiria. Wenye maguta walikuwa wakipata bidhaa za wafanyabiashara. Bila kuwasahau wenye biashara ndogo ndogo na wenye michezo ya watoto kama magari ya watoto, mabembea nk. nao walishukuru sana.
WANAMKUBALI SANA. AKIPITA WANAMSHANGILIA...TOZOOOO TOZOOOO... HUKU WAKITABASAMU.
 
Back
Top Bottom