99.9% ya Wananchi wanamkubali Rais Samia Suluh Hassan

99.9% ya Wananchi wanamkubali Rais Samia Suluh Hassan

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2013
Posts
14,694
Reaction score
7,912
Nimetembea sehemu nyingi sana Tanzania, kwenye mikusanyiko ya watu wanampongeza Rais Samia kwa kuwa na uongozi thabiti. Mpaka jana, kulikuwa na maonyesha ya biashara ya kina mama wa kila kabila, kila dini na wa kila rangi. Maonyesho hayo yanaoitwa Women Galla.

Wanawake walileta mpaka vyakula wanavyouza mitaani(mama ntilie, huku wanaiwata mama lishe) na bidhaa mbalimbali nk. waliniambia tumefanya biashara tunamshukru Mungu, na tunamshukuru Mh. Rais Samia. Kina mama wajasiriamali waliniambia wapo hapo jana ikiwa ni siku 4 na pia wakamshukuru sana Meya wa mji huo kwa kuandaa tamasha hilo.

Na wakazi wa mji huo pia walifurahi nakusema ni ubinifu haujawahi kutokea, na kuwaletea wasanii wa Mama Kimbo, waliniambia huu ni ubunifu wa hali ya juu hasa kufanyika katikati ya mji. Vijana wengi pia walishukuru kwa kupata kazi ya usalama wa eneo husika, walipata ajira.

Pia vijana wa bodaboda, bajaji, guta ya pikipiki kwa wingi wao walishukuru sana kwa kupata abiria. Wenye maguta walikuwa wakipata bidhaa za wafanyabiashara. Bila kuwasahau wenye biashara ndogo ndogo na wenye michezo ya watoto kama magari ya watoto, mabembea nk. nao walishukuru sana.
 
Zaburi 12:1-5

[1]BWANA, uokoe, maana mcha Mungu amekoma,
Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.
[2]Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe,
Wenye midomo ya kujipendekeza;
Husemezana kwa mioyo ya unafiki;
[3]BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza,
Nao ulimi unenao maneno ya kiburi;
[4]Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda;
Midomo yetu ni yetu wenyewe,
Ni nani aliye bwana juu yetu?
[5]Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge,
Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji,
Sasa nitasimama, asema BWANA,
Nitamweka salama yeye wanayemfyonya
 
Nimetembea sehemu nyingi sana Tanzania, kwenye mikusanyiko ya watu wanampongeza Rais Samia kwa kuwa na uongozi thabiti. Mpaka jana kulikuwa na maonyesha ya biashara ya kina mama, wa kila kabila na kila dini, na wa kila rangi...
Yaani ulitegemea hapo Kizimkazi ukutane na upinzani dhidi ya Samia? Hata kama wapo wataminywa tu.
 
Kama bado hajamtumbua huyu jamaa basi jua ataendelea kutokukubalika kwa 99.9999%
JamiiForums62088488.jpeg
 
Kwahiyo watanzania wote ni hao wanawake mama lishe na hao bodaboda?!

Ninachoshukuru ni kuwa hizi shida na ugumu wa maisha ni watu wa chini ndio wanaoteseka sababu ya kukosa kwao akili.

Huwezi kuta mtu mwenye akili zake timamu anashiriki upuuzi kama huo. Ni hao bodaboda, mama ntilie, wazee wasio na mbele wala nyuma, na wapuuzi wengine ndio kazi yao kujitokeza kwenye hizo hafla za kipuuzi ili kuambulia 5000 na kofia halafu wanarudi majumbani mwao na kulalamika nyoko nyoko nyoko tozo..... Matako yao.

Endeleeni kusapoti na mtakomeshwa tu maana nyie ndio mnabeba limsalaba la ugumu wa maisha. Matozo, maVAT, madeni na kadhalika nyie ndio mnalipishwa katika vibukubuku mnavyonyang'anywa na mgambo na tra na halimashauri.

Shenzi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimetembea sehemu nyingi sana Tanzania, kwenye mikusanyiko ya watu wanampongeza Rais Samia kwa kuwa na uongozi thabiti. Mpaka jana...
Labda kama unasemea asilimia 99.9% ya machawa wake 😂😂😂!
 
Hiyo ipo wazi machoni na akilini mwa mamilioni ya watanzania ambao wameonyesha upendo wa kipekeee kwa mh Rais wetu kwa namna wanavyomkubali, hata Mimi huku niliko kiukweli mh Rais wetu anakubalika sijapata kuona,

watu wanaimani kubwa Sana na mh Rais wetu, watu wanasema wanahitaji mh Rais aendelee kutuongoza Kama Rais kutokana na namna alivyo gusa maisha yao.

Kama kwetu wakulima ndio hutwambii kitu juu ya mh Rais wetu kwa namna alivyogusa na kukonga nyoyo zetu baada ya kutoa Ruzuku katika mbolea na kupelekea kushuka kwa Bei ambayo Ni tofauti na msimu uliopita
 
Back
Top Bottom