51% ya wabunge wa JMT hawana shahada [Degree] | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

51% ya wabunge wa JMT hawana shahada [Degree]

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JJB, Aug 17, 2012.

 1. JJB

  JJB JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asalaam,
  Katika tafiti nilizofanya kwenye website ya bunge, zaidi ya nusu (50+%) ya wabunge hawana degree. Hii inadhihirisha jinsi gani chombo kikuu cha kutunga sheria na kusimamia serikali hakina wataalamu.
  Katika tafiti zangu nimebaini kuwa;
  1. Wabunge wengi ni form four graduates na wana poccess certificates za mambo mbalimbali.
  2. Wabunge wengi wasio na degree ni wale wa viti maalumu, huku wengi wao wakitokea CCM na CUF.
  3. Wabunge wengi watokao visiwani hawana hata deploma.(STASHAHADA) i.e 60%.
  MY CONCERN:
  HIVI BUNGE LETU LINASIMAMIA SERIKALI AU LINASIMAMIWA NA SERIKALI.
  Happy Ramadhan Kareem.
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Na katika hao 40% ambao wanaonyesha wana degree karibia 30% ni degree za kuchakachua...sasa ndio uamini kwa nini tunaona vioja na vurugu bungeni siku hizi....ni kwa sababu hatuna wasomi tuna wahuni tu huko
   
 3. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Naona umeanzisha vita ambayo wengi watachangia negative. Ila kwasasa ni vema tukawa na viongozi walioenda shule, hivyo kuwa rahisi kutafuta ufumbuzi katika changamoto mablimbali. Sikatai kuwa kuna watu ambao hawana Degree lakini wanaufanisi wa hali ya juu kuliko hata wenye nazo, ila hii imekuwa utetezi kwa wale ambao hawajaenda shule na hawajiwezi katika kupambanua changamoto zozote.

  Nafikiri tutafute njia nzuri ya kuchagua viongozi wetu, maana pia kuwa na degree siyo kuwa wewe unaweza uongozi zaidi. Bali inaondoa shaka kuwa angalau utakuwa na uwelewa wa mambo.

  Naomba nikupe assignment nyingine, je hao wenye degree ndiyo wafanisi zaidi? Na je hizo Degree ni za halali/ zinatambulika??
   
 4. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sifa na kujuakusoma na kuandika na mamuzi yao hupitishwa kwa kupaza sauti! “Serikali itaendelea kutumia sheria mbaya mpakazitakpobadlishwa’’ Pinda
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Vioja na Vurugu zenyewe bora vingekuwa ni mabishano ya hoja, worse inakuwa ni kushabikia au kuponda hoja kwa vile tu zimetolewa na fulani!
  In actual fact haihitaji hata kufanya utafiti kwenye website!...you just watch the session for 30 min...u have all the data!
   
 6. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,792
  Likes Received: 3,879
  Trophy Points: 280
  hao wenye degree mbona nao hatuoni tofauti na wasio na degree hasa kutoka ccm! mfano wewe unaona tofauti ya mchango kati ya mwigulu mwenye degree first class ya uchumi na Lusinde wa darasa la saba?? AU ipo tofauti ya kimtizamo na mchango kati ya dr.Mary Nagu na Ole sendeka??
   
 7. JJB

  JJB JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kenyans have a bill,waiting the signature of the head of states which commands each MP should have atleast a degree to support his/her stay in the house of representatives. TANZANIANS WORK UP, LETS BE OURSELVES IN 2015.
   
 8. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wanaotunga hizo sheria ni wao. Hebu jaribu kufikiria kama mswaada wa namna hii ukipelekwa bungeni, utakwamishwa kwa asilima ngapi? Lazima itakuwa sawa au zaidi ya 51%. Bunge letu linahitaji wasomi wenye uelewa wa mambo mbalimbali ili tusonge mbele.
   
 9. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  ASILIMIA 99.9 YA WABUNGE WA CDM WANADEGREE MBILI,ASILIMIA 99 YA WABUNGE WA CCM HAWANA HATA DEGREE MOJA,ASILIMIA 80 YA WABUNGE WA CUF HAWANA DEGREE.

  ASILIMIA 99.9 YA WABUNGE WAKRISTO WANA DEGREE ,ASILIMIA 99.9 YA WABUNGE WAISLAM HAWANA HATA DIPLOMA


  ASILIMIA 99 YA WABUNGE KUTOKA ZENJI WAMEMALIZA MADRASATUL TUU HAWAJUI HAT FORM ONE nI NINI
   
 10. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  sidhani kama taifa linahitaji utitiri wa shahada wakati huu lakini linahitaji watanzania wenye uthubutu wakuleta mabadiriko ya kweli kwa nchi na maisha ya watanzania wenzao
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Kuwa na Shahada si lazima ni Hekima na Uongozi Bora; Wale waliokuwa Mafisadi wanawakatia Umeme wananchi Nchi Nzima

  Hao wote walikuwa na Madigree hawakujali Uzalendo, Walijali ni lini Matumbo yao yatajaa makaratasi ya kijani; Green US Dollars

  Wengine Wana-Degree wanaona Mimi ni Mbunge nitapata kidogo kidogo kwenye Mauzo ya Bangi... Wengine 10% za Madini

  Wengine ndio hao Wasomi kabisaa wanaiuza Serengeti...

  Lakini kuna ambao hawajasoma na Wanapendwa na Wananchi wao sababu Wanatekeleza Matakwa yao na pia kuwatumikia

  Ipasavyo, na ni Mzalendo hakwenda kutafuta hizo 10% au kujitangaza kama wengine Mfano; SUGU yeah Elimu ndogo lakini

  Dunia Imemfundisha Mengi sidhani kama Wamachinga wa Mbeya - Watu wa chini kabisa; watalalamikia Uongozi wake; au

  Daktari Mbeya atalalamikia Uongozi wake... Uongozi wake hauna Matabaka; ni Mzalendo; hapo Elimu haikutakiwa kama wewe

  Utakavyo...
  Jamaa zako wote wenye ELIMU WANA UWALAKINI; WEZI; WATOROSHAJI UTAJIRI WA NCHI.
   
 12. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii ni kwa wachache mno kama ulivyotoa mfano kwa Sugu na tena wenye exposure kubwa ya kimaisha. Lakini wengi na hasa wasiokuwa na exposure ya maisha zaidi ndo wanaotudidimiza. Tukubali kwamba msomi ananafasi kubwa zaidi ya kutumia elimu yake kujenga au kubomoa kwa umakini zaidi kuliko asiyekuwa na elimu. Kikubwa tuchague wasomi ambao watatumia elimu zao kujenga nchi.Huoni utofauti ya Dr. za ukweli na wengine?
   
 13. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  chukulia mfano mtu amesoma degree ya umeme, mwingine ya muziki, mwingine ya beauty therapy, mwingine ya kilimo. Degree hizo zitawasaidia vipi katika kuamua kama mpaka wa Tanzania ni Malawi uko ziwani au nchi kavu, utawasaidia vipi kujua kwa daraja la Kigamboni siyo muhimu zaidi ya madaraja yanayounganisha wilaya mbalimbali nchini?
  Hakuna uhusiano kati ya degree na ubunge. Unawakilisha mawazo na matakwa ya watu sio kuweka akili zako kwenye mahitaji yao. Sifa ya mwakilishi ni kuheshimu matakwa ya anaowawakilisha. Sasa degree ya nini hapo? Mtu anaweza asiwe na cheti chochote lakini akawa ana ujuzi mkubwa wa mambo mbalimbali. Kwa reference someni historia ya malcolm X.
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Wametajwa Wabunge wa CUF kuwa wengi wao hawana hizo ELIMU; Lakini wabunge wa CUF ni wakali kweli kuhusu

  UFISADI, CCM hawana advantage kuhusu Uzalendo Wamechota Chota kila Mahali Utajiri wa Nchi, yaani hadi Madiwani wao

  Ni wachotaji kwa Baraka ya baadhi ya Wabunge kwenye Kamati za Bunge, na Wengi wao humo ndani ni Wenye Madigree

  Wewe Speaker anakataza Wabunge kutoongelea mbunge gani anatoa rushwa jimboni kwake? Huyu Mama ana Degree

  Kwanini anafanya hivyo? Si Maficho? it is totally crazy More Money Mongering... Hii haina sababu ya Usomi; Ni Uozo wa

  Wabunge wa CCM; RADA issue mshitakiwa Mkubwa ni Mwanasheria Mkuu, Sio wabunge ambao hawajasoma...

  Kwahiyo Mnatakwa Wasomi wote ili Nchi yooote iuzwe? tutakuwa kama CONGO-Kinsasha? Ubaya ni nini hamtaweza kuishi

  Uingereza au Nchi yoyote ya UEROPE labda Malaysia au Thailand...
   
 15. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Miongoni mwa sifa za mtu kuwa mbunge kwa mujibu wa katiba ni awe mtanzania aliyefikisha umri wa miaka 21 na angalau awe amemaliza darasa la saba.
   
 16. K

  KABALE Member

  #16
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nimekuja kuelewa katika vitu ambavyo vinawatenganisha Watanzania ni elimu. Mtu akipost thread kuhusu ELIMU anakumbana na mawazo kinzani. Lakini ukweli unabaki pale pale kwamba ELIMU tena ya UKWELI kwa ustawi wa taifa letu. Ndiyo maana unakuta watu wabunge wetu kwenye bunge la Afrika ya Mashariki toka tanzania wana waachia uwanja wenzao toka Kenya, Uganda na Rwanda. Hawajui lugha na hoja hakuna...kisa tunatanguliza c=CHAMA fulani kuliko weledi...Njia ya mwongo ni fupi...Tubadilike
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Sitetei ujinga,

  Lakini

  Luiz Inácio Lula da Silva alikuwa na shahada gani? Na kaacha legacy gani amabayo wasomi zaidi yake hawakuweza?

  Na shahada zenyewe mnazozungumzia ni zipi? Hizi za kina first class economist Mwigulu Nchemba na Baba Rizi Mkuu wa kaya au nyingine?

  Nipe Lula mmoja asiye na shahada over any Kikwete with a Ph.D!

  Naweza kuondoa standard ya degree kwa mtu kama Lula (trade unionist) Kawawa (trade unionist) Zuma (freedom fighter of sorts) kwa sababu nikiwauliza "kwa nini huna degree?" wanaweza kunipa sababu itakayonifanya nione kwamba wana sifa za uongozi kubwa kuliko degree, na pengine wamejifunza mengi zaidi ya degrees ambazo mara nyingine zinakuwa si relevant.

  Kuna watu wanaanza uongozi tangu wadogo, wanatoka katika familia masikini katika nchi masikini, nchi zenyewe zetu hizi chuo kikuu kimoja mpaka juzi. Wengine ilibidi wafanye kazi kuwasomesha wengine, wengine ilibidi wapiganie uhuru ili nchi iwepo, wengine ilibidi waende kwenye chuo cha dunia ma trade unionist huko,wengine ma enterpreneurs kama kina Bill Gates wameona chuo kitawachelewesha tu.

  Kwa hiyo, swala muhimu ni maelezo kwa nini mtu hana degree.

  Mie mtu anayeniambia alipata nafasi ya kusoma akashindwa kwa sababu za kifamilia - yeye alikuwa anategemewa kufanya kazi na mama yake alikuwa mgonjwa, hakuweza kuacha kazi kwenda kuchukua degree- bado nampa maksi zake za kujitoa na kuwa kiongozi.

  Tuangalie mambo kwa undani zaidi, na hii brainwashed education ya kupangiwa na wazungu tusii overrate.

  Elimu haipimwi kwa degree.

  Ingekuwa hivyo tusingeona madudu Magogoni pale ambapo mpaka leo watu wanatumia email ya yahoo at the risk of national security na wandishi wao hawajui kuandika hata sentensi moja bila kupindisha sarufi.

  Tuongelee wabunge wenye mchango wa kisomi na wasio na mchango wa kisomi.

  Usomi ni werevu, usambe shahada.
   
 18. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Ni kweli; nadhani wengi wetu tuna equate lugha ya kiingereza na elimu; Rais wa Brazil hakuwa na shida sana kwani lugha yao ndio lugha rasmi ya taifa na hata anapo interact na wenzake, bado anakuwa on point kwani kinachoendelea ni tafsiri; kiswahili kingekuwa katika hali hiyo, mbona wanasiasa wetu wenye hazina tosha ya misamiati wangetupeleka mbali sana;
   
 19. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Katiba mpya lazima tubadili hapo kwenye ELIMU iwe hivi angalau awe na degree moja. Hii itasaidia kuondoa wabunge incompetent na WAUZA unga kama akina Munde Tambwe.
   
 20. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Upo sahihi lakini tujiandae kupata upinzani mkali kweli kweli juu ya hilo kwani hata wakati wa uchaguzi, mara nyingi wenye elimu huwa wanatengenezewa fitina na zinaingia vizuri kwa wapiga kura wengi. Wenzetu wa UK kwa mfano hali yao ipo kama ifuatavyo:

   Nine in ten MPs in 2010 attended university – by far the highest proportion of any
  Parliament to date. This includes just under three in ten who were educated at either
  Oxford or Cambridge universities. Oxford has produced 102 MPs serving in the 2010
  Parliament.


   38% of Conservative MPs were educated at Oxford or Cambridge compared with
  20% of Labour MPs and 28% of Liberal Democrat MPs.


   Newly elected MPs were even more likely to be graduates – with 94% attending a
  university,
  including 69% who had attended a leading research university, and 28%
  who had attended Oxbridge.

  Source: The Educational Backgrounds of Members of Parliament in 2010 - Sutton Trust
   
Loading...