Wabunge wa Zanzibar ndani ya bunge la JMT kazi yao ni ipi hasa?

jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
19,193
36,122
Kipindi cha maswali na majibu wabunge wa Tanganyika huuliza masuala mbalimbali kuhusu utekerezaji wa serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Pia katika kuchangia bajeti mbalimbali za wizara serikali mfano wizara za maji..tamisemi..uchukuzi..afya..ambazo nyingi sio za masuala ya muungao na wala hazitekezi na kusimamia miradi hiyo upande wa zenji.

Je, wabunge hawa wa zenji kazi yao hasa huwa nini kwenye mikutano hii ya bunge ambao asilimia 95% hujadili bajeti ya Tanganyika kupitia koti la JMT?

Mapendekezo.

Wabunge kutoka Zanzibar waingie bungeni pale tu masuala ya muungano yanapo jadiliwa ili kupunguza upotevu wa fedha za walipa kodi wa Tanganyika kutoka kwa wabunge wasio kuwa na mchango wowote na wasio faidika na miradi ambayo haitekerezwi upande wa visiwani.

Tupunguze utiriri huu wa wabunge wasio na faida ndani ya bunge na fedha hizo ziende kutekeleza maendeleo ya wanachi kupunguza ukali wa maisha.

N.b: Nafahamu wabunge wengi ni mbeleko ya JPM kupitia tume feki ya uchaguzi wala hawatokani na wananchi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi cha maswali na majibu wabunge wa Tanganyika huuliza masuala mbalimbali kuhusu utekerezaji wa serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Pia katika kuchangia bajeti mbalimbali za wizara serikali mfano wizara za maji..tamisemi..uchukuzi..afya..ambazo nyingi sio za masuala ya muungao na wala hazitekezi na kusimamia miradi hiyo upande wa zenji.

Je wabunge hawa wa zenji kazi yao hasa huwa nini kwenye mikutano hii ya bunge ambao asilimia 95% hujadili bajeti ya Tanganyika kupitia koti la JMT?.

Mapendekezo.

Wabunge kutoka Zanzibar waingie bungeni pale tu masuala ya muungano yanapo jadiliwa ili kupunguza upotevu wa fedha za walipa kodi wa Tanganyika kutoka kwa wabunge wasio kuwa na mchango wowote na wasio faidika na miradi ambayo haitekerezwi upande wa visiwani.

Tupunguze utiriri huu wa wabunge wasio na faida ndani ya bunge na fedha hizo ziende kutekeleza maendeleo ya wanachi kupunguza ukali wa maisha.

N.b: Nafahamu wabunge wengi ni mbeleko ya JPM kupitia tume feki ya uchaguzi wala hawatokani na wananchi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza muungano uvunjwe hauna faida
 
Kosa sio wabunge wa Zanzibar kuingia kwenye mikutano ya Bunge la JMT ambalo linajadili bajeti ya Tanganyika, Bali ni kwanini bajeti ya Tanganyika inajadiliwa kwenye Bunge la JMT?
 
Back
Top Bottom