51% ya wabunge wa JMT hawana shahada [Degree]

Suala la msingi la kikatiba ni kutoa fursa sawa kwa kila mwananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote. Iwe kwenye kuongoza au kuongozwa.

Unapoweka vigezo vya elimu ya shahada kwa mfano, ni sawa na wewe kusema hata mtu awe na uwezo kiasi gani na awe amepeleka maendeleo kiasi gani kwa wananchi wake, madamu hajarasimishwa kwa kutumia elimu ya Mzungu, basi huyo hafai.

Hii inapingana na hata kanuni za msingi za utaratibu wa utawala kwenye jamii za Kiafrika.

Sawa mkuu, kama ni hivyo basi tuache tu Ndege wanaofanana WARUKE pamoja.
 
The takeaway from this thread is very simple.

Do no confuse "education" with "degree".

The two may run concomitantly or discordantly.
 
hao wenye degree mbona nao hatuoni tofauti na wasio na degree hasa kutoka ccm! mfano wewe unaona tofauti ya mchango kati ya mwigulu mwenye degree first class ya uchumi na Lusinde wa darasa la saba?? AU ipo tofauti ya kimtizamo na mchango kati ya dr.Mary Nagu na Ole sendeka??
Mi nna shaka na hiyo elimu ya mwigulu nchemba kwa lusinde no doubt anachosema kinareflect education level yake ya std 7 ila wana mtera kweli walichagua au walichaguliwa. Na huyu mchumi wa mapwepande hebu a act lyk educated kuwa rafiki na lusinde sio maana yake awe kaa yeye. Education is only education when it changes someones behaviour. Hawa jamaa wako obssessed na system I mean dumb system.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Tatizo Watanzania siku hizi wanazuzuka sana na shahada za chuo kikuu. Na ukiwa dokta ama profesa ndiyo hadhi inapanda.

Laiti watu wangejua kuwa shahada za chuo kikuu hazihusiani na sifa ya uongozi labda tusingekuwa na watu ambao shahada zao zina mushkeli.
 
Historia inatueleza kwamba mwaka 1961 kulikuwa na only a handful of University graduates - hawakuwa wanafika kumi kati ya jumla ya watanzania milioni tisa (1961). Hivi, out of curiosity tu, Je Mwalimu asingekuwa na elimu aliyokuwa nayo na badala yake angekuwa na upeo sawa na the rest of the population au angetokea mtu mwingine mwenye upeo sawa na the majority in the population, leo Tanzania ingekuwa wapi? Nadhani mazingira ya uongozi yanahitaji elimu, hasa katika mazingira ya dunia ya sasa ambayo yanazidi kuwa complex na yanayohitaji umakini na uwezo wa hali ya juu kuyatatua; Uwepo wa viongozi wenye elimu ambao wanashindwa ku 'deliver' isiwe ndio hoja ya msingi ya kusema tuwajaribu hata wasio na elimu; huku ni kujidanganya na tutazidi kudidimia; suala muhimu ni kuhimiza fursa za elimu zipanuliwe zaidi, huku jamii ikiwekeza katika viongozi wasomi, lakini muhimu zaidi, kuwe na mechanism ya ku monitor 'performance' ya viongozi hawa;

Kwa hiyo unataka kusema nini?

Kwamba by 1961 kwa sababu hatukuwa na University graduates basi watu hawakuwa na elimu?

Hivi Mtwa Mkwawa alivyokuwa anawaadhibu Wajerumani kule pande za Kitonga, alikuwa graduate wa University gani vile?

Alihitimu degree ya "American Civil War Tactics" au "Napoleonic Field Ambush"?
 
Kwa hiyo unataka kusema nini?

Kwamba by 1961 kwa sababu hatukuwa na University graduate basi watu hawakuwa na elimu?

Hivi Mtwa Mkwawa alivyokuwa anawaadhibu Wajerumani kule pande za Kitonga, alikuwa graduate wa University gani vile?

Alihitimu degree ya "American Civil War Tactics" au "Napoleonic Field Ambush"?

Kama maisha yangu yangekuwa confined just within my yard nyumbani, elimu ya kupewa na baba na mama yangu ingenitosha kabisa to survive in such a small world; but not in today's world ambayo u dont exisit alone as a village au household bali kwa interactions na jamii nyingine na maisha yetu yakiwa yanakuwa influenced na factors way beyond our borders, na mahusiano haya yakiwa in a very unfair manner, huku complexities zinazidi kuongezeka and the only way to survive ni kukabiliana with such - kijamii, uchumi, kisiasa, sayansi na teknolojia n.k.
 
Sawa mkuu, kama ni hivyo basi tuache tu Ndege wanaofanana WARUKE pamoja.

Usisahau kwamba hakuna utafiti unaonyesha kuwa kila mtu anapokuwa ana shahada ya juu zaidi basi ana uwezo mkubwa zaidi wa kuongoza.

Mfano mdogo tu, kuna maprofessa hata kuongoza darasa hawawezi, seuze nchi nzima!

Tunapigania watu wapate elimu, kwa fursa sawa nchi nzima, lakini uchaguzi wa anaefaa kuongoza wananchi uachwe kwa wananchi wenyewe.
 
Kiranga,

unathamini utamaduni, jambo ambalo ni muhimu sana; pia unajali hali za watu wengi (kielimu), jambo ambalo pia ni muhimu sana; lakini tunapotofautiana ni pale unapoashiria kwamba kilicho bora zaidi ni kuwaacha ndege wanaofanana waruke pamoja;
 
Kama maisha yangu yangekuwa confined just within my yard nyumbani, elimu ya kupewa na baba na mama yangu ingenitosha kabisa to survive in such a small world; but not in today's world ambayo u dont exisit alone as a village au household bali kwa interactions na jamii nyingine na maisha yetu yakiwa yanakuwa influenced na factors way beyond our borders, na mahusiano haya yakiwa in a very unfair manner, huku complexities zinazidi kuongezeka and the only way to survive ni kukabiliana with such - kijamii, uchumi, kisiasa, sayansi na teknolojia n.k.

Kwamba Mkwawa alimpigaje Mjerumani bila degree hujajibu, swali lililenga kuonyesha kwamba kuna elimu iliyokuwa haipimiki kwa degree.

Naelewa umuhimu wa degree, lakini let's not dumb down the meaning of education by equating "education" to "degree".

That in itself will be a lack of education.
 
Asalaam,
Katika tafiti nilizofanya kwenye website ya bunge, zaidi ya nusu (50+%) ya wabunge hawana degree. Hii inadhihirisha jinsi gani chombo kikuu cha kutunga sheria na kusimamia serikali hakina wataalamu.
Katika tafiti zangu nimebaini kuwa;
1. Wabunge wengi ni form four graduates na wana poccess certificates za mambo mbalimbali.
2. Wabunge wengi wasio na degree ni wale wa viti maalumu, huku wengi wao wakitokea CCM na CUF.
3. Wabunge wengi watokao visiwani hawana hata deploma.(STASHAHADA) i.e 60%.
MY CONCERN:
HIVI BUNGE LETU LINASIMAMIA SERIKALI AU LINASIMAMIWA NA SERIKALI.
Happy Ramadhan Kareem.

Kazi kuu ya bunge ni kutunga sheria, ningetegemea walau 50% wawe wamepitia masomo ya sheria kwa kiwango fulani. Wenye digrii nyingine wajikite kwenye taasisi za maendeleo na utafiti.
Kutokufahamu sheria ndio kunafanya Bunge liwedhaifu. Fananisha michango ya Lisu Bungeni.
Pia Ukizungumzia digrii inabidi uelewe imepatikana vipi na wapi. Digrii ya Lukuvi imepatikana dukani sawa na ya Mrema
 
Kiranga,

unathamini utamaduni, jambo ambalo ni muhimu sana; pia unajali hali za watu wengi (kielimu), jambo ambalo pia ni muhimu sana; lakini tunapotofautiana ni pale unapoashiria kwamba kilicho bora zaidi ni kuwaacha ndege wanaofanana waruke pamoja;

And what exactly do you mean by "wache nedege wanaofanana waruke pamoja"?
 
Usisahau kuwa hakuna utafiti unaonyesha kuwa kila mtu anapokuwa ana shahada ya juu zaidi basi ana uwezo mkubwa zaidi wa kuongoza.

Mfano mdogo tu, kuna maprofessa hata kuongoza darasa tu hawawezi, seuze nchi nzima!

Tunapigania watu wapate elimu, kwa fursa sawa nchi nzima, lakini uchaguzi wa anaefaa kuongoza wananchi uwachwe kwa wananchi wenyewe.

Huu ni mjadala tofauti sasa; kuwa na tatizo hilo ni kutokana na factors nyingi ambazo hatujazijadili kwani kuna both endogenous and exogenous factors on why tunakabiliwa na janga hili; lakini bado it doesnt disqualify umuhimu wa elimu miongoni mwa both, wanaoongoza na wanaoongozwa; dunia ya sasa is too complex kukabiliana nayokwa mwendo uliokuwa otherwise; viongozi wachache ambao uwezo wao kuongoza hauendani na ukubwa wao wa elimu wasituvuruge tukadhani kwamba tutaweza kusonga mbele bila ya elimu miongoni mwa wanao ongoza na wanaoongozwa, hasa wale wanao ongoza, ili mradi wawe na elimu relevant kutatua matatizo ya jamii zao, lakini muhimu zaidi, uwezo wa kutumia kikamilifu elimu hizo na pia uzalendo kwa taifa lao;
 
Kazi kuu ya bunge ni kutunga sheria, ningetegemea walau 50% wawe wamepitia masomo ya sheria kwa kiwango fulani. Wenye digrii nyingine wajikite kwenye taasisi za maendeleo na utafiti.
Kutokufahamu sheria ndio kunafanya Bunge liwedhaifu. Fananisha michango ya Lisu Bungeni.
Pia Ukizungumzia digrii inabidi uelewe imepatikana vipi na wapi. Digrii ya Lukuvi imepatikana dukani sawa na ya Mrema

Mie nimeuliza, degree zenyewe ni zipi?

Achana na hizo za Lukuvi na Mrema za kununua.

Hao waliopita "Choo Kikuu" wenyewe si tunawaona, wana afueni gani ya ku justify kwamba ndio wawe standard?

Wewe mtu na akili zake anaweza kuniambia Mzengo Pinda anayesema wakuu wa mikoa na wilaya wapiganie CCM waziwazi (graduate wa Law UDSM 1975 huyu) ndiye awe standard bearer?
 
Kazi kuu ya bunge ni kutunga sheria, ningetegemea walau 50% wawe wamepitia masomo ya sheria kwa kiwango fulani.

Unakosea sana.

Kama masomo ya sheria ni muhimu hivyo (ikiwemo shahada), kwa nini nchi kama Marekani haina hiyo requirement kwenye katiba yake kuhusiana na lawmakers wake na majaji wa mahakama kuu yake?
 
And what exactly do you mean by "wache nedege wanaofanana waruke pamoja"?

kwamba jamii zetu kwa kiasi kikubwa zina watu ambao hawakupata bahati ya kwenda shule vizuri; lakini wamekuwa wanachagua viongozi wenye elimu watatua matatizo yao; lakini viongozi hawa wamekuwa wanawaangusha; hivyo bora wajirudi na kuchagua viongozi wanaofanana nao kielimu, na kwa pamoja pengine watafanikiwa kujiletea maendeleo; it can definately work, but i don't believe in that school of thought;
 
Hivi yale majimbo yanayowakilishwa na maprofesa na madokta yenyewe maendeleo yake yakoje ukilinganisha na jimbo kama la Mtera linalowakilishwa na Livingstone Lusinde?
 
Mie nimeuliza, degree zenyewe ni zipi?

Achana na hizo za Lukuvi na Mrema za kununua.

Hao waliopita "Choo Kikuu" wenyewe si tunawaona, wana afueni gani ya ku justify kwamba ndio wawe standard?

Wewe mtu na akili zake anaweza kuniambia Mzengo Pinda anayesema wakuu wa mikoa na wilaya wapiganie CCM waziwazi (graduate wa Law UDSM 1975 huyu) ndiye awe standard bearer?

Unajua kiranga, elimu sio kigezo peke yake cha kutengeneza mazingira yenye utawala bora; tatizo unalolizungumza ni kweli lipo, lakini wengi humu tunakuwa hatuelewani kwasababu hatujapanua mjadala zaidi; ningeshauri sasa tuanze kuangalia endogenous and exogenous factors zinazopelekea uwepo wa tatizo hili miongoni mwa viongozi wenye elimu, lakini while we hold constant umuhimu wa elimu miongoni mwa viongozi katika kutatua matatizo ndani ya jamii wanazoziongoza;
 
Back
Top Bottom