51% ya wabunge wa JMT hawana shahada [Degree]

Ni kweli; nadhani wengi wetu tuna equate lugha ya kiingereza na elimu; Rais wa Brazil hakuwa na shida sana kwani lugha yao ndio lugha rasmi ya taifa na hata anapo interact na wenzake, bado anakuwa on point kwani kinachoendelea ni tafsiri; kiswahili kingekuwa katika hali hiyo, mbona wanasiasa wetu wenye hazina tosha ya misamiati wangetupeleka mbali sana;

Having said all that I have said.

I want to emphasize kwamba, kama nilivyosema mwanzo, sitetei ujinga.

Wabunge wetu wenye degree tu ni vituko.

Sasa ndio maana wakuu wanaona bora watumie rule of thumb tu kuwatenganisha "the sheep from the goat" kwa kutumia degree, kitu ambacho si sawa.

Ila ukweli ni kwamba wabunge wetu wengi- degree or not- hasa wale walioibuka ibuka tu bila kupata world class exposure, wanatia kichefuchefu.

Mtu unaweza kuwa unasikiliza mchango wa mbunge ukaamua kuflip channel au kuzima redio.

Kwa sababu hata ukiondoa swala la substance, presentation tu tabu unamsikiliza mtu ana meander ovyo kama an inexperienced teenager unexpectedly exposed infront of a massive crowd.

We ma experienced lawyers walio graduate toka 1975 huko kina Mizengo Pinda, wamekaa usalama wa taifa na ikulu wakaenda kuwa wabunge na mawaziri all those years tunasikia wanavyochemka kila siku.

I shudder to equate degrees and usomi. Kwa sababu hao kina kabwela ndo itakuwa ajabu. But that need not be reduced to a rule of thumb.There is always an outlier.

And we don't want to be so simplistic to dishearten the occassional brilliant Mnyika sans degree.
 
bungeni kuna Phd & professors kibao lakini ukienda kwenye profiles zao utakuta wao ndio wanaoongoza kwa kuwa na michango michache, ukiwauliza umesaidia nini nchi tangu uingie bungeni wanakujibu "serikali haisikilizi/haithamini au haitaki kutumia taaluma/ ushauri wetu"
Elimu usipoitumia haina faida hata msigwa alisema bungeni kuna maprofesa wanafikiria kama mtoto wa darasa la pili
 
mkubwa hujakosea ndo mana mbunge mmoja aliwahi kuchorwa amebeba kamusi anaingia nayo mjengoni
 
Katiba mpya lazima tubadili hapo kwenye ELIMU iwe hivi angalau awe na degree moja. Hii itasaidia kuondoa wabunge incompetent na WAUZA unga kama akina Munde Tambwe.

Hii approach ina matatizo mawili.

1. Inaingilia haki ya mwananchi wa Tanzania kuongoza. Kwamba kwa kumuwekea masharti ya ziada Mtanzania kuongoza, unaondoa uchaguzi wa viongozi kutoka kwa wananchi na unaupeleka kwa Ombudsmen. Kwa kutumia sheria hiyo hiyo ya "mbunge lazima awe na degree" tungeweza kuondoa vilaza wengi, lakini pia hata John Mnyika, mtu ambaye wengi wanamkubali umakini wake na ametoa mchango mkubwa kuliko wengi wenye degree, asingeweza kuwa na nafasi ya kuwa mbunge. Tutajenga matabaka ya wazi yasiyo na sababu na kuwaondolea wananchi uchaguzi.

2. Kuuza unga si monopoly ya wasiosoma. Waliosoma hawako above kuuza unga kwa hiyo kama unataka kuhakikisha hatupati wabunge watakaotuaibisha kwa habari za kuuza unga kataza watu waliokuwa convicted kwa kesi hizo kugombea ubunge, degree haina uhusiano wa moja kwa moja na kuuza unga.

3. Bado hujanijibu swali la Lula.

Tutenganishe "ELIMU" na "DEGREE".

Unaweza kuwa na degree bila elimu = Mwigulu Nchemba

Unaweza kuwa na elimu bila degree = John Mnyika (at least by his bunge page)

Tusitake kui reduce elimu iwe quantifiable by paper credentials.
 
Kwa nchi ambayo elimu yake haipatikani kwa usawa na haki kwa wote, kuweka kigezo cha degree ni kuwadhulumu haki wengi wa raia nchini.

Hii inaweza hata kupelekea kujengeka kwa tabaka la familia zinazotoa viongozi kwa vile zina uwezo wa kusomesha watoto wao katika shule nzuri ambazo zinawapa karibia uhakika wa kufika chuo kikuu na kupata degree.

Tukitaka kigezo hicho elimu ya shahada kitumike basi kwanza tuhakikishe watu wote wana fursa sawa ya kupata elimu hadi ya chuo kikuu
 
Wabunge wetu wenye degree tu ni vituko.

Ila ukweli ni kwamba wabunge wetu wengi- degree or not- hasa wale walioibuka ibuka tu bila kupata world class exposure, wanatia kichefuchefu.

Mtu unaweza kuwa unasikiliza mchango wa mbunge ukaamua kuflip channel au kuzima redio.

Kwa sababu hata ukiondoa swala la substance, presentation tu tabu unamsikiliza mtu ana meander ovyo kama an inexperienced teenager unexpectedly exposed infront of a massive crowd.

We ma experienced lawyers walio graduate toka 1975 huko kina Mizengo Pinda, wamekaa usalama wa taifa na ikulu wakaenda kuwa wabunge na mawaziri all those years tunasikia wanavyochemka kila siku.

I shudder to equate degrees and usomi. Kwa sababu hao kina kabwela ndo itakuwa ajabu. But that need not be reduced to a rule of thumb.There is always an outlier.

And we don't want to be so simplistic to dishearten the occassional brilliant Mnyika sans degree.

Nadhani pia wengi tunafanya kosa la kufananisha Elimu na Intelligence. Binafsi sidhani kama elimu pekee inakusaidia kama haupo intelligent. Ndio maana unakuta mtu anaweza kuwa highly intelligent lakini hana elimu au anakuwa highly educated lakini hayupo intelligent.

Kwanini inakuwa hivi? Ni vigumu kuja na jibu kamili, lakini kwa mtazamo wangu ambao pengine ni mfupi ni kwamba, while Elimu ni knowledge unayopata katika mazingira rasmi, hasa shuleni/chuo n.k, Intelligence ni UWEZO wa kupata that knowledge/kujifunza au to acquire ujuzi au maarifa fulani katika mazingira hayo, lakini muhimu zaidi ni kwamba uwezo huu wa kujifunza/acquire ujuzi/maarifa ni lazima uendane na UWEZO wa kutumia ujuzi au maarifa hayo katika mazingira yako. Kwahiyo key issue hapa ni "UWEZO" to acquire knowledge (elimu shuleni) na "UWEZO" to utilize whatever you have acquired (elimu/knowledge shuleni). Lakini vile vile, unaweza ukakutana na mtu mwenye both – very highly educated and highly intelligent lakini bado akawa mjinga kabisa. Why? I don't know, may be kwetu ni kitu inherent/our nature as humans.
 
hao wenye degree mbona nao hatuoni tofauti na wasio na degree hasa kutoka ccm! mfano wewe unaona tofauti ya mchango kati ya mwigulu mwenye degree first class ya uchumi na Lusinde wa darasa la saba?? AU ipo tofauti ya kimtizamo na mchango kati ya dr.Mary Nagu na Ole sendeka??
Nimeipenda hii.
kwa sasa watu hawaoni tofauti ya kuchagua msomi au la kuwawakilisha. Ni mpaka pale wawakilishi wasomi watakapoamua kuacha kutumia siasa ku-analyse issues na kutumia elimu zao, otherwise wote wanafanana tu
 
Until then........

Until then tuwaache watu waliopata elimu ya lazima ya msingi wagombee. Iwapo wabunge wenye shahada watafanya vizuri sana kwenye Bunge na wasiokuwa na shahada watafunikwa katika michango na shughuli zao bungeni, nadhani kunaweza kutokea natural selection of a sort, ambapo wananchi wenyewe wakaanza kuchagua wenye shahada.

Lakini bado hapo hakutakuwa na mwananchi aliyenyimwa fursa ya kugombea nafasi ya uongozi.
 
Nadhani pia wengi tunafanya kosa la kufananisha Elimu na Intelligence. Binafsi sidhani kama elimu pekee inakusaidia kama haupo intelligent. Ndio maana unakuta mtu anaweza kuwa highly intelligent lakini hana elimu au anakuwa highly educated lakini hayupo intelligent.

Kwanini inakuwa hivi? Ni vigumu kuja na jibu kamili, lakini kwa mtazamo wangu ambao pengine ni mfupi ni kwamba, while Elimu ni knowledge unayopata katika mazingira rasmi, hasa shuleni/chuo n.k, Intelligence ni UWEZO wa kupata that knowledge/kujifunza au to acquire ujuzi au maarifa fulani katika mazingira hayo, lakini muhimu zaidi ni kwamba uwezo huu wa kujifunza/acquire ujuzi/maarifa ni lazima uendane na UWEZO wa kutumia ujuzi au maarifa hayo katika mazingira yako. Kwahiyo key issue hapa ni "UWEZO" to acquire knowledge (elimu shuleni) na "UWEZO" to utilize whatever you have acquired (elimu/knowledge shuleni). Lakini vile vile, unaweza ukakutana na mtu mwenye both – very highly educated and highly intelligent lakini bado akawa mjinga kabisa. Why? I don't know, may be kwetu ni kitu inherent/our nature as humans.

Ushaona?

Kuna watu wako perceptive na assertive bila kupata formal education, hii ndiyo wengine wanaita "street smarts". Mtu anaweza ku connect the dots kwa kuangalia bottom lines tu bila hata kupata advantage ya ku analyze details.

Anaweza ku "connect the dots".

Mwingine amesoma kakariri kilomita za barabara zote kama Magufuri, lakini ukimuuliza "the shortest distance from Muleba to Songea by road" anaweweseka, ukimtoa kidogo tu kutoka kile alichojitayariha nacho unamuumiza. Hawezi ku connect the dots.
 
Until then tuwaache watu waliopata elimu ya lazima ya msingi wagombee. Iwapo wabunge wenye shahada watafanya vizuri sana kwenye Bunge na wasiokuwa na shahada watafunikwa katika michango na shughuli zao bungeni, nadhani kunaweza kutokea natural selection of a sort, ambapo wananchi wenyewe wakaanza kuchagua wenye shahada.

Lakini bado hapo hakutakuwa na mwananchi aliyenyimwa fursa ya kugombea nafasi ya uongozi.

Very good observation.

Ukiwa na kigezo cha ubunge ambacho hakipo accessible kwa wananchi wote, kimsingi unasema kwamba haki ya uongozi unaitoa kwa sehemu kubwa ya wananchi.

Matokeo yake walioongoza na familia zao ndio watakuwa wanaongoza wao kila siku huku wengine ambao hawana uwezo wa kupata hiyo degree ndio watakuwa wa kuongozwa daima.

Sifa za uongozi zimewekwa simple kwa sababu maalum. Sababu yenyewe ni kwamba ultimately wananchi wenyewe ndio waachiwe kuchagua.

Sio some formula ambayo hata hatuna uhakika nayo kwani hakuna guarantee kwamba wabunge wenye shahada ndio wanaofanya vizuri zaidi.

Let's not dumb down swala zima la elimu.

Kinachotakiwa ni kuongoza awareness na elimu kwa jamii yote, kwa sababu kama mkuu alivyosema hapo juu, kuna ma profesa wamekuwa disappointed kwa sababu hawasikilizwi na seriklai.

Sasa kama tuna an educated populace, hapo ndo sehemu ya lobbyists na pressure groups kuipa pressure serikali.
 
Intelligence inapimwa kwa matendo na kauli zetu; Ebu tujaribu kuwa more practical on this matter. Kwa mfano mdogo tu, Signature ya narubongo inatamka kwamba:

"Chadema kinatumia alama ya vidole viwili kama manati, manati kamwe haiwezi kuua tembo" Livingstone Lusinde (2012).

How intelligent is this statement by MBUNGE Lusinde? And je, is Narubongo using it sarcastically au he finds it ‘appealing/draws favourable attention'? Nina uhakika ameiweka out of sarcasm.

Ok, quote nyingine from Mzee Mwanakijiji (signature yake humu) inasema hivi:

Binafsi NAKERWA, NAKASIRISHWA, NA KUCHUKIZWA sana na haya mambo kwamba eti "ameshauriwa vibaya na wasaidizi wake!" Huwa mara zote najiuliza ikiwa anashauriwa vibaya ni kwanini basi kila wakati awe anachukua huo ushauri mbaya!! - NasDaz

I think this quote (by NasDaz) is one of the most intelligent quotes in recent period katika jamii yetu ya watanzania.
 
Until then tuwaache watu waliopata elimu ya lazima ya msingi wagombee. Iwapo wabunge wenye shahada watafanya vizuri sana kwenye Bunge na wasiokuwa na shahada watafunikwa katika michango na shughuli zao bungeni, nadhani kunaweza kutokea natural selection of a sort, ambapo wananchi wenyewe wakaanza kuchagua wenye shahada.

Lakini bado hapo hakutakuwa na mwananchi aliyenyimwa fursa ya kugombea nafasi ya uongozi.

Hivi hapa suala la msingi ni kutoa fursa kwa wananchi kuongoza au kuwapatia wananchi fursa ya kujipatia kiongozi bora wa kuweza kutatua matatizo yao? Hoja yako inaendana zaidi na dhana ya Bora Kiongozi kuliko Kiongozi Bora; either way can be okay depending unajengea vipi hoja;
 
Very good observation.

Ukiwa na kigezo cha ubunge ambacho hakipo accessible kwa wananchi wote, kimsingi unasema kwamba haki ya uongozi unaitoa kwa sehemu kubwa ya wananchi.

Matokeo yake walioongoza na familia zao ndio watakuwa wanaongoza wao kila siku huku wengine ambao hawana uwezo wa kupata hiyo degree ndio watakuwa wa kuongozwa daima.

Sif za uongozi zimewekwa simple kwa sababu maalum. Sababu yenyewe ni kwamba ultimately wananchi wenyewe ndio waachiwe kuchagua.

Hili ndilo lililonifanya ni hoji uteuzi wa wabunge wa viti maalum wa Chadema. Kuwa kila ukiwa na elimu ya juu zaidi ndio unapata fursa zaidi ya kuteuliwa kuwa Mbunge [Kwa mujibu wa model ya Kitila]. Hii sio tu kuwa inapingana na dhana nzima ya viti maalum (kuwa wapewe wanawake wasiokuwa na fursa) bali pia inapingana na nadharia nyuma ya sera ya chama kuwa "kikiingia madarakani kitahakikisha kunakuwa na fursa sawa ya elimu kwa wote"

Katika nchi ambayo hakuna fursa sawa ya elimu kwa wote, kuchagua kiongozi kwa elimu ni kum-adhibu mwananchi ambae mfumo ulimbagua kumpa elimu.
 
Nimekuja kuelewa katika vitu ambavyo vinawatenganisha Watanzania ni elimu. Mtu akipost thread kuhusu ELIMU anakumbana na mawazo kinzani. Lakini ukweli unabaki pale pale kwamba ELIMU tena ya UKWELI kwa ustawi wa taifa letu. Ndiyo maana unakuta watu wabunge wetu kwenye bunge la Afrika ya Mashariki toka tanzania wana waachia uwanja wenzao toka Kenya, Uganda na Rwanda. Hawajui lugha na hoja hakuna...kisa tunatanguliza c=CHAMA fulani kuliko weledi...Njia ya mwongo ni fupi...Tubadilike

Mkuu elimu bhana huwezi ukaipuuza, mbaya zaidi tupo kwenye nchi ambayo imejaa watu kutumiwa kwa matakwa ya wachache. hii ndo imewafanya wabunge wengi hasa wa ccm wenye elimu ndogo kushindwa kutumia utashi wao wa ufahamu wa mambo katika kutimiza jukumu lao la kuisimamia serikali, na badala yake wamekuwa wafuata upepo na kujineemesha kwa miposho mikubwa kuliko hata majukumu yao. Hebu tujiulize, kwa nini hali imekuwa tofauti sana bungeni baada ya wabunge wa upinzani kuongezeka hasa hawa wa chadema??? hapo utagundua kwamba, hata ile busara anayokuwa nayo mtu, lazima ipewe nafasi ya kuchangia kwa hoja pasipo kuhofia kuitwa kwenye cocus ya chama na kutishiwa kuwajibishwa. ndio maana hata wabunge wa CDM wenye kiwango kidogo cha elimu wanafanya vizuri sana kuisimamia serikali kuliko hao wenye ma-degree waliopo CCM.
 
Hivi hapa suala la msingi ni kutoa fursa kwa wananchi kuongoza au kuwapatia wananchi fursa ya kujipatia kiongozi bora wa kuweza kutatua matatizo yao? Hoja yako inaendana zaidi na dhana ya Bora Kiongozi kuliko Kiongozi Bora; either way can be okay depending unajengea vipi hoja;

Suala la msingi la kikatiba ni kutoa fursa sawa kwa kila mwananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote. Iwe kwenye kuongoza au kuongozwa.

Unapoweka vigezo vya elimu ya shahada kwa mfano, ni sawa na wewe kusema hata mtu awe na uwezo kiasi gani na awe amepeleka maendeleo kiasi gani kwa wananchi wake, madamu hajarasimishwa kwa kutumia elimu ya Mzungu, basi huyo hafai.

Hii inapingana na hata kanuni za msingi za utaratibu wa utawala kwenye jamii za Kiafrika.
 
Marekani huhitaji kuwa na shahada ya sheria ili uwe jaji wa mahakama kuu (Supreme Court). Na hata kwenye jurisdiction zingine (huko huko Marekani) huwa hakuna educational au bar passage requirements.
 
Historia inatueleza kwamba mwaka 1961 kulikuwa na only a handful of University graduates - hawakuwa wanafika kumi kati ya jumla ya watanzania milioni tisa (1961). Hivi, out of curiosity tu, Je Mwalimu asingekuwa na elimu aliyokuwa nayo na badala yake angekuwa na upeo sawa na the rest of the population au angetokea mtu mwingine mwenye upeo sawa na the majority in the population, leo Tanzania ingekuwa wapi? Nadhani mazingira ya uongozi yanahitaji elimu, hasa katika mazingira ya dunia ya sasa ambayo yanazidi kuwa complex na yanayohitaji umakini na uwezo wa hali ya juu kuyatatua; Uwepo wa viongozi wenye elimu ambao wanashindwa ku 'deliver' isiwe ndio hoja ya msingi ya kusema tuwajaribu hata wasio na elimu; huku ni kujidanganya na tutazidi kudidimia; suala muhimu ni kuhimiza fursa za elimu zipanuliwe zaidi, huku jamii ikiwekeza katika viongozi wasomi, lakini muhimu zaidi, kuwe na mechanism ya ku monitor 'performance' ya viongozi hawa;
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom