jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Nyani Ngabu said:Usafi wa kinywa Watu wengi umetupitia kushoto. Ni wachache sana kati yetu tunaokwangua ndimi zetu mara mbili kwa siku. Ni wangapi tunajua hata kama kuna tongue scrapers zilizo mahsusi kwa kazi hiyo tu?
Tongue scrapers ni muhimu sana katika kupigana na bad breath. Wale anaerobic bacteria wanaosababisha mdomo kunuka hujizalia sana kwenye ndimi hasa kwa sehemu ya nyuma kule karibu na koromeo. Sehemu ingine ambao hao bacteria wanapenda kujihifahi ni kwenye paa la kinywa (palate). Huko nako mtu unapaswa kupitisha mswaki.
Flossing. Idadi kubwa kati yetu hawajui flossing ni nini. Flossing husaidia sana katika kuondoa mabaki ya chakula yaliyonasa katikati ya meno. Sasa fikiria mtu anakula mchemsho, viepe, kitimoto, na vinginevyo halafu hakuna cha kufloss wala nini. Badala yake anatumia kijiti. Yale mabaki ya chakula yakikaa sana katikati ya meno huwa yanatoa harufu.
Na vile vijiti huwa havifikii sehemu nyingi tu za meno na hata huko zinakofika huwa havifanyi kazi sawa na nyuzi za flossing. Mtu ambaye hajawahi kufloss humu ndani na ajaribu siku moja aone jinsi ambavyo flossing ilivyo effective.
Mouthwash. Ni wachache sana tunaotumia mouthwash. Hizi nazo husaidia sana katika kuua harufu mbaya. Mtu ukishamaliza kuukwangua ulimi wako, ukishamaliza kufloss, ukishamaliza kusugua meno yako pamoja na paa la kinywa na fizi unasukutua na mouthwash kabla ya kusukutua na maji. Mtu ukizingatia na kufanya huo mchakato utakuwa umelipunguza tatizo la harufu mbaya kwa kiasi kikubwa sana.
Mwisho watu wengi hawajui kuwa kikubwa kisababishacho harufu mbaya mdomoni ni anaerobic bacteria. Hawa ni bacteria ambao hushamiri pasipo na oxygen ya kutosha. Sasa mdomo mara nyingi huwa unafungwa na hivyo kupelekea hao bacteria kujizalia na kushamiri.
Kwa hiyo hapo la msingi, baada ya kuzingatia yote hayo yahusuyo usafishaji ni muhimu pia kuuweka mdomo kuwa oxygenated mara kwa mara. Na hili linawezekana kwa kunywa maji throughout the day. Sisemi unywe maji kama ng'ombe. Just space out your water intake without long intervals in between and you'll be straight for the most part.
Hayo yote ukiongezea na routine teeth cleaning performed by a qualified dentist should do it in getting rid of bad breath.
What's wrong with that?
Flossing is highly effective in keeping your teeth clean and healthy by getting rid of food debris that gets stuck between your teeth especially in those hard to reach areas of your mouth/teeth.
Unasema ukweli lakini umezungumza lugha ambayo ni nje kabisa ya mtanzania wa kawaida,ama watanzania walio wengi.Nyani Ngabu said:Jaribu kwenda kwenye maduka makubwa makubwa ya dawa baridi uwaulizie. Kwenye haya maduka yetu mengine ya akina Mangi sidhani kama unaweza kuzipata hizo dental floss.
Uko very out of touch,ushauri wako ni mzuri lakini you really have forgotten where you come from.
Kwa wengi wa watanzania,yote uliyoyasema ni kama anasa kwao...
Sikubaliani na analysis yako moja kwa moja....
Maelezo uliyoyatoa hata hivyo hayata resonate na wabongo wengi...