3 Bedroom House, toa changamoto!

3 Bedroom House, toa changamoto!

Ondoa ukuta wote ndani ya living room, ondoa ukuta unaogawa living room na kitchen badala yake weka wooden frame tuili iwe open dinning and kitchen its more fashionable and less expensive .ondoa mlango kwenye kolido its not needed.
Oops, ukuta wote wa living room? I thought open kitchen ni sawa, yaani dining na kitchen iwe one big hall kuwe na design fulani hivi ya makabati...
Screenshot_2022-05-30_120431.jpg
 
Hapana Ndugu nilimtuma pesa akasimamie ujenzi akaja na kitu kama hicho. Na kimesimama kweli kweli. Yaani ilivyoelezwa hapo kama vile unaiona nyumba yangu.
Safi sana mkuu, nyumba ikijengwa vizuri kwa standard zake unaipenda. Bahati mbaya wengi wanayaona makosa baada ya kuzama ndani.
 
Safi sana mkuu, nyumba ikijengwa vizuri kwa standard zake unaipenda. Bahati mbaya wengi wanayaona makosa baada ya kuzama ndani.
Nilikuwa makini sana. Na namwamini alifanya ninavyotaka.
 
Hivi kuna shida vyumba vyote kua master? Nilikua nafanya kazi ya kutengeneza domes kwa mhindi fulani nikakuta nyumba ya vyumba vinne vyote ni master. Vina closet, ukubwa sawa na bafu na choo. Kisha kuna bafu na choo kwa ambaye atakua sebuleni.

Sijakutana na nyumba nyingine ya hivyo. Kuna shida kifundi?
SAHII kabisa,
mambo ya kunyer nje yamepitwa na wakati.
Choo master inakua na privacy zaidi
 
Kuna mwamba alitisha zaidi kajenga nyumba ya vyumba vitatu vyote master ila haina corridor ila milango yote ya vumba iko sebuleni.
Hahaha, zile setup za zamani. Milango yote inaanzia sitting room. Amezingua sana!
 
Superb, sema kona ndani ya nyumba hua zinatengeneza dead spaces, yaan huwezi kuweka hata ndoo ya maji
 
Tumezoea kuona nyumba zikiwa na milango miwili tu wa sebuleni na jikoni.

Hii ya stoo kuwa na mlango kwenye "veranda" ni mpya.
 
Tumezoea kuona nyumba zikiwa na milango miwili tu wa sebuleni na jikoni.

Hii ya stoo kuwa na mlango kwenye "veranda" ni mpya.
Ndio maana ya design mkuu, wapo ambao hadi master bedroom inakuwa na exit door yake. Yani ni vile wewe na taste yako tu.
 
Darasa tosha for designer, Pongezi sana kwa wote mliotoa maoni yenu makini zaidi👏👏 Binafsi nimejifunza kitu, Ama JF ni kisima cha maarifa..
 
Viwanja vingi vya mjini Ni 20/15.
Kuna sehemu aliweka kipimo Cha chumba kimoja kua ni 3.5mita, almost futi 12.

Ukingalia
mapana yake anajumla vyumba Kama vinne, ambapo jumla Ni futi 48. Almost mita16 mapana.

Ukiacha mita 1 ya ujirani mwema kila upande, jumla ni mita 18. Na hapo bado hajaacha mita 2 kila upande za kujengea fensi

NB: hapa Imezingatiwa hajapakana na barabara yoyote Ile pembeni anapotakiwa kuacha mita 3 barabara ya TARURA au mita 5 za barabara za tanroad.

NB: kwa nyumba Hii ili kujenga fensi pembeni Lazima awe na mapana ya kuanzia mita 22 nakuendelea.

Ukienda kwa marefu,
Makadirio ni marefu ya vyumba vitatu vya futi 12 kila kimoja, ambapo jumla Ni futi 36.ambayo ni sawa na mita 12.

Ukiacha mita 1 ya ujirani mwema kila upande, jumla mita 14. Na hapo bado hajaacha mita 2 kila upande ili kujenga fensi. Ambapo Itakua jumla mita 18.

NB:
1. hapa Imezingatiwa hajapakana na barabara yoyote Ile pembeni anapotakiwa kuacha mita 3 barabara ya TARURA au mita 5 za barabara za tanroad.

2. kwa nyumba Hii ili kujenga fensi mbele na nyuma, Lazima awe na marefu ya kuanzia mita 18 nakuendelea.


Hitimisho,
Kwa kujibana bana Sana,
Unaona kabisa anahitaji kiwanja Cha mapana 22 na marefu 18,
Na hapo imezingatiwa Yuko landlocked, hajapakana na barabara yoyote Ile.

Ili nyumba hii ikae vizur,
Tena iwe na barabara ya kuingilia gari mpaka nyumbani na Apate parking na sehemu angalau ya kufua,kuanika nguo, watoto kucheza.

Ni Lazima marefu yaongezeke kufikia angalau mita 30 na mapana yawe mita 25.

Na hiki kwa mjini,
Kukipata sio kiwanja kidogo Wala Cha pesa ndogo mkuu.
You are a good teacher
 
Darasa tosha for designer, Pongezi sana kwa wote mliotoa maoni yenu makini zaidi👏👏 Binafsi nimejifunza kitu, Ama JF ni kisima cha maarifa..
Nzuri sana kama you're planning to start building your own house. Muhimu sana kuzingatia mambo ya msingi kabla hujaanza kuweka tofali.
 
Ina kona nyingi kama inavyoonekana, hivyo hata kama ni kubwa bado kwa hizi kona zake nafasi ipo. Kiwanja cha 20x20 nyumba inakaa vizuri kabisa na space ya kutosha nje. Kwenye 20x20 ukijenga nyumba yenye 150m² hadi 180m² sio mbaya... unakuwa na 220m² free space, nafasi kubwa tu.

Hapo matofali kiasi gani?
 
Back
Top Bottom