3 Bedroom House, toa changamoto!

3 Bedroom House, toa changamoto!

Ina kona nyingi kama inavyoonekana, hivyo hata kama ni kubwa bado kwa hizi kona zake nafasi ipo. Kiwanja cha 20x20 nyumba inakaa vizuri kabisa na space ya kutosha nje. Kwenye 20x20 ukijenga nyumba yenye 150m² hadi 180m² sio mbaya... unakuwa na 220m² free space, nafasi kubwa tu.
Mkuu,
Kiwanja cha 20 kwa 20 kwa vipimo vya vyumba vyako vya futi 12 haikai Hii nyumba mkuu.

Vinginevyo labda ufanye modification za mapana na marefu ya nyumba yako mkuu.

Ndo maana nikisisitiza uweke vipimo clear kabisa ili tukushauri vizur.
 
Kingine,
Unapaswa kujua kua Hizo square mita 150,
Ni jumla ya eneo lote la nyumba nzima marefu na mapana yake.

Bila kuzingatia Kuna vi-portion vimezidi au vimepelea kwenye mapana na marefu ya nyumba.

Hii nyumba,
Ukiijenga Bila vipimo, Unaweza jikuta choo Kiko kwa jirani, au umebana Sana Kia's bati lako linamwaga maji kwa jirani yako.

Kama ni mtata,
Mtajikuta mnaanza migogoro ya mipaka, au unalazimika upasuke ununue kipande kilichobaki kwake. Ambapo Lazima akunyooshe kwenye Bei, lasivyo bomoa.

Kitu Ambacho sio kizur na kinatoa hasara na ukijaribu kubomoa unajikuta unaharibu ramani.
 
Kama ni Dar, angalau room iwe na madirisha mawili na kuendelea kutokana na joto na diririsha liwe na 3m na kendelea, chumba cha kulala master bedroom kiwe na 4x3m na kuendelea kusudi ya hewa na kabati la nguo,
Master bedroom ianzie 4x4m iwe na sehem mtu anaweza kukaa kama akija mgeni kumsalimia mama aliejifungua, sehem ndogo ya viti viwili
Jiko liwe kubwa ndio sehem ya mwanamke kujidai, nadhani store haina umuhimu sana maana makabati ya jikoni ni store tosha,
Sebule ambayo ndio uwanja wa mwanaume uwe mkubwa angalau 5x4.

Bedroom za watoto ni wastani wa 4x3.5m², naamini ni spacious kabisa maana hapo utajengea kabati na nafasi ya kutosha.
Master bedroom iwe angalau 4x5m².

Kuna scenario mbili hapa kwa mtu anayejenga;
*Kuna wanaopenda sitting room kubwa coz wanatumia mda wao mwingi huko.
*Kuna wanaopenda master bedroom kubwa coz wanapenda kutumia mda mwingi chumbani
Sitting room ya 30m² naamini kibongobongo ni kubwa tu.

Asante kwa observation yako mkuu.
 
Mkuu,
Kiwanja cha 20 kwa 20 kwa vipimo vya vyumba vyako vya futi 12 haikai Hii nyumba mkuu.

Vinginevyo labda ufanye modification za mapana na marefu ya nyumba yako mkuu.

Ndo maana nikisisitiza uweke vipimo clear kabisa ili tukushauri vizur.
Hii ina 14m×15m, kwa nini isikae kwenye kiwanja cha 20x20 mkuu?
Ninaposema 20x20 namaanisha mita, sio miguu.
 
Kama ni Dar, angalau room iwe na madirisha mawili na kuendelea kutokana na joto na diririsha liwe na 3m na kendelea, chumba cha kulala master bedroom kiwe na 4x3m na kuendelea kusudi ya hewa na kabati la nguo,
Master bedroom ianzie 4x4m iwe na sehem mtu anaweza kukaa kama akija mgeni kumsalimia mama aliejifungua, sehem ndogo ya viti viwili
Jiko liwe kubwa ndio sehem ya mwanamke kujidai, nadhani store haina umuhimu sana maana makabati ya jikoni ni store tosha,
Sebule ambayo ndio uwanja wa mwanaume uwe mkubwa angalau 5x4.
Mkuu acha masihara Basi,
Dirisha la mita 3 si sawa na futi 9 hizo.

Dirisha la futi 9,
Si karibu linameza ukuta mzima wa chumba Cha futi 12?
 
Hii ina 14m×15m, kwa nini isikae kwenye kiwanja cha 20x20 mkuu?
Ninaposema 20x20 namaanisha mita, sio miguu.
Hebu weka vipimo twende sawa mkuu,
Hii nyumba kwenye 20×20 inakaa Ila kwa tabu Sana.
 
Choo cha public mbona wageni watakuwa wanachungulia vyumbani?
Chungulia tena mzee mwenzangu, najua macho kidogo yanaleta ukungu

Public toilet haiingiliani na choo cha watoto.
 
Kuna watu wanapenda nyumba zenye nafasi mkuu, nyumba ikikosa korido kwangu binafsi inaboa sana. Korido inakula nafasi lakini inafanya nyumba ipendeze.
Upo sahihi, Ila zisiwe zina long distance, kwa mtazamo wangu lakini
 
Hivi kuna shida vyumba vyote kua master? Nilikua nafanya kazi ya kutengeneza domes kwa mhindi fulani nikakuta nyumba ya vyumba vinne vyote ni master. Vina closet, ukubwa sawa na bafu na choo. Kisha kuna bafu na choo kwa ambaye atakua sebuleni.

Sijakutana na nyumba nyingine ya hivyo. Kuna shida kifundi?
 
Back
Top Bottom