3 Bedroom House, toa changamoto!

ERoni

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
43,613
89,977
Kabla haijawekwa kwa AutoCad, toa changamoto yako hapa, nini kimekosewa, nini kipo sawa...wapi parekebishwe..

20220527_141331.jpg
 
Nimeanza kucheka kwanza....kuna mtu atasema 'chumba cha watoto wa kiume na kike visipakane na chumba chako kisitazamane na vyumba vya watoto' nawaza kwa sauti tu!
Hoja nzuri mkuu, hapo inabidi mchoraji alifikirie hilo. Vyumba vya watoto visiwe karibu, ila nahisi kajaribu kutofanya milango ya vyumba kutizamana..
 
Vipimo ujaweka kote,
Kwa haraka haraka
Hii nyumba Ni kubwa mno, Kama una kiwanja Cha kidogo Unaweza kosa Hata parking.

Hiyo sitting room Ni kubwa balaa
Yes, vipimo vimefichwa ila iko na vipimo vyake kabisa. Kama mtu anataka nyumba yenye space ya kutosha, mf. mtu anakuambia anataka sebule kubwa(kuanzia 30m²/ 5x6) au zaidi, master bedroom kubwa(20m² / 4x5 au zaidi).

Challenge ya bugdha kwa wanaoenda public toilet kupitia mlango wa master naikubali, japo hapo ukiangalia ni watoto tu, guests wanaokuja na kusepa wana washroom yao.

Otherwise challenge accepted mkuu!
 
Simple plan ni nyumba yenye wing 3. Wing moja inabeba master bedroom pekee yake, wing moja vyumba vya watoto na family bathroom na wingi ingine jiko,sebule na dining room.
 
Hilo nmekuja kuliona baadae,
Hongera Sana, Hii idea ya washroom ya wapitaji nmeipenda
 
Sasa vipimo hakuna umejuaje itakuwa kubwa kiasi cha kukosa parking? Kiwanja chake amesema size?
Ina kona nyingi kama inavyoonekana, hivyo hata kama ni kubwa bado kwa hizi kona zake nafasi ipo. Kiwanja cha 20x20 nyumba inakaa vizuri kabisa na space ya kutosha nje. Kwenye 20x20 ukijenga nyumba yenye 150m² hadi 180m² sio mbaya... unakuwa na 220m² free space, nafasi kubwa tu.
 
Ukiweka vipimo vyote tutapata picha kamili.
 
Simple plan ni nyumba yenye wing 3. Wing moja inabeba master bedroom pekee yake, wing moja vyumba vya watoto na family bathroom na wingi ingine jiko,sebule na dining room.
Uko sahihi 100% mkuu, siku hizi naona watu hawapendi corridors sana ili kupunguza ukubwa wa nyumba. Mimi naona corridors ni muhimu, yaani nyumba ikikosa corridors naona haina space. Ushawahi kuiobserve hii kitu?
 
Kama ni Dar, angalau room iwe na madirisha mawili na kuendelea kutokana na joto na diririsha liwe na 3m na kendelea, chumba cha kulala master bedroom kiwe na 4x3m na kuendelea kusudi ya hewa na kabati la nguo,
Master bedroom ianzie 4x4m iwe na sehem mtu anaweza kukaa kama akija mgeni kumsalimia mama aliejifungua, sehem ndogo ya viti viwili
Jiko liwe kubwa ndio sehem ya mwanamke kujidai, nadhani store haina umuhimu sana maana makabati ya jikoni ni store tosha,
Sebule ambayo ndio uwanja wa mwanaume uwe mkubwa angalau 5x4.
 
Sasa vipimo hakuna umejuaje itakuwa kubwa kiasi cha kukosa parking? Kiwanja chake amesema size?
Viwanja vingi vya mjini Ni 20/15.
Kuna sehemu aliweka kipimo Cha chumba kimoja kua ni 3.5mita, almost futi 12.

Ukingalia
mapana yake anajumla vyumba Kama vinne, ambapo jumla Ni futi 48. Almost mita16 mapana.

Ukiacha mita 1 ya ujirani mwema kila upande, jumla ni mita 18. Na hapo bado hajaacha mita 2 kila upande za kujengea fensi

NB: hapa Imezingatiwa hajapakana na barabara yoyote Ile pembeni anapotakiwa kuacha mita 3 barabara ya TARURA au mita 5 za barabara za tanroad.

NB: kwa nyumba Hii ili kujenga fensi pembeni Lazima awe na mapana ya kuanzia mita 22 nakuendelea.

Ukienda kwa marefu,
Makadirio ni marefu ya vyumba vitatu vya futi 12 kila kimoja, ambapo jumla Ni futi 36.ambayo ni sawa na mita 12.

Ukiacha mita 1 ya ujirani mwema kila upande, jumla mita 14. Na hapo bado hajaacha mita 2 kila upande ili kujenga fensi. Ambapo Itakua jumla mita 18.

NB:
1. hapa Imezingatiwa hajapakana na barabara yoyote Ile pembeni anapotakiwa kuacha mita 3 barabara ya TARURA au mita 5 za barabara za tanroad.

2. kwa nyumba Hii ili kujenga fensi mbele na nyuma, Lazima awe na marefu ya kuanzia mita 18 nakuendelea.

Hitimisho,
Kwa kujibana bana Sana,
Unaona kabisa anahitaji kiwanja Cha mapana 22 na marefu 18,
Na hapo imezingatiwa Yuko landlocked, hajapakana na barabara yoyote Ile.

Ili nyumba hii ikae vizur,
Tena iwe na barabara ya kuingilia gari mpaka nyumbani na Apate parking na sehemu angalau ya kufua,kuanika nguo, watoto kucheza.

Ni Lazima marefu yaongezeke kufikia angalau mita 30 na mapana yawe mita 25.

Na hiki kwa mjini,
Kukipata sio kiwanja kidogo Wala Cha pesa ndogo mkuu.
 
Back
Top Bottom