Bome-e
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 17,104
- 26,070
Kwa hali ilivyo sasa inabidi Kigoma ipate Rais 2025 walau na huku tukumbukwe.
Maana bila Rais kutokea huku, maendeleo yataendelea kusuasua. Imechukua zaidi ya miaka 10 kwa kipande cha Nyakanazi kuunganishwa na Kakonko, bado Kakonko-Kibondo-Kasulu ili Kahama iwe imeunganishwa na kigoma.
Maji ya uhakika bado ni changamoto. Watu wa Kagera, Rukwa na Kigoma tumeambiwa tutatumia hospitali ya rufaa Chato umbali ukiwa ni mamia ya kilomita.
Sasa nadhani 2025 ni zamu yetu watu wa kigoma kutoa Rais ili na sisi tupae kwa kasi. Kigoma iliahidiwa kuwa Dubai kabla hata ya kusemwa Chato kuwa jiji kama Wuhan.
Watu wa kusini inabidi tuingie makubaliano, mtuunge mkono 2025 na sisi tutawaunga mkono 2035. Bila hivyo tutaendelea kuyasikia kwenye Bomba hayo maendeleo ya kweli.