2025 ni zamu ya Kigoma, tumecheleweshwa mno

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
17,065
26,044
Kwa hali ilivyo sasa inabidi Kigoma ipate Rais 2025 walau na huku tukumbukwe.

Maana bila Rais kutokea huku, maendeleo yataendelea kusuasua. Imechukua zaidi ya miaka 10 kwa kipande cha Nyakanazi kuunganishwa na Kakonko, bado Kakonko-Kibondo-Kasulu ili Kahama iwe imeunganishwa na kigoma.

Maji ya uhakika bado ni changamoto. Watu wa Kagera, Rukwa na Kigoma tumeambiwa tutatumia hospitali ya rufaa Chato umbali ukiwa ni mamia ya kilomita.

Sasa nadhani 2025 ni zamu yetu watu wa kigoma kutoa Rais ili na sisi tupae kwa kasi. Kigoma iliahidiwa kuwa Dubai kabla hata ya kusemwa Chato kuwa jiji kama Wuhan.

Watu wa kusini inabidi tuingie makubaliano, mtuunge mkono 2025 na sisi tutawaunga mkono 2035. Bila hivyo tutaendelea kuyasikia kwenye Bomba hayo maendeleo ya kweli.
 
Mchawi wenu huyu hapa....kilia msimu wa uchaguzi lazima apeleke mtu sokoni kwa vipande ishirini vya fedha!
download.jpg
 
Mchawi wenu huyu hapa....kilia msimu wa uchaguzi lazima apeleke mtu sokoni kwa vipande ishirini vya fedha!
View attachment 1676194
Jimbo lake ni dogo sana katika mkoa mzima wa Kigoma!

Nways kwa sasa sio mbunge,vp hayo maendeleo yapo? Vipi majimbo mengine ambayo yalikuwa CCM mbona hali ni ileile?
Naunga mkono hoja kuwa Rais 2025 ni zamu ya Muha wa Kigoma kuongoza nchi!
 
Kama waha bado mna fikira kwamba dereva wa treni anaweza kuwa ni chuma, hivi mnaweza kutoa potential candidate kwenye nafasi ya urais. Anzeni kupunguza ushamba na ubishi usio na maana..
 
Naunga mkono hoja! Lakini siyo lazima Rais atoke mkoa wa Kigoma ndiyo maendeleo yaje! Kilimanjaro anagalau watu wake wana maendeleo lakini tangu nchi ipate uhuru haijawahi kutoa Rais hata mmoja.
Ila tumeona mfano kwa Chato wa namna rahisi zaidi ya kupata maendeleo!
 
Kama waha bado mna fikira kwamba dereva wa treni anaweza kuwa ni chuma, hivi mnaweza kutoa potential candidate kwenye nafasi ya urais. Anzeni kupunguza ushamba na ubishi usio na maana..
Acha dharau kijana,kigoma tuna wasomi wengi wenye sifa za kuongoza nchi!
2025 Rais anatoka Kigoma!
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom