2020 GEORGIA BANK ROBBERY: Mtu mmoja (inasemekana ni mwanajeshi muasi) anawezaje kuwachukua mateka watu zaidi ya 40 kwa wakati mmoja bila kizingiti?

Kuna mtekaji ndege mmoja alichukua pesa ndefu sana na akachomoka miaka hiyo hawajamuona mpaka leo,aliteka ndege akalazimisha itue mahali aletewe mpunga otherwise analipua akaletewa mpunga akaamrisha ndege iondoke ilipokua katikati huko msituni kalazimisha pilot afungue nyuma kule kuna ndege zilikua nauwezo kufunguka kule nyuma hata ikiwa inatembea bila madhara yoyote.jamaa alitoka na parachute akapotea huku nyuma kulikua na ndege mbili za wanajeshi zinaifuatilia ile ndege ya mtekaji.ilipotua wanafanikiwa kuwatoa abiria aah wapi mtekaji kashayeya na madola yote waliyompa.jamaa walimtafuta miaka nane mpaka wakakata tamaa wakasema kafa.issue ikabumbuluka kuna dogo aliokota dola mtoni huko na alipokwenda kuchange au kutumia ndio ikajulikana ni kati ya zileee zilizopigwa na mtekaji,msako ukaanza upya.badae wakakata tamaa tena
Jamaa usikute yuko zake thailand huko vijijini analima tu mpunga wake huku ana hazina yake saaafi kaitunza tu.
 
Kuna mtekaji ndege mmoja alichukua pesa ndefu sana na akachomoka miaka hiyo hawajamuona mpaka leo,aliteka ndege akalazimisha itue mahali aletewe mpunga otherwise analipua akaletewa mpunga akaamrisha ndege iondoke ilipokua katikati huko msituni kalazimisha pilot afungue nyuma kule kuna ndege zilikua nauwezo kufunguka kule nyuma hata ikiwa inatembea bila madhara yoyote.jamaa alitoka na parachute akapotea huku nyuma kulikua na ndege mbili za wanajeshi zinaifuatilia ile ndege ya mtekaji.
Daaah...
 
Tafuta hiyo story mkuu ni nzuri sana ,sikumbuki niliisoma wapi ningekuwekea link ukafaidi
Zile dola zote jamaa walizipiga mark ndo wakamplekea ili akitumia tu mahali au yoyote wamkamate kwa ushahidi.ndio akaja nayo huyo dogo
 
ilipotua wanafanikiwa kuwatoa abiria aah wapi mtekaji kashayeya na madola yote waliyompa.jamaa walimtafuta miaka nane mpaka wakakata tamaa wakasema kafa.issue ikabumbuluka kuna dogo aliokota dola mtoni huko na alipokwenda kuchange au kutumia ndio ikajulikana ni kati ya zileee zilizopigwa na mtekaji,msako ukaanza upya.badae wakakata tamaa tena
Jamaa usikute yuko zake thailand huko vijijini analima tu mpunga wake huku ana hazina yake saaafi kaitunza tu.
Huu ni zaidi ya ushetani hakika
 
Aya ya mwisho uliyoibold ndio inafanya watu wakuone kimeo hata ule uzi wa kula rambirambi walikudis kwasababu una hulka zote zinazofanana na mla rambirambi wa taifa.
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Eti ndugu zangu watanzania;

Mtu mmoja (inasemekana ni mwanajeshi muasi) anawezaje kuwachukua mateka watu zaidi ya 40 kwa wakati mmoja bila kizingiti?

View attachment 1618831

Polisi katika jamhuri ya zamani ya Soviet ya Georgia walikuwa wakimtafuta jambazi wa benki ambaye alishikilia watu zaidi ya 40 mateka kwa masaa kabla ya kuwaachilia na kutoroka na pesa alizopewa.

Mtu mwenye silaha aliwachukua mateka wafanyikazi wa benki na wateja katika mji wa Zugdidi magharibi mwa Georgia Jumatano, akidai pesa taslimu $ 500,000. Baada ya wahusika kumpatia kiasi hicho cha pesa na gari ambalo alitaka, jambazi huyo aliwaachilia mateka walio wengi na kuondoka na mateka watatu waliobaki.

Mtu huyo aliwaachilia usiku wa manane katika eneo lenye misitu na kisha kutoweka. Akiongea wakati wa mkutano wa serikali, waziri mkuu wa Georgia, Giorgi Gakharia, aliwasihi polisi wamfuatilie haraka mwanajeshi huyo, na kuongeza kuwa "lazima kusiwe na dhana kwamba uhalifu unaweza kufanyika pasipo kuadhibiwa."

View attachment 1618816

Waziri wa Mambo ya Ndani bwana Vakhtang Gomelauri aliwaambia waandishi wa habari kuwa madai ya jambazi yule yalitekelezwa kwa sababu "kwa serikali yetu na kwangu mimi, maisha ya watu ni muhimu zaidi kuliko pesa." Alisema kuwa haikufahamika mara moja ikiwa mshambuliaji alikuwa na msaidizi kati ya mateka wale.

ANGALIZO: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania yangu.

Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu. Hakika umasikini ni m-baya sana.


NDUGU YANGU USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Back
Top Bottom