2020 GEORGIA BANK ROBBERY: Mtu mmoja (inasemekana ni mwanajeshi muasi) anawezaje kuwachukua mateka watu zaidi ya 40 kwa wakati mmoja bila kizingiti?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Eti ndugu zangu watanzania;

Mtu mmoja (inasemekana ni mwanajeshi muasi) anawezaje kuwachukua mateka watu zaidi ya 40 kwa wakati mmoja bila kizingiti?

lLKNnToK42c-700x394.jpg


Polisi katika jamhuri ya zamani ya Soviet ya Georgia walikuwa wakimtafuta jambazi wa benki ambaye alishikilia watu zaidi ya 40 mateka kwa masaa kabla ya kuwaachilia na kutoroka na pesa alizopewa.

Mtu mwenye silaha aliwachukua mateka wafanyikazi wa benki na wateja katika mji wa Zugdidi magharibi mwa Georgia Jumatano, akidai pesa taslimu $ 500,000. Baada ya wahusika kumpatia kiasi hicho cha pesa na gari ambalo alitaka, jambazi huyo aliwaachilia mateka walio wengi na kuondoka na mateka watatu waliobaki.

Mtu huyo aliwaachilia usiku wa manane katika eneo lenye misitu na kisha kutoweka. Akiongea wakati wa mkutano wa serikali, waziri mkuu wa Georgia, Giorgi Gakharia, aliwasihi polisi wamfuatilie haraka mwanajeshi huyo, na kuongeza kuwa "lazima kusiwe na dhana kwamba uhalifu unaweza kufanyika pasipo kuadhibiwa."

66995.jpg


Waziri wa Mambo ya Ndani bwana Vakhtang Gomelauri aliwaambia waandishi wa habari kuwa madai ya jambazi yule yalitekelezwa kwa sababu "kwa serikali yetu na kwangu mimi, maisha ya watu ni muhimu zaidi kuliko pesa." Alisema kuwa haikufahamika mara moja ikiwa mshambuliaji alikuwa na msaidizi kati ya mateka wale.

ANGALIZO: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania yangu.

Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu. Hakika umasikini ni m-baya sana.


NDUGU YANGU USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Back
Top Bottom