Naam Mkuu
platozoom, kama Watanzania ndio wangekuwa wanapiga kura ni wazi ushindi ungekuwa wa Trump. Lakini kwa kuwa Wamarekani ndio wanapiga kura, wakurupukaji kama Trump, Ikulu waisikie tu. Vyombo vilivyomjenga ndivyo hivyo hivyo vitambomoa...hii yanikumbusha mother of all battles Iraq; vyombo vya habari vilivyomjenga Sadam Husein, mtu hungeweza kuamini anaweza kushindwa
🙂🙂🙂!
Hizi mvua zinazomnyeshea Drumbf (Trump) kwa sasa ni rasharasha tu, subirini mvua za vuli zianze...sina hakika kama ataweza kuvuka salama! Kumbuka kila neno linalotoka mdomoni mwake litachambuliwa na kuchambuliwa na kuchamuliwa. Na mtu asikudanganye na mabilioni yake...kama kweli anayo, angetulia na asingeutamani Urais wa Marekani kwa sababu nafasi yake ya kuchaguliwa ni
positively nothing!