2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi

'This is one too many'' Sauti hizi zinaweza kupuuzwa na UKAWA kwa muda, mbele ya safari zitasikika pamoja na zile za nyikani, sitaki kubashiri ...!!!

Kwamba, taasisi inasimama kama mtu, I can't wrap up my head

Kwamba, mtu anachukua umiliki wa taasisi! Real

Ukawa waombe sana Mungu washinde urais. Endapo watashindwa itakuwa disaster, umoja utavunjika na kila mtu atachukua hamsini zake.
Tutaanza square one, hadi waje kusimama miaka mingine 20.
Siipendi CCM na sitakaa kuja kuwapigia kura maisha yangu. Bado sijaamua.
 
Habari hizi hazikuumizi wewe tu bali ni watanzania wote, tuliokuwa na imani na Chadema/Ukawa, tuliokuwa na imani na viongozi wetu, tuliopata majeraha kwa ajili ya Chadema/Ukawa, tuliokuwa mstari wa mbele kuelemisha wananchi jinsi ufisadi unavyowaadhiri wao na familia zao na nk.

Leo hii hawa viongozi tuliowaamini kuwa viongozi wetu wanajifungia chumbani na kuja na maamuzi ya kipumbavu namna hii. Hawezekeni viongozi wasiozidi 20 wajifungie ndani na kutuchagulia mgombea urais, hii haki hawana na hawatawahi kuwa nayo. Na kama wakingángánia na msimamo wao, ambao kipaumbele kwao ni matumbo yao basi huyu Lowassa wakamchague wenyewe..

Pendekezo langu ni kuwa watuache wananchama tuchangue ni nani tungependa hawe mgombea wetu.. Huitishwe uchaguzi kila kanda/ au hata baadhi ya mikoa ili wanachama wapinge kura ya ni nani kwa mtazamo wao wanaona anafaa kupeperusha bendera ya Ukawa. ..

Dada Alinda, tatizo labda ulikuwa na imani kubwa na viongozi wa siasa kuliko ulivyopaswa kuwa, hakuna principles kwenye vyama vyetu, siasa zetu hazina misingi za kusimamia ambazo unaweza sema chama hiki kinasimamia hapa, hakuna.Atleast ACT wanajaribu kujenga kwenye hilo. Vyama vyetu hivi vipo kotekote, ni fursa za matukio zinazotofautisha nani anaongelea nin wakati gani, na ukifikiri kuwa wanaongea wanayomaanisha utajipa pressure bure.Tuna wanasiasa wachache sana nchini hii wanaomaanisha wanachoongea, wengi ni just talk, ukiichukulia serious ndio matokeo yake haya.

Pia japo kikatiba ndivyo lakini Tanzania hatujafika bado kwa chama kuwa ni cha wanachama kwa maana ya nguvu ya wanachama, Waafrika bado tumejengeka kwenye misingi ya uchifu na huku kwenye vyama viongozi wa chama ndio kila kitu, japo hatukiri hadharani lakin fikra sahihi za viongozi wa chama ndio msingi wa maamuzi ya vyama, huo ndio ukweli ambao huna namna ya kuurekebisha kwa sasa, viongozi wa vyama huamua kwa niaba ya wanachama na vikao vyvyote vitakavyoitishwa ni kubariki tu uamuzi huo, la ukibishana/kukataa kilichoamuliwa na kiongozi wako basi ndipo jina lile maarufu MSALITI linapokuja, watu wengi hulichukulia neno hilo too serious kuliko ata lilivyo, ndivyo siasa zetu zilivyo.

Ni aibu unawezaje kumchangua mgombea urais mtu aliyejiunga/atakayejiunga ndani ya wiki 1? kama ACT wangefanya hivyo niwaelewa maana ni chama kichanga. Lakini si Chadema si Nccr si Cuf wala si NLD hivi vyama ni vyama vikongwe vina wagombea walioiva, vimejengwa usiku na mchana, mvua na jua leo hii unachukua kapi kutoka CCM na kulipa ugombea urais? Inamaana wakati mnajigenga hamkufahamu kuwa baada ya miaka 5 kuna uchanguzi hivyo ni muhimu kuandaa watu kama 3 au zaidi kwa ajili hiyo?

Ni aibu ni fedheha na ni masikitiko. Ila kura yangu, familia yangu na majirani zangu kamwe hazitakwenda kwa Lowassa.

Kisiasa uamuzi wa kumchukua Lowassa na kumfanya mgombea wa UKAWA ni miongoni mwa maamuzi ya manufaa sana kwa UKAWA yaliyofanyika, ata kama hawatashinda urais lakini kama kundi la Lowassa litamfuata UKAWA, kama ataweza kuendelea kuvikamata vyombo vya habari, kama ataweza kumaintain mtandao wake wa mobilization, kama ataweza kumaintain mtandao wake wa pesa za kampeni, ukiongeza na uzoefu wa kampeni/serikali/CCM basi kwenda na Lowassa kwenye uchaguzi ni bora bahati ya mtende kisiasa na itaipeleka UKAWA/Chadema kwenye level ya juu zaidi kisiasa kuliko ilivyo sasa.

Mbowe kaonyesha uongozi kwenye hili maana badala ya kujifariji amekuwa halisi zaidi, kwa kwenda na jeshi hili la kukodi wanaweza sasa kushinda urais, wanaweza kupata viti vingi zaidi vya ubunge kuliko ambavyo wangepata kwa kwenda na wagombea waliozoeleka, mathalani Dr Slaa au Prof Lipumba.

Lakini kingine ambacho hatukiongelei humu, ni factor ya Lowassa kwenye kuwaunganisha UKAWA, kumbuka kabla ya hili UKAWA ilikuwa kwenye mtihani mkubwa wa kuwa pamoja, Lowassa ana-cement mahusiano haya, Lowassa pia kupitia CCM Zanzibar ana uwezo wa kuisadia CUF kwenye uchaguzi wa Zanzibar.

Japo hili linaipa fursa pia CCM kuepuka mashambulizi juu ya ufisadi na kuipa nafasi sasa CCM kuitumia point hiyohiyo kujinadi kama chama kinachojisafisha na kinachorudi kwenye misingi ya kuasisiwa kwake, lakini mafanikio ya kampeni yatategemea timu hizi itakavyokuwa zimejipanga, zitakavyoubeba vizuri ujumbe wake bila kusahau upepo utakaobebwa na vyombo vya habari utakaosaidia kufanya ujumbe huo uaminike.Vyovyote itakavyokuwa ni risk worth taking.
 
Hivi ni vipengele vya katiba ya CHADEMA:
7.7.8
Wajumbe
wa Mkutano Mkuu Taifa watakuwa wafuatao:
-
(a)
Wajumbe wote wa Kamati Kuu
(b)
Wajumbe wote wa Baraza Kuu
(c)
Wenye viti wa Wilaya/Majimbo
(d)
Makatibu wote wa Majimbo/Wilaya
(e)
Wajumbe ishirini watakaochaguliwa na Mikutano Mikuu ya kila
Baraza la cham
a kuingia kwenye Mkutano Mkuu Taifa kwa
uwiano wa:
-
(i)
Wajumbe kumi na tano kutoka Tanzania Bara
(ii)
Wajumbe wa tano kutoka Tanzania Zanzibar kwa kila
baraza
(f)
Mjumbe Mwakilishi wa kila Wilaya
7.7.9
Mkutano Mkuu Taifa utakutana mara moja katika
kipindi cha miaka
mitano. Mikutano Mikuu maalum / dharura inaweza kuitishwa wakati
wowote ukiwepo ulazima kwa utaratibu utakaowekwa na Kanuni.
7.7.10
Kazi za Mkutano Mkuu wa Taifa ni:
-
(a)
Kuchagua Mwenyekiti wa Chama Taifa na Makamu wake wawili
(b)
Kuja
dili taarifa za Baraza Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo
kwa utekelezaji.
(c)
Kuteua mgombea wa Uraisi na mgombea wenza wake kwa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea Urais wa
Zanzibar.

(d)
Kujadili na kuridhia Itikadi, falsafa na sera za Chama kisha
kuweka mikakati na miongozo ya utekelezaji.
(e)
Kujadili na kuridhia programu ya Chama kwa kuzingatia
mapendekezo ya Baraza Kuu.
(f)
Kuzingatia na kutoa maamuzi juu ya rufaa na masuala ya
kinidhamu yanayowakilishwa na Baraza kuu.
(g)
Kupokea na kujadili t
aarifa ya Bodi ya wadhamini wa..

Viongozi wa Chadema tunaomba mtwambie ni lini mkutano mkuu umemchangua Lowassa kuwa mgombe urais??

Mkutano wa Baraza Kuu bila shaka utafanyika, lakini hautaweza kwenda kinyume na uamuzi ambao tayari umepitishwa na viongozi, kumbuka maamuzi yoyote yanahitaji maandalizi ambayo viongozi wote wa chama wataagizwa kuyafanya wanapowaleta wajumbe kwenye mkutano huo, na kufanya maandalizi(mobilization) yaliyo kinyume na walichoamua viongozi ni USALITI, adhabu yake pamoja na mengine ni kufukuzwa kwenye chama.Hivyo in reality uamuzi utakaotoka kamati kuu huo ndio uamuzi wa chama, huku kwingine ni kukamilisha ratiba tu.
 
Nipo hapa nafanya kazi na maisha mengine kwavile mkate wetu hautegemei kubeba viatu vya mtu. Wala usitaraji kutoweka

Nimesimama kutetea kile ninachokiona ni kweli kwa mujibu wangu. Tunaandika bila woga wala hofu. Hatuandikii chooni

Tunathubutu mchana kweupe, hatuandiki waraka tunajenga hoja

Mkuu hasira zako hazisadii maana mwisho wa siku kinachochambuliwa ni hoja.

Mjadala unaendelea

pole mkuu
 
Mkuu Waberoya

1. Unaweza kujadili hoja bila kutukana. Kutukana hutokea pale ambapo kuna ombwe la hoja.
Nadhani unafahamu kwanini jukwaa lilianzishwa. Kama unaona pana ugumu wa kujenga hoja bila kutukana,hamia kule

2. Midhali upo hapa unachangia na kusoma kwa bidii, hoja zilizopo zina akili. Vinginevyo, unawezaje kuhangaika na eneo lisilo na akili la wapumbavu. Nadhani ujiangalie kama kweli unatumia akili kusoma vitu visivyo na akili

3. Tumekuuliza uweke ushahidi wa chuki dhidi ya jamaa yako Zitto. Hujaweka! hivyo, maneno yako hayana uzito au mashiko

4. Tuweke kumbu kumbu sawa. Kwamba Zitto litenda mabaya, hilo halina ubishi. Atasimama ima kutetea au kuhukumiwa nalo. Wala hakuna hoja itakayondoa ukweli wa uzi huu

5. Yes ACT ni mpini wa kumaliza upinzani. Hoja ipo valid kwasababu ACT ya Cheyo inahukumiwa kama ACT si UDP

6. Tumesimama katika utaifa, hilo tumelisema na tunalisema. Hatutakubali siasa majitaka kama za ACT

7. Tumesimama kama taifa na umma umetuelewa.
Muulize 'mzee' kama anakanyaga Tanzania kama ilivyokuwa. Na hatutasimama, tutaendelea bila kumuonea mtu au kumhurumia

8. Unakumbuka kauli yangu kwako kila mara ?

Ukweli unatuweka huru ndio maana tunasimama bila na kusema hili tunalikubali hili hapana.

Kama tunavyomueleza Zitto na siasa zake za chuki dhidi ya kanda na makabila, vivyo hivyo tutaeleza mwingine na wengine kwa yale watakayotenda

Hapendwi mtu inapendwa hoja

naruadia tena pole mkuu! nakuelewa vizuri sana, imekuwa mapema mno, kuliko ilivyotarajiwa

tuendelee na hoja, najua uchungu wako, nashindwa namna ya kukufariji

ila sifa nyingi kwako mkuu, at least kuwa muwazi na kutopelekwa pelekwa

mengine ni yangu, nimeyabeba
 
'MAANDALIZI ' YA UCHAGUZI YANAENDELEA

TAFITI ZINA MENGI ZAIDI YA NAMBA

GOLI LA MKONO NI UKWELI AU UZUSHI?

Kuelekea uchaguzi, tumewaasa wapinzani kuhusu uchaguzi. Tumesisitiza, mikutano tu na sanduku la kura haitoshi

Katika nchi zenye demokrasia za mashaka kuna mambo yanayotakiwa kuangaliwa kwa upeo mpana

Majuzi wameteuliwa wajumbe wa tume ya uchaguzi

Hatujui ni kwasababu zipi lakini busara hazionyeshi kama hilo lilikuwa jambo la kufanywa kwa muda huu.

Tumesikia kauli za mwenyekiti wa tume akikemea udini kwa wapinzani.

Huko mitaani kampeni za ukanda na ukabila zinafanyika bila wasi wasi

Kilichoshtua wengine ni mwenyekiti wa tume alipopuuza kauli za CCM kwamba wapinzani hawawezi kwenda Ikulu kwa njia yoyote

Kauli hiyo si ya kampeni tukiiangalia vema. CCM wakiwa na vyombo vyote vya dola na serikali, kauli hiyo ni kuashiria hali isiyo nzuri.

Kwamba, inaweza kuwa ni maagizo ya chama tawala au inaweza kutokea hataka kama haipaswi.

Kuidharau kauli hiyo kwa kisingizio cha kampeni ni jambo tunaloliona ni la hatari na halikuwa na mizania

Siku za karibuni taasisi za tafiti za uchaguzi zimetoa matokeo.

Huko nyuma taasisi iliyokuwa inaongoza kwa tafiti hizo ni REDET ambayo wananchi wametokea kuidharau.

Viongozi wa REDET wameonekana kushiriki shughuli katika hali ya ukada wa vyama vya siasa

CCM kupitia tafiti zao zisizojulikana ziefanyikaje nayo imetoa tafiti zake ikionyesha namba zinazofanana sana na tafiti zinazoendelea

Tafiti ya Twaweza imekuja kukiwa na malalamiko mengi katika jamii juu ya usahihi wake.

Malalamiko hayo yameondoa ile thamani 'tarajiwa' ya tafiti hizo

Leo synovate wametoa tafiti, ambayo haina matokeo tofauti na yale ya CCM na Twaweza

Pengine inaweza kuwa ni msisito mzuri kuwa tafiti za Twaweza na CCM zinawiana na tafiti nyingine ili kuondoa sintofahamu

Tafiti zinaweza kufanana hata hivyo, hata kama zimefanyika nyakati tofauti au za karibu sana kama hizi tunazoona

Tafiti hizi zimekuja ikiwa ni takribani mwezi mmoja kamili hadi uchaguzi.

Zimekuja kukiwa na mkanganyiko wa kampeni na hali kutokuwa nzuri hasa kwa upande husika.

Hatuwezi kupingana na takwimu zao, isipokuwa tunazihoji kwa kina na kubaki na maswali mengi kuliko majibu

Kwa mtazamo wetu, taasisi zote zinaonekana kukaa ''kikao'' na kuamua tafiti zianze lini na zimalizike lini.

Katika kipindi cha wiki moja tafiti zote ikiwemo ya CCM zimetoka, ndani ya mwezi mmoja kuelekea uchaguzi.

Pengine huo ni muda wa kutosha, hata hivyo kuna maswali yanatatiza sana

Katika nchi za wenzetu, tumeshuhudia tafiti zikiwa kichocheo au kivunja moyo cha kambi husika.

Na mara nyingi sana tafiti hutegemea upande kama sehemu ya kampeni ukiacha zile za kimataifa zinazohifadhi hadhi na heshima yao

Huko nyuma MwanaCCM mmoja alizungumzia goli la mkono. Kwamba, iwe iwavyo CCM itashinda hata kwa goli la mkono

Kauli hiyo imefuatiwa na ile ya wapinzani hawawezi kuingia Ikulu kwa njia yoyote

Goli la mkono katika nchi ya kidemokrasia si jambo zuri. Na wala goli la mkono si kura au wizi tu.

Goli la mkono ni lazima laweza kuwa la kisaikolijia kwa wahusika.

Ni kwa njia hiyo goli la mkono linaweza kupata uhalali hata referee kupeta ikiwa limejengewa mazingira mazuri toka mwanzo

Goli la mkono walilosema CCM inaweza kuwa mzaha, hata hivyo, lisidharauliwe maana linawezekana kabisa.

Haiwezekani kauli ya goli la mkono ianguke kutoka hewani tena wahusika wakiwa kimya na viongozi wakiwa kimya!

Goli la mkono hatujui ni kitu gani, inaweza kuwa kauli ya kampeni kama ile ya hawezi kwenda Ikulu.

Tume ya uchaguzi inaweza kutusaidia maana hatujui goli la mkono katika uchaguzi wa kura lina maana gani

Tusemezane
 
Hakuna Demokrasia ya kweli Tanzania. Chama Tawala CCM kinainajisi Demokrasia na hata washiriki na wasaidizi kwa utashi binafsi au utashi wa kulazimishwa ambao ni Dola na Taasisi zinazopaswa kuwa huru kusimamia haki na usawa, zimeegemea kuhakikisha kuwa uhalali wa CCM kuendelea kutawala hata kwa kudhulumu na kuinajisi haki na demokrasia inaendelea.

Ufahali huu wa kudharau watu na kutojali haki na demokrasia, kunatikisa kwa nguvu kiberiti cha uvumulivu uliotufanya tuwe tulivu na kujifanya kuwa na amani kwa unafiki.
 
Unajua CCM ya Nyerere ilikuwa inakubalika kuwa Chama Dola kwa kuwa kilikuwa ni chama kinachofanya kazi kwa ajili ya wananchi wake. Lakini CCM ya Mwinyi ilikuwa hewani japo ilikuwa chama dola, ya Mkapa ikawa ya wawekezaji na ikaanza kuwa na "wawekezaji" wazawa waliokitumia kama kichoteo cha utajiri na ngao ya ulinzi kwa mafisadi, lakini bado ni chama dola. Madhara ndio haya tunayoyaona.
 
'MAANDALIZI ' YA UCHAGUZI YANAENDELEA

TAFITI ZINA MENGI ZAIDI YA NAMBA

GOLI LA MKONO NI UKWELI AU UZUSHI?

Kuelekea uchaguzi, tumewaasa wapinzani kuhusu uchaguzi. Tumesisitiza, mikutano tu na sanduku la kura haitoshi

Katika nchi zenye demokrasia za mashaka kuna mambo yanayotakiwa kuangaliwa kwa upeo mpana

Majuzi wameteuliwa wajumbe wa tume ya uchaguzi

Hatujui ni kwasababu zipi lakini busara hazionyeshi kama hilo lilikuwa jambo la kufanywa kwa muda huu.

Tumesikia kauli za mwenyekiti wa tume akikemea udini kwa wapinzani.

Huko mitaani kampeni za ukanda na ukabila zinafanyika bila wasi wasi

Kilichoshtua wengine ni mwenyekiti wa tume alipopuuza kauli za CCM kwamba wapinzani hawawezi kwenda Ikulu kwa njia yoyote

Kauli hiyo si ya kampeni tukiiangalia vema. CCM wakiwa na vyombo vyote vya dola na serikali, kauli hiyo ni kuashiria hali isiyo nzuri.

Kwamba, inaweza kuwa ni maagizo ya chama tawala au inaweza kutokea hataka kama haipaswi.

Kuidharau kauli hiyo kwa kisingizio cha kampeni ni jambo tunaloliona ni la hatari na halikuwa na mizania

Siku za karibuni taasisi za tafiti za uchaguzi zimetoa matokeo.

Huko nyuma taasisi iliyokuwa inaongoza kwa tafiti hizo ni REDET ambayo wananchi wametokea kuidharau.

Viongozi wa REDET wameonekana kushiriki shughuli katika hali ya ukada wa vyama vya siasa

CCM kupitia tafiti zao zisizojulikana ziefanyikaje nayo imetoa tafiti zake ikionyesha namba zinazofanana sana na tafiti zinazoendelea

Tafiti ya Twaweza imekuja kukiwa na malalamiko mengi katika jamii juu ya usahihi wake.

Malalamiko hayo yameondoa ile thamani 'tarajiwa' ya tafiti hizo

Leo synovate wametoa tafiti, ambayo haina matokeo tofauti na yale ya CCM na Twaweza

Pengine inaweza kuwa ni msisito mzuri kuwa tafiti za Twaweza na CCM zinawiana na tafiti nyingine ili kuondoa sintofahamu

Tafiti zinaweza kufanana hata hivyo, hata kama zimefanyika nyakati tofauti au za karibu sana kama hizi tunazoona

Tafiti hizi zimekuja ikiwa ni takribani mwezi mmoja kamili hadi uchaguzi.

Zimekuja kukiwa na mkanganyiko wa kampeni na hali kutokuwa nzuri hasa kwa upande husika.

Hatuwezi kupingana na takwimu zao, isipokuwa tunazihoji kwa kina na kubaki na maswali mengi kuliko majibu

Kwa mtazamo wetu, taasisi zote zinaonekana kukaa ''kikao'' na kuamua tafiti zianze lini na zimalizike lini.

Katika kipindi cha wiki moja tafiti zote ikiwemo ya CCM zimetoka, ndani ya mwezi mmoja kuelekea uchaguzi.

Pengine huo ni muda wa kutosha, hata hivyo kuna maswali yanatatiza sana

Katika nchi za wenzetu, tumeshuhudia tafiti zikiwa kichocheo au kivunja moyo cha kambi husika.

Na mara nyingi sana tafiti hutegemea upande kama sehemu ya kampeni ukiacha zile za kimataifa zinazohifadhi hadhi na heshima yao

Huko nyuma MwanaCCM mmoja alizungumzia goli la mkono. Kwamba, iwe iwavyo CCM itashinda hata kwa goli la mkono

Kauli hiyo imefuatiwa na ile ya wapinzani hawawezi kuingia Ikulu kwa njia yoyote

Goli la mkono katika nchi ya kidemokrasia si jambo zuri. Na wala goli la mkono si kura au wizi tu.

Goli la mkono ni lazima laweza kuwa la kisaikolijia kwa wahusika.

Ni kwa njia hiyo goli la mkono linaweza kupata uhalali hata referee kupeta ikiwa limejengewa mazingira mazuri toka mwanzo

Goli la mkono walilosema CCM inaweza kuwa mzaha, hata hivyo, lisidharauliwe maana linawezekana kabisa.

Haiwezekani kauli ya goli la mkono ianguke kutoka hewani tena wahusika wakiwa kimya na viongozi wakiwa kimya!

Goli la mkono hatujui ni kitu gani, inaweza kuwa kauli ya kampeni kama ile ya hawezi kwenda Ikulu.

Tume ya uchaguzi inaweza kutusaidia maana hatujui goli la mkono katika uchaguzi wa kura lina maana gani

Tusemezane

Mwalimu wangu Nguruvi3 kwema? Unisamehe kwa kukaa kimya muda mrefu Jamvini, nilikua na majukumu mengi kdg, japo huwa nakusoma sana pamoja na wadau wengine wa Jamvi.

back to the topic, nimeufuatilia uchaguzi huu kwa karibu sana na mpaka sasa kumekua na sintofaham nyingi sana kwa pande zote CCM na Upinzani ( hapa nawazungumzia UKAWA maana ACT kwa hakika wanasikitisha na sidhani kama ni wapinzani halisi kwa mienendo yao). Pia nafasi ya tume na vyombo vingine vya dola Nitawazungumzia kdg hapo chini ACT na nafasi yao kwa uchaguzi huu.

Kwa upande wa upinzani nimewaona kama vile walikua bado hawajajipanga kwenye kugawana majimbo vizuri na hii inawaletea migogoro ambayo kimsingi haikupaswa kuwepo kabisa, maana inawapa mwanya adui yao kujipenyeza miongoni mwao na kuwachezesha shere bila sababu ya msingi, hii athari yake ni kubwa sana kwenye umoja wao na pia kujipanga zaidi kwaajilinya nafasi ya uraisi, pia bado msisitizo wa kuelewa kwamba sio UKAWA wanaogombea bali ni CDM maana kama vile watachanganyikiwa. Pia viongozi wengi wa UKAWA ni kama hawajielewi wanakurupuka sana na kujikuta wanakosa focus.

Ka CCM kwa mara ya kwanza nimeona kampeni za kipekee na zinazojaa kahsfa, matusi na personal attacks kwa upinzani tena wazi wazi bila kukemewa kuna "character assassination" ya wazi kabisa, mfani juzi nilimshuhudia mtu anaitwa Msukuma anasema mgombea alijisaidia jukwaani (alitumia abusive language ambayo siwezi kuiweka hapa), nilitegemea angalau akemewe au hata kuombewe radhi, looo kumbe ndio mmtindo, kimsingi ni siasa za kupanic sana. Zamani wapinzani walikua wanasiasa za namna hii na za hofu kubwa ila sasa ajabu CCM ndio wamekua na panic ya ajabu mno ya personal attacks, mgombea anajitahidi kutokwenda huko ila jopo lake linamdrag kwenda huko.

Udini na ukabila, kipekee hili jambo hata kama hatulitaki bado linaonekana kuchomoza na ninhatari sana kwa taifa, mgombea wa UKAWA aliropoka kanisani Tabora kuhusu dhehebu lake, akaomba radhi haraka, ila sasa ikazid7 kuchichewa na wapinzani wake saaana na kuchichewa kuni mpaka kuifanya big deal na kete kwao, ila sidhani kama ni uugwana kwa hawa watu kuendelea kueneza propoganda za namna hii maana ni hatari.
Pia suala la Ukabila ni risk sana kwa taifa, tumeshuhudia makada wakipiga kampeni na kuomba kura kikabila tena kwa kuongea kwamba huyu mtu ni wa kwetu, yale yale ya kanisani, inatisha sana, siasa za amna hii zitalipasua taifa siku za usoni, ni mbegu mbaya sana na nadhani tume na msajili wanaona haya.
Juzi nimeona tamko la jumuia fulani hivi ya kiislam imetoa tamko lake, ukilisoma lile tangazo na maudhui yake, utaona kwa jicho la tatu kwamba kuna shida mahali na kuna kitu nyuma yake, kwa kipindi hiki sitarajii kabisa eti taasisi huru kama ya dini ielekeze wafuasi wake eti wasipigie kura mtu fulani au chama fulani, ni ajabu sana.

ACT, mkuu Nguruvi3 kwa hili nakukumbuka sana, mada yako ya ACT mpini wa CCM kuua upinzani, mwanzo sikukuelewa kabisa, ila sasa nakuelewa vizuri kwa nn uliyaona haya miezi mingi nyuma, chaajabu kabisa watu wa chama hili kutwa kucha kazi yao ni kushambulia CDM kuliko CCM, klimsikiliza Mchange pale Zakiem, yeyekwake yeyekwake adui ni CDM na Lowassa tu sio CCM. Nimewafuatilia makada wao mitandaoni nao ni balaa, wanawapiga mawe wapinzani kuliko CCM, nabaki kujiuliza wapo kutaka dola inayoshikiliwa na CCM au wapo kutaka kuwa chama mbadala wa upinzani?? Kwamba wao wana vision ya kuwa wapinzani tu tena chini ya CCM na sio kushika dola.

Tume na vyombo vya dola, ni muhimu sana sasa tume iwe balanced kuwakemea wote wanaovunja kanuni bila kuangalia chama atokacho mtu, mathalani wengine wakikamatwa kwa kuzidisha wengine wakaachwa inazua maswali mengi sana kwamba hii sheria ipo kwaajili ya watu fulani tu au wote, hili pia ni kwa polisi, kama wameamua ku exercise nguvu yao kwa wavunja kanuni kama kuwakamata viongizi basi iwe ni kwa wote ili kundoa maswali na sintofaham.

Mwisho, kuna maisha baada ya uchaguzi, heshima na staha ni jambo la msingi sana, pia mambo yanayoelekea kuligawa taifa hili either kwa ukabila au udini basi ukemewe kwa uwazi bila aibu kabisa kwa yoyote anayetumia mbinu hizi chafu, maana tunaweza kuona ni lugha za kisiasa au kampeni, ila kimsingi tunajenga precedence na sumu mbaya sana kwa taifa.

Kimsingi nautazama uchaguzi huu kwa jicho la pekee sana na ni amuomba Mungu atuvushe salama
 
wewe na wenzako msiilamikie ACT,nyie ndio mlianza kuishambulia ACT ata kabla ya kupata usajili wa dumu,kwa niaba ya CHADEMA, na ACT iliposajiliwa haikuwa na namna kujibu Hoja zenu,na CHAMA chenu mlichokua mnakipigia chapuo,Leo mnalia lia tu,kipindi Kuna tetesi LOWASA kwenda ACT ilionekana mpango wa kuhijumu CDM.

mjitathimini upya juu ya uandishi wenu wa kuidhurumu ACT,nakumbuka Mchambuzi alisema atazunguka nchi mzima kupiga kampeni kuwa ACT wazalendo, sio CHAMA HALALI,sijui kaishia wapii
 
Last edited by a moderator:

Ndugu yangu sina hakika kama huwa unztusom sawasawa, kwanza nianze kwa kukusahisha, mimi binafsi sina chama chochote cha siasa na wala sina kadi au uhusiano wowote na chama chochote, mabandiko yangu huwa yanalenga mtazamo wangu binafsi kwa maendele ya nchi yetu na demokrasia kwa ujumla wake, so usinihusishe na chama chochote, na pole kama utakua unaniona naegemea popote sina nasaba na chama chochote.

Back to your argument, kimsingi mkuu Adharusi sisi tunakosoa, kuonya na kushauri kwa jambo lolote bila kubagua chama, itikadi wala nafai ya mtu, kama umetusoma vizuri kuanzia hao CDM unaodhania tuna nasaba nao mara nyingi tumewakosoa na kuwakemea na pia kuwaonya kwa madhaifu yao mengi sana, ukiweza refer baadhi ya nyuzi kama "Juice ya maembe ikulu", "ukawa na uwekezaji usiotabirika" Makosa ya waoinzani kuelekea uchaguzi mkuu na mabandiko mengine mengi, kama wewe ni mkweli wa nafsi yako utakubaliana kwamba kwenye suala la kukosoa na kuonya hatubagui yyt kuanzia Wapinzani mpaka watawala. Usituhukumu kwa mafikirio yako yasiyo sahihi.

Kuhusu ACT, hapa tunasema wazi kabisa kwamba ni chama ambacho kipo designed kuboa upinzani hasa CDM, malengo ya kuundwa kwake toka mwanzo ni hasira za wao kufukuzwa walikukua so kwa sasa wanaongozwa na personal engravance dhidi ya CDM na kuona kwamba wao ndio adui yao namba moja, kwa kifupi focus yao ni kuibomoa CDM na wao kuwa chama mbadala. well sijajua matazamio yao ila kimsingi wanafanya kazi ya kuisaidia CCM dhidi ya wapinzani wao hasa kipindi hiki cha uchaguzi. Mimi haininipi shida yyt la tu nahoji nini malengo a focus ya hiki chama??

Umezungumzia kwamba sasa wanajibu hoja za CDM, hapa sio kweli hata kdg huwezi kujibu hoja kwa matusi, kashfa na fitina, hoja wangejibu kwa kujipambanua kwa sera zao bila kufanya personal attacks kwa CDM na kuonyesha kwamba wao ni wataarabu na hawapo kulipiza kisasi kwa namna yyt ile, mkuu hebu angalia matamshi ya viongozi wao kama H.Mchange,Mwigamba, Kitila na wengine kuanzia majukwaani mpaka mitandaoni, wanajibu hoja za CDM? Jewanajua wanapambana na nani kwenye uchaguzi huu?? Je focus yao kubwa nn?
 
KOSA LA KIUFUNDI WANALOFANYA

HALI SI NZURI, CCM WAMEPOTEZA MWELEKEO

MBINU HIZI ZITAWARUDI

Kuelekea uchaguzi jumapili , kampeni zinafikia tamanati.

Katika kufunga kampeni kuna mbinu zinatumiwa na makundi ili kushinda kura.

Mbinu za karibuni ni zile za kumhusisha Lowassa na Richmond pamoja na mgao wa umeme

Kwa wachambuzi wa mambo ya kisiasa, hii si dalili njema kwa upande wa chama tawala.

Haina maana watapoteza uchaguzi, inaashairia uwezekano wa kupoteza mihImili, mhimili au nguvu katika bunge (2/3)

Tuhuma dhidi ya Lowassa zinawarudi wenyewe. Kila mtu anafahamu Lowassa alikuwa kada wa CCM na nyakati zote CCM walikuwa kimya bila kumtupia lawama, madongo au tuhuma. Ni hadi pale alipoondoka, CCM wanakuja na mbinu hizo

Wananchi wanafahamu yaliyotokea. Hata kama wataaminishwa ubaya wa Lowassa, kuna maswali mengi kuliko majibu

Kwanza, ikiwa CCM walifahamu ubaya wake, ilikuwaje walimwacha hadi kujijenga kiasi hicho?

Pili, ikiwa CCM walifahamu madhambi yake kwanini hawakuchukua hatua dhidi yake kwa wakati ule?

Tatu, CCM wanapokuja na tuhuma dhidi yake, hoja ni nini hasa kwani wananchi hawana vyombo vya dola

Nne, kwanini CCM wadhani kuwa matatizo kama Richmond ni makubwa kuliko mengine kama Escrow na wanyama pori?

Hadi hapo, maswali yanaiweka CCM ''on spot' kwa maana kuwa suala kama la Escrow linarudi masikioni kwa namna nyingine

Hili la Richmond lilizuiwa na CCM bungeni kwa kutumia wingi wao, wananchi watajiuliza, kama walijua kuna uovu kwanini walikaa kimya hadi siku za uchaguzi?

Lakini pia wananchi wanajiuliza, wapi CCM ilipo na inatetea vipi rekodi yake ambayo kwa miaka 10 tu iliyopita imegubikwa na kashfa, ufujaji wa pesa n.k. katika utendaji wake. Hayo yanafanywa chini ya hao hao wanaoleta mashtaka mbele ya wananchi.

Kwanini CCM isieleze imefanya nini kukabiliana na uhalifu wanaousema, bali imejikita kuleta mashtaka kwa wananchi

Ni kutokana na hilo, wananchi wengi wanaonekana wameshafanya maamuzi iwe kuichagua au la

Hizi habari za kuleta mashtaka CCM ikiwa na dola na vyombo vyake ni ishara ya hali kuwa tete.

Hali ni mbaya wakijua uwezekano wa kupoteza meli upo, au meli kuzama na kubaki na mzigo upo au mzigo kuzama na kubaki na meli

Anayewashauri CCM katika hatua hizi za mwisho hakufikiri.

Unapoleta suala la kashfa ni sawa na kuamsha vidonda vilivyokuwa vimesahaulika.

Hatudhani kuwa Richmond ni tatizo zaidi ya mengi yaliyotokea

Hao wanaopita wakikumbusha Richmond, wanakumbusha ESCROW na Wanyamapori waliopanda ndege

Wanakumbusha jinsi ndege za jeshi la nchi nyingine zinavyoweza kuingia nchini na kubeba wanyama chini ya uangalizi wa CCM.

Hili katika siasa linaitwa technical mistake, si error au glitch ni dalili kuwa li[po jambo

Katika mazingira ya kwaida, CCM walipaswa kutetea rekodi ya miaka 50 ambayo ni mtaji mkubwa. Hakuna anayezungumzia, wamejikita katika kashfa nyingi zikiwa zimetendwa na makada wao wawe CCM au wamehama

Hakuna sababu ya CCM kuleta mashtaka, hoja ni je walifanya nini kuzuia uhalifu.

Kama hawakutenda lolote, mashtaka yanawezaje kuwasaidia wananchi na wananchi wana nguvu ipi zaidi ya ile CCM waliyopewa kikatiba?

Hili la Richmond, limeamsha vidonda na CCM italipa gharama kwa kiasi fulani. Aliyewashauri amewadanya

Watu wanAzungumzia kashfa zote baada ya haya kuibuliwa, je hilo linawasaidia CCM?

Tusemezane
 
Rais JK .

Anatueleza kile alichosema Mnyika

1 Aliyeapa kulinda mali na watu wa Tanzania ni Rais

2 Aliyepewa mamlaka ya kuunda serikali ni Rais

3Aliyepewa mamlaka ya kuteua waziri mkuu ni Rais

Waziri mkuu ni kiongozi wa serikali bungeni, si kiongozi wa nchi. Kazi yake ni kusimamia , kutetea na kutekeleza maagizo ya serikali iliyoundwa na Rais bungeni.

Inapotokea sintofahamu waziri mkuu humuona bosi wake ambaye ni Rais kwa maamuzi ya mwisho. Waziri mkuu hana maamuzi ya mwisho kwasababu anawajibika kwa Rais

Rais ndiye mwenyekiti wa baraza la mawaziri ambalo waziri mkuu yumo kama mjumbe. Mwenye baraza ni Rais

Rais ndiye mkuu wa vyombo vya usalama na ulinzi wa nchi zikiwemo taasisi nyeti zinazowajibika kwake

Rais aliwahi kuhojiwa na kusema ' Hakuona tatizo na Richmond'

Waziri mkuu alipojiuzulu Rais akasema 'ni ajali ya kisiasa'. Hakuwaeleza wananchi tatizo lilikuwa wapi au nani

Bungeni Lowassa alitaka suala lirudi, aliyezuia ni Spika Sitta kwa maelekezo ya serikali inayoongozwa na Rais

Kwa miaka Zaidi ya 8 Rais hakuwahi kuwaeleza wananchi tatizo ni lipi na nani anahusika

Miaka 8 hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika

Kilichofanyika ni Dowans na mengine tunayojua ni watoto wa Richmond

Lowassa amechukua fomu CCM,Mwenyekiti wa CCM aliona hilo. Walimkata hakutueleza sababu

Leo Rais aliyetueleza ni ajali ya kisiasa, na ambaye kwa miaka 8 amemuezi Lowassa high table, anatuambia ni ya Lowassa

Kama alijua ni ya Lowassa na kuna tatizo kwanini hakumchukulia hatua?

Leo siku yake ya mwisho ofisini anatueleza jinsi alivyoshindwa kusimamia serikali yake mwenyewe.

Anatueleza matatizo kana kwamba alichaguliwa kutueleza matatizo na si kutafuta suluhu.

Anataka watu wachukue hatua ili hali alikuwa na vyombo vyote na hakujaribu.

Rais analalamika kwa wananchi!!!

Tujiulize, hivi hasara ya Richmond ndiyo tatizo pekee nchi hii? Mbona Rais hakutueleza wanyama walivyopanda ndege. Nani alihusika? Mbona hakutueleza kwanini aliwapa wahalifu nafasi ya kurudisha pesa za kashfa zingine?

Rais hakutupa summary ya Kagoda, meremeta na juzi Escrow. Hakulalamika kuhusu uchafu huo anatueleza Richmond

Rais hakutueleza safari 410 zimelisaidiaje taifa

Inasikitisha sana, kwamba akijua tatizo akliacha leo anatumia tatizo liloumizataifa kuomba kura

Kama Richmond ni ya EL, EPA, KAGODA , ESROW ni zanani? Lini atatuambia wahusika?

Inaendelea
 
SUALA LA AFYA

Katika hali ya kawaida, afya ya mtu ni jambo sensitive. Hata hivyo, kama tunaogelea wagombea pengine limepungua ukakasi.

Rais alipozungumzia afya ya mtu akiwa kiongozi wa umma ni jambo lililostikisha wengi

Linasikitisha wengi kwasababu wakati anagombea ameaunguka mara kadhaa, na hakuna taarifa yoyote inayoweza kueleza tatizo lake.

Umma uliingiwa na simanzi kwa kutambua ni binadamu, yanapomfika ni mapenzi ya mwenyezi nasi tunapaswa kusikitika

Lakini pia hakuna anayeweza kueleza kwa uyakinifu Safari za Mh Rais huko Marekani zilikuwa ni za kiserikali au zilikuwepo nyingine

Wakati alipokwenda Marekani kwa matibabu ya tezi dume, watu walidhani amehudhuria mkutano kumbe alikuwa hospitali

Kama afya ingekuwa kigezo katika taifa letu, Kikwete asingekuwa Rais.

Alishaonyesha afya mgogoro kila mara alipokuwa anaanguka majukwani. Iweje leo hiyo aione kama agenda?

Alipomchagua Lowassa , je hakujua afya yake ilikuwa na matatizo kama alivyodai leo?

Katika hali ya uungwana, kuzungumzia afya ya mtu katika kampeni za siasa ni kunyanyapaa na kumdhalilisha.

Hatudhani kama ugonjwa unaweza kutumika kuomba kura.

Yapo mengi ambayo Rais alikuwa na fursa ya kuyaeleza bila kuleta idhara ya afya

Pengine hli linaonyesha CCM ilivyoishiwa kiasi cha kugeuza personality kama matatizo ya Watanzania

Rais hakutenda haki,na Watanzania pengine wamekereka kuliko CCM ilivyotarajia.Mzaha na afya ya mtu si jambo la kuchekelea

Hata hivyo, chama hicho cha Mwalimu Nyerere kimeingia na hofu kwa kuzingatia ukweli kuwa hali si ile iliyozoeleka na kwamba kijiti kinaweza kuvunja mwiko na hilo laweza kutia wahusika kiwewe.

Ndiyo hayo tuliyosikia Mwanza, si sera bali mjadala wa mtu na afya yake

CCM kuanzia kwa JKN na pengine kupunzishwa kwa JMK si jambo la masihara.

Siasa za namna hii ni hatari kwani zinachangia sana uwepo wa hasira, chuki na visasi

Kuna yoyote awaye anayeweza kutuuliza 'kwanini sisi Tanzania ni masikini"

Tusemezane
 
KWANINI CCM WAMEKWENDA MWANZA

JK ALIYASEMA YA RICHMOND NA AFYA KWA BAHATI MBAYA?

CCM imefunga kampeni zake katika mikoa ya kanda ya ziwa. Ni mikoa yenye wakazi na wapiga kura. Kubwa Zaidi huko ndiko anakotoka mgombea wao

Katika hali ya kawaida, mkoa wa Mwanza haukuwa eneo la hofu na kwa kuzingatia mgombea ni mwenyeji wa huko, ushindi ulioenkana kuwa ni dhahiri. CCM pengine wangeonekana katika maeneo yaliyogeuka miba kama Mbeya na Iringa, haikuwa hivyo!!

Wameelekea Mwanza kutokana na nguvu kubwa sana ya upinzani inayoonekana eneo hilo. Kazi hiyo ingegawa kura za kanda ya ziwa. Kwa kutambua baadhi ya maeneo yamekuwa na 'uasi' kama mikoa ya kusini dhidi ya CCM na kwa kujua kuna maeneo imeshapoteza kama Mbeya, Kilimanjaro na Arusha CCM haikuwa na budi bali kurudi Mwanza

Kurejea Mwanza ni katika hesabu za kupata wapiga kura wa maeneo hayo ambayo tunaweza kusema hayatabiriki kiurahisi

Kauli ya Mwenyekiti wa CCM kuhusu Richmond haikuja kwa bahati mbaya. Imetolewa siku za mwisho za kampeni ili kuzuia uharibifu ambao ungeweza kutokea. CCM wanafahamu kwa miaka 8 ya JK nchi imeongozwa kwa kashfa za wizi na ufisadi

Nyingi ya hizo, zilifanyika Lowassa akiwa hayupo. Kuongealea Richmond mapema kungeamsha vidonda vya EPA, Kagoda, Escrow na mlolongo mwingine. Njia iliyokuwa bora ni kuongelea siku ya mwisho ili wananchi wasiwe na nafasi ya kusikia au kujadili tena

CCM walichosahau ni kuwa chuki dhidi yao ambayo ni ya wazi imetokana na wananchi wengi kuchoshwa, si na rushwa au ufisadi bali namna serikali ilivyoshughulikia mambo hayo. Kwamba, hakukuwa na lolote lililofanyika kukabiliana na hujuma dhidi ya nchi. Hata mgombea wa CCM amesema atapambana na rushwa na kuziba mianya hiyo

Hii ina maana Magufuli ambaye ni waziri wa JK anajua rushwa ilivyotawala kwa miaka 10 ya utawala wa JK

Maswali ya kujiuliza, je wananchi watabadili misimamo yao kutokana na hotuba za jana

Kwa jicho pevu, hata pale walipoaminishwa Fulani ni jambazi, mwizi na mnayng'anyi, wananchi wameonekana kutojali
Kwa maneno mengi, wizi ujambazi na ufisadi ni dalili tu za maradhi, lakini maradhi ni serikali dhaifu iliyolea yote

JK anaposimama na kumnadi Mgombea wake, kwa kiasi Fulani ameamsha hisia badala ya kuzuia.

Watu hawajali tena kuhusu rushwa kwasababu ni mfumo rasmi wa CCM na JK katika miaka 10. Kinachoonekana ni watu kuwa na upinzani tu kwavile wamechoka

Hotuba ya JK hatudhani kama itakuwa na manufaa kwa CCM kwasababu watu wengi walishaamua ima kuiunga mkono CCM au kuitosa. Hatudhani wale waliosimama kumzomea Magufuli mbele ya FFU wanaweza kubadili msimamo wao usiku mmoja. Na wale walioamini tu kuwa CCM ndio yenyewe wanaweza kubadili msimamo wao asubuhi hii

Hata hivyo, JK amemamliza muda wake akiacha legacy itakayomwandama kwa muda mrefu huko ustaafuni. Haya ya kusema hakujua Richmond wakati yeye ndiye mwenye dhamana yanaeleza mengi juu ya utawala wake ambayo pengine hatapenda kuyasikia lakini yatasemwa yataandikwa

Haya ya kuongelea afya za watu, nayo yataacha doa kubwa kwake siku za mbeleni.

Iwe iwavyo, JK amekiacha chama cha Mwalimu Nyerere katika hali mbaya sana. Matokeo ya aina yoyote hayawezi kunasua na hilo. Bado CCM wanaamini chama kimedhoofika kama si kufikia mikononi mwa JK.

Jioni ya leo na kuendelea zitaeleza kwa undani kuhusu JK bila yeye kuwa na fursa ya kujitetea

Tujiulize, mihimili miwili itakapokuwa na umiliki tofauti nini kitafuata kwa katiba hii ya 1977?

Tusemezane
 
KWANINI CCM WAMEKWENDA MWANZA

JK ALIYASEMA YA RICHMOND NA AFYA KWA BAHATI MBAYA?

CCM imefunga kampeni zake katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Ni mikoa yenye wakazi na wapiga kura wengi. Kubwa Zaidi huko ndiko anakotoka mgombea wao

Katika hali ya kawaida, mkoa wa Mwanza haukuwa eneo la hofu na kwa kuzingatia mgombea ni mwenyeji wa huko, ushindi ulioenkana kuwa dhahiri. CCM pengine wangeonekana katika maeneo yaliyogeuka miba kama Mbeya na Iringa, haikuwa hivyo!!

Wameelekea Mwanza kutokana na nguvu kubwa sana ya upinzani inayoonekana eneo hilo.

Kazi hiyo ingegawa kura za kanda ya ziwa. Kwa kutambua baadhi ya maeneo yamekuwa na 'uasi' kama mikoa ya kusini dhidi ya CCM na kwa kujua kuna maeneo imeshapoteza kama Mbeya, Kilimanjaro na Arusha CCM haikuwa na budi bali kurudi Mwanza

Kurejea Mwanza ni katika hesabu za kupata wapiga kura wa maeneo hayo ambayo tunaweza kusema hayatabiriki kiurahisi

Kauli ya Mwenyekiti wa CCM kuhusu Richmond haikuja kwa bahati mbaya.

Imetolewa siku za mwisho za kampeni ili kuzuia uharibifu ambao ungeweza kutokea.

CCM wanafahamu kwa miaka 8 ya JK nchi imeongozwa kwa kashfa za wizi na ufisadi

Nyingi ya hizo, zilifanyika Lowassa akiwa hayupo. Kuongealea Richmond mapema kungeamsha vidonda vya EPA, Kagoda, Escrow na mlolongo mwingine. Njia iliyokuwa bora ni kuongelea siku ya mwisho ili wananchi wasiwe na nafasi ya kusikia au kujadili tena

CCM walichosahau ni kuwa chuki dhidi yao ambayo ni ya wazi imetokana na wananchi wengi kuchoshwa, si na rushwa au ufisadi bali namna serikali ilivyoshughulikia mambo hayo.

Kwamba, hakukuwa na lolote lililofanyika kukabiliana na hujuma dhidi ya nchi.

Hata mgombea wa CCM amesema atapambana na rushwa na kuziba mianya hiyo

Hii ina maana Magufuli ambaye ni waziri wa JK anajua rushwa ilivyotawala kwa miaka 10 ya utawala wa JK

Maswali ya kujiuliza, je wananchi watabadili misimamo yao kutokana na hotuba za jana

Kwa jicho pevu, hata pale walipoaminishwa Fulani ni jambazi, mwizi na mnayng'anyi, wananchi wameonekana kutojali
Kwa maneno mengi, wizi ujambazi na ufisadi ni dalili tu za maradhi, lakini maradhi ni serikali dhaifu iliyolea yote

JK anaposimama na kumnadi Mgombea wake, kwa kiasi Fulani ameamsha hisia badala ya kuzuia.

Watu hawajali tena kuhusu rushwa kwasababu ni mfumo rasmi wa CCM na JK katika miaka 10.

Kinachoonekana ni watu kuwa na upinzani tu kwavile wamechoka

Hotuba ya JK hatudhani kama itakuwa na manufaa kwa CCM kwasababu wengi walishaamua ima kuiunga mkono CCM au kuitosa.

Hatudhani wale waliosimama kumzomea Magufuli mbele ya FFU wanaweza kubadili msimamo wao usiku mmoja.

Na wale walioamini tu kuwa CCM ndio yenyewe wanaweza kubadili msimamo wao asubuhi hii

Hata hivyo, JK amemamliza muda wake akiacha legacy itakayomwandama kwa muda mrefu huko uraiani

Haya ya kusema hakujua Richmond wakati yeye ndiye mwenye dhamana yanaeleza mengi juu ya utawala wake ambayo pengine hatapenda kuyasikia lakini yatasemwa yataandikwa

Haya ya kuongelea afya za watu, nayo yataacha doa kubwa kwake siku za mbeleni.

Iwe iwavyo, JK amekiacha chama cha Mwalimu Nyerere katika hali mbaya sana.

Matokeo ya aina yoyote hayawezi kunasua na hilo. Bado CCM wanaamini chama kimedhoofika kama si kufikia mikononi mwa JK.

Jioni ya leo na kuendelea zitaeleza kwa undani kuhusu JK bila kuwa fursa ya kujitetea kama kiongozi wa nchi na mwenyekiti wa CCM.

Alichokifanya ni 'fungulia mbwa' kwamba ni haki na sawa kumjadili kama anavyojadili wenzake tena akijivua majukumu na mamlaka.

Tusemezane
 
Nguruvi, kutii sheria bila shuruti ni sehemu ya maendeleo na pia ni ustaarabu.

Siku ya leo kampeni haziruhusiwi.

Jenga nchi yako kwa kutii sheria bila shuruti...
 
Nguruvi, kutii sheria bila shuruti ni sehemu ya maendeleo na pia ni ustaarabu.

Siku ya leo kampeni haziruhusiwi.

Jenga nchi yako kwa kutii sheria bila shuruti...
Sijui kama kuna sharia inayozuia watu wasifanye tathmini kwa maono yao katika blogs, forums n.k.

Tunachofanya ni kile kile cha kila siku, taifa mbele. Tunakataa ubabaishaji , uongo na unafiki
 
Kiburi, jeuri, dharau, kujiamini
Katika masuala ya uongozi/utawala; hayo ni matokeo ya tabia ya mtu kupata nyadhifa bila kufuata taratibu. Kwenye siasa hayo ni matokeo ya tabia ya mtu kulazimisha ushindi wakati hakupigiwa kura tena akiwa na uhakika kuwa hakuna yeyote atakayemuadhibu kwa uporaji huo wa ushindi kutoka kwa mchaguliwa halisi wa wapiga kura. Hii ndiyo tafsiri yangu ya maneno hayo Mkuu.
 
Back
Top Bottom