2015: Tunahitaji Rais mwenye UWEZO! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2015: Tunahitaji Rais mwenye UWEZO!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 26, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Wazo la leo:

  Tanzania haiitaji Rais kijana... kwani tunapeleka Ikulu mbeba vyuma au mtunisha misuli au atakuwa na kazi ya kupiga push ups ofisini? Na hatuwezi kumkataa mtu kwa sababu ni mzee kwani anaenda kubebeshwa viroba vya mchele au kukimbia marathon?

  Tena hata hatuhitaji Rais msomi wa kivile! Mwaka 2015 Watanzania wanahitaji Rais ambaye atavunjilia mbali sera zilizoshindwa za CCM, kuifumua mifumo mibovu ya kiutawala iliyodumu kwa miaka karibu hamsini sasa na kutupa uongozi wa kutufanya tujiamini kuwa tunaweza na akatuongoza katika kujenga taifa la kisasa lenye kujali utu wa watu na siyo vitu vya watu.

  Tunahitaji rais na pamoja naye viongozi wenye UWEZO wa kufikiri kwa usahihi, kuamua kwa usahihi na kutenda kwa usahihi wakitambua dhamana ya uongozi ambao taifa linawapa. RAIS ajaye wa Tanzania ni lazima awe na UWEZO; UMRI wake usihusishwe kabisa na uwezo huo.

  Kiongozi ajaye basi ni lazima we ni MTU WA WATU; ambaye amejitofuatisha katika mambo makubwa yafuatayo: Wazo hili litaendelea...
   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  kamwe watanzania wa leo hawawezi ku risk eti kwa sababu tu ni mzalendo'kuna mambo mengi ya kuangalia'mimi nikiwa kama kiongozi wa kampuni nimeamua kumpa mtu mzima mwenye umri wa 55 awe CEO wa kampuni'vijana wengi waliomba lakinii tulifikia uamuzi baada ya kuelewa umuhimu wa umri na exprience na reason'zito kabwe hafai hata kuwa waziri mkuu'inawezekana akafaa kuwa waziri wa kawaidi chini ya uangalizi maalum'zito atatumika kuharibu upinzani'ni mnafiki halafu ni ndumilakuwili'wakati ccm inashambulia chama chake yeye amejitenga kana kwamba siyo kiongozi' namshauri ajiunge ccm wamsimamishe agombee huo urais wake
   
 3. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ofcourse! U're right.
   
 4. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ...Yaani haya yote ni kwa sababu tu kijana mwenye uwezo, Zitto, katangaza kuutaka urais 2015?mwisho wa siku Watanzania wataamua 2015 kama walivyoamua 1961, 1985,1995 na 2005...

  ...Filikunjombe alipozungumza na gazeti hili kuhusu halfa hiyo alihoji: “Kwani tatizo ni nini? Hapa kuna habari ndugu… kuwa sehemu ya Tanzania kwa nini Kigoma isitoe rais?” Zitto: Urais usitugombanishe

  ...Na mie niongeze tu, kwanini kijana mwenye uwezo asiwe Rais 2015?Yes He Can...
   
 5. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  Huyo ndiye Rais tunayemtaka
   
 6. c

  chama JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji
  Ahaa haa haa !Umeshakatiwa fungu nini? Naona kampeni zimeanza mapema; na mzee huyo mwenye uwezo lazima atoke Chadema au chama chochote kile? Wazee wapo wengi!

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 7. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mm 2po pamoja..hata kama ana miaka 80 na ana uwezo mbona shughuli inapigwa...
   
 8. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nadhani unahitaji kuisoma hiyo thread upya mkuu!
   
 9. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Uwezo wa mtu kuwa kiongozi hatuwezi kuupima kwa umri wake, kwa sababu sote tu mashahidi namna ambavyo wazee kwa vijana wameharibu nchi hii wakiwa viongozi...angalia umri wa wezi wa EPA na ufisadi mwingine, angalia umri wa akina Liyumba...angalia umri wa akina Maige...Ekelege...Masha...Mkulo...Chami...hawa wote ni hawafanani kwa umri, ni vijana kwa wazee, na wamepata nafasi za kuongoza na tunaweza kuwapima kwa walichokifanya wakiwa madarakani kuwa si kwa umri wao, bali uwezo wao.
   
 10. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 467
  Trophy Points: 180
  Hatuhitaji rais anayepambana na chama chake, asiye na mashirikiano wa viongozi wake, hatuhitaji rais asiyeshirikiana na kambi yake badala yake anashirikiana na mpinzani wa chama chake eti kwa kwa reason kwamba yeye ni mtu wa watu wote habagui chama.
  Hatuhitaji rais asiyetetea chama chake hasa katika kukijenga. Ni afadhali heche na LEMA WANAOKATA mbuga kila siku wakikijenga cham kuliko kiongozi anyeongoza kupitia mitandao na magazeti.shame on him
   
 11. c

  chama JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  "UMRI wake usihusishwe kabisa na uwezo huo."

  Kama huelewi kusoma riwaya nyamaza kimya

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 12. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Diector 1
  Thinking zako kwa zitto zinaonekana una chuki za kupindikua na zitto. Pendekeza hao waezee wako tuwaone kama hatutashuhudia ukimpendekeza EL. Acha uchonganishi.
   
 13. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tukianza ubaguzi dhidi kundi fulani mathalalni wazee, au vijana, watafuata wanawake, kisha tutabagua walemavu, halafu kanda, ukabila, dini, rangi, mwisho tutasema Rais lazima awe na kimo cha sm 200. Ni upuuzi mtupu kuangalia mtu anayefaa kuwa Rais kwa vigezo vya kibaguzi ktk nchi ambayo Nyerere alitujengea usawa kwa wote kwa miaka mingi. Wako wazee waliovuruga nchi zao na wako vijana waliovuruga nchi zao kama huyo wa Syria naye aliingia kama kijana. Kumbukeni mafanikio yaMzee wa miaka 74, king cobra wa Zambia.
   
 14. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mwl. Nyerere alishasema tumuogope sana mtu anataka kukimbilia IKULU, alisistiza Ikulu hakuna biashara, akasema
  tena tumuogope mtu huyo kama UKOMA, ZITTO ni UKOMA namuogopa....
   
 15. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 467
  Trophy Points: 180
  Charles Taylor ameingia akiwa kijana lakini nini alichokifanya.angalia leo mawaziri vijana hapa bongo akina Ngeleja, Nyarandu, chami na wengine.Ubaguzi hautakiwa mandela ametawala akiwa mzee lakini angalia mafanikio yake.Benjamini mkapa alikuwa tayari mzee.Japo Ben kosa lake ni sera ya ubinafsishaji lakini ni eneo moja tu alilochemsha.Angalia kijana wetu JK ni aibu kuendela kutaja.
  Tuna hitaji rais atayesema wazi kuchukia rushwa na aonekane kuichukia kwa matendo
   
 16. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kumbe humu anazungumziwa Zitto!!
   
 17. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Well said Mwanakijiji….lakini iwe ni rais kijana au mzee; mwenye busara au asiye na busara bado hawezi kukukabiliana na changamoto zxa msingi za taifa hili ikiwa bado atakuwa anaongozwa na Katiba inayosimamia utawala bora wa kimagharibi! Nchi yetu ina matatizo makubwa; yasiyoweza kunyanyulika kwa folk lift wala kwa winch! Kabla ya huyo rais ambae wewe na wengine wote tungependa tuwe nae kwanza anapaswa kupewa nyenzo itakayobeba matakataka makubwa kuliko yote yaliyopo nchini kwetu na kwenda kuyatupilia mbali…ikibidi hata bahari ya Pacific ili yasirejee tena nchini mwetu! Matakata haya, ni maadili mabovu ya Watanzania; ingawaje tunataka kuaminishana kwamba ni maadili mabovu ya Viongozi wa CCM! Nyenzo pekee anayopaswa kupewa rais huyo chaguo la wote ni Katiba ya Kidikteta…..Sio Kiongozi wa Kidikteta; bali ni Katiba ya Kidikteta itayaoondowa makandokando yote yaliyogubika mioyo hasidi ya Watanzania walio wengi!

  Vyovyote iwavyo, hata kama Rais ajae atoke mbinguni, bado hawezi kuondoa makandokando hayo chini ya katiba inayohubiri Utawala Bora; Utawala Bora wa Kimagharibi! Mfumo ambao, moja ya nguzo zake kuu ni Utawala wa Sheria!! Mfumo ambao unatuambia kwamba mtu atabaki kuwa mtuhumiwa hadi pale itakapothibitika; beyond reasonable doubt kwamba kosa analotuhumiwa nalo kwamba ni kweli amefanya!! Kwamba; leo hii ingawaje William Mhando anatuhumiwa kufanya ufisadi TANESCO lakini bado huwezi kuwa na grounds za kumpeleka korokoroni na kumtupa jela….huwezi kufanya hivyo kwa kuwa huna ushahidi; huo ndio Utawala wa Sheria; moja ya nguzo muhimu kabisa za Utawala Bora!!! Wengine nao wanadai Maswi (Katibu Mkuu wa Nishati) ndie fisadi na ananufaika na Puma Energy….huyo nae, huwezi kumpeleka mahakamani kwavile hakuna ushahidi…na hata ukimpeleka bado atashinda kesi; huo ndio Utawala wa Sheria, ambao ndio msingi mkuu wa Utawala Bora!

  Hivyo basi, tatizo sio ni rais wa aina gani, bali ni katiba ya aina gani !! Tunahitaji kwanza katiba ya kidikteta itakayo-shape maadili ya Watanzania!Tunahitaji Katiba ya Kidikteta ambayo itamafanya rais yeyote ajae 2015 kufanya si kwa kutaka bali kwa kulazimishwa na Katiba Ya Kidikteta!! Katiba ambayo, itatamka wazi, ile kutuhumiwa peke yake inatosha kabisa kumpeleka mahakamani mtuhumiwa na badala ya kutaka upande wa mashitaka ndio uthibitishe beyond reasonable doubt tuhuma dhidi ya mtuhumiwa; basi ni mtuhumiwa ndie athibitishe beyond reasonable doubt kwamba tuhuma dhidi yake si sahihi…tuhuma ninazozungumza hapa ni zile ambazo ndizo kansa kuu ya nvchi hii; TUHUMA ZA UFISADI!! Katiba ya Kidikteta ambayo pia itatamka wazi kwamba; kumzushia mtu tuhuma ambazo si za kweli; hiyo nayo ni serious crime ili kuzuia watu kuwazushia wenzao kwavile tu wanafahamu wazi kwamba Katiba Yetu Mujarabu Ya Kidikteta itamwajibisha yule anayemzushia!

  Anyway, nazani hili linahitaji thread inayojitegemea lakini nihitimishe tu kwamba kwa katiba yoyote itakayoendeleza Mfumo wa Utawala Bora ambao moja ya nguzo zake kuu ni Utawala wa Sheria basi haitakuwa na msaada wenye tija kwa rais awaye yote labda tu aamue kuvunja misingi ya katiba inayohubiri utawala bora!
   
 18. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,705
  Likes Received: 322
  Trophy Points: 180
  Tunahitaji kuwa na raisi anayeweza kutimiza Country strategic Plan. Bila kuwa na dira na taasisi kamili hata tupate raisi mwenye akili kama nani hatuwezi endelea. Ma Great thinker tuanzishe mjadala wa '' NATIONAL STRATEGIC PLATFORM''
   
 19. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Utanisamehe mkuu, sikujua kama mleta uzi kama alitarajia audience ya "wasomaji wa riwaya" pekee!
  Ila naomba kuchangia tu kidogo kwenye ulichoandika kisha ntawaachia nyie 'wataalamu wa usomaji riwaya' kuchangia zaidi.

  Anyways,Kwa hiyo kwako wewe 'msomaji wa riwaya' hapo kwenye bluu maana yake ni 'Rais mzee' au?!
  Hebu jaribu kwenda kinyume cha unavyotafsiri uone kama itakataa!!

  Halafu unajua mkuu, uwezo wa kutafsiri maana ya ndani katika habari ni "subjective" sio "objective"
  ila kwa kuwa Mwanakijiji yupo humu ni vema ukamuuliza, bila kujaribu kulazimisha maana yako ambayo
  kwa vyovyote vile inaendana na uelewa wako, na kama ujuavyo uelewa wetu ni tofauti, tena tofauti sana.

  Kwangu mimi naona kaongelea Uwezo bila kujali Umri, sasa kwa kuwa nyie 'wataalamu wa kusoma riwaya' huwa mnatengeneza 'picha' zenu 'akilini' kutokana na 'utunzi' husika, mnaruhusiwa kuona vinginevyo!
   
 20. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,195
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe Mkuu kwani Kipindi cha Mwinyi alishawahi kuwa na Mshauri aliyebobea kwenye mambo ya Uchumi nafikiri uliona alipotufikisha
   
Loading...