2015: Tunahitaji Rais mwenye UWEZO!

Rais awe kijana.Wazee wengi wa Tanzania wana mawazo mgando.
Kwa mfano, umoja/baraza la vijana, wanawake, wazazi ... haya yote ni mawazo ya nani? Nani aliamua miundo hii ya vyama?
So, obsolete!!! kila chama kinafuata miundo ya kizamani sana.
UKITAKA KUFANYA KITU UNAAMBIWA WAZEE WA CHAMA WAMEKATAA.
Ni wakati muafaka wazee wakae pembeni, hakuna mzee mwanasiasa mwenye jambo jipya, wote walikuwa kwenye system na wameshaharibu. Wakae pembeni.
 
Siyo vijana tu wanaonyanyua vyuma. Tembeleeni gym halafu muingie weight room muone jinsi kulivyo na mchanganyiko wa ma rika tofauti.

Hata vibibi vinabeba vyuma. Vibabu ndo usipime kabisa.
 
Rais awe kijana.Wazee wengi wa Tanzania wana mawazo mgando.
Kwa mfano, umoja/baraza la vijana, wanawake, wazazi ... haya yote ni mawazo ya nani? Nani aliamua miundo hii ya vyama?
So, obsolete!!! kila chama kinafuata miundo ya kizamani sana.
UKITAKA KUFANYA KITU UNAAMBIWA WAZEE WA CHAMA WAMEKATAA.
Ni wakati muafaka wazee wakae pembeni, hakuna mzee mwanasiasa mwenye jambo jipya, wote walikuwa kwenye system na wameshaharibu. Wakae pembeni.

Nani huyo kijana unayetaka awe rais?
 
Mimi naamini hata umri wa kikomo ni muhimu, kuna mahali nilisikia mwalimu wakati anang'atuka watu walishaanza kumuita hambiliki (hashauriki) na alikuwa mkali kwa kuitwa jina hili.

Unafikiri alikuwa anaitwa "haambiliki" kwa sababu ya uzee? Unajua Nyerere aliacha Urais akiwa na miaka mingapi? Kukupa taarifa tu alikuwa na miaka 63. Michael Sata wa Zambia ana miaka 74, Mwai Kibaki 80, Truman alipoapishwa alikuwa 60 na Regan 69!!! think about it.. Rais kijana Marekani kuapishwa alikuwa ni T. Roosevelt akiwa na miaka 42 na mzee zaidi akiwa ni Regan! Marekani kwa miaka yote na marais 44 imewahi kuwa na marais 2 waliokuwa chini ya miaka 45!! And its doing just fine.
 
Rais awe kijana.Wazee wengi wa Tanzania wana mawazo mgando.
Kwa mfano, umoja/baraza la vijana, wanawake, wazazi ... haya yote ni mawazo ya nani? Nani aliamua miundo hii ya vyama?
So, obsolete!!! kila chama kinafuata miundo ya kizamani sana.
UKITAKA KUFANYA KITU UNAAMBIWA WAZEE WA CHAMA WAMEKATAA.
Ni wakati muafaka wazee wakae pembeni, hakuna mzee mwanasiasa mwenye jambo jipya, wote walikuwa kwenye system na wameshaharibu. Wakae pembeni.

Unafikiri hawa wazee waliibuka tu wakiwa na mvi? unawaona wazee waliingia na kupewa nafasi mbalimbali wakiwa vijana!! Wote unaowaita wazee leo ukirudi kati ya 1964-1972 walipoingizwa kwenye utumishi wa umma wengi walikuwa ndio "vijana" wa wakati huo!!! Kwanini unafikiri vijana wa "sasa" watakuwa na tofauti?
 
Mwanakijiji,

Je ni kwa vile tu kijana wa Kigoma inaonekana ameamua na katangaza nia "mapema"?
 
Utanisamehe mkuu, sikujua kama mleta uzi kama alitarajia audience ya "wasomaji wa riwaya" pekee!
Ila naomba kuchangia tu kidogo kwenye ulichoandika kisha ntawaachia nyie 'wataalamu wa usomaji riwaya' kuchangia zaidi.

Anyways,Kwa hiyo kwako wewe 'msomaji wa riwaya' hapo kwenye bluu maana yake ni 'Rais mzee' au?!
Hebu jaribu kwenda kinyume cha unavyotafsiri uone kama itakataa!!

Halafu unajua mkuu, uwezo wa kutafsiri maana ya ndani katika habari ni "subjective" sio "objective"
ila kwa kuwa Mwanakijiji yupo humu ni vema ukamuuliza, bila kujaribu kulazimisha maana yako ambayo
kwa vyovyote vile inaendana na uelewa wako, na kama ujuavyo uelewa wetu ni tofauti, tena tofauti sana.

Kwangu mimi naona kaongelea Uwezo bila kujali Umri, sasa kwa kuwa nyie 'wataalamu wa kusoma riwaya' huwa mnatengeneza 'picha' zenu 'akilini' kutokana na 'utunzi' husika, mnaruhusiwa kuona vinginevyo!

Mimi nakubaliana kabisa na unachosema ila mwanakijiji hamaniishi hivyo, yupo kwenye kampeni! soma maneno ya mwanakijiji hapa nanukuu "Unafikiri alikuwa anaitwa "haambiliki" kwa sababu ya uzee? Unajua Nyerere aliacha Urais akiwa na miaka mingapi? Kukupa taarifa tu alikuwa na miaka 63. Michael Sata wa Zambia ana miaka 74, Mwai Kibaki 80, Truman alipoapishwa alikuwa 60 na Regan 69!!! think about it.. Rais kijana Marekani kuapishwa alikuwa ni T. Roosevelt akiwa na miaka 42 na mzee zaidi akiwa ni Regan! Marekani kwa miaka yote na marais 44 imewahi kuwa na marais 2 waliokuwa chini ya miaka 45!! And its doing just fine."

Chama

Gongo la mboto DSM
 
"Ujana" si tija. Umri ni kwa ajili ya eligibility tu. Hauhuusiani na uwezo wa uongozi. Hata mtu wa miaka 70 anaweza kuwa na u wezo mkubwa wa kufanya kazi ambazo zinahitaji akili zaidi kuliko mtu wa miaka 40. Lakini kama ana miaka 70 na bado ana nguvu za mwili kwanini asipewe nafasi hiyo? Wengi wetu baba zetu ndio wamefika miaka 70 hivi unafikiri kweli tunaweza kusema hawafai kufanya kazi yoyote inayohitaji hekima na uwezo wao wa kiakili?

Ninachojengea hoja hapa ni kuweka suala la umri kwenye context sahihi. Haiwezekani mtu aseme "tunahitaji viongozi vijana" au "sasa ni zamu ya vijana" halafu watu wakashangilia? Kwanini tunataka viongozi wanyanyua vyuma ili vijana washinde kirahisi?

Mkuu Chama, nadhani umeona alivyoelezea alichomaanisha hapa. Na ndio maana jana nikaomba umuulize akueleweshe.

Mimi nakubaliana kabisa na unachosema ila mwanakijiji hamaniishi hivyo, yupo kwenye kampeni! soma maneno ya mwanakijiji hapa nanukuu "Unafikiri alikuwa anaitwa "haambiliki" kwa sababu ya uzee? Unajua Nyerere aliacha Urais akiwa na miaka mingapi? Kukupa taarifa tu alikuwa na miaka 63. Michael Sata wa Zambia ana miaka 74, Mwai Kibaki 80, Truman alipoapishwa alikuwa 60 na Regan 69!!! think about it.. Rais kijana Marekani kuapishwa alikuwa ni T. Roosevelt akiwa na miaka 42 na mzee zaidi akiwa ni Regan! Marekani kwa miaka yote na marais 44 imewahi kuwa na marais 2 waliokuwa chini ya miaka 45!! And its doing just fine."

Chama

Gongo la mboto DSM

Nukuu ya Mwanakijiji hapo juu inapingana na hicho ulichosema kwenye wekundu.
Binafsi sioni kama kuna kampeni yeyote hapo.

Labda unieleweshe vizuri.
 
Bob Lee Swagger;
Jifunze kusoma riwaya ndipo utaelewa maandiko ya mwanakijiji; mbona haji yeye mwenyewe kukanusha?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Bob Lee Swagger;
Jifunze kusoma riwaya ndipo utaelewa maandiko ya mwanakijiji; mbona haji yeye mwenyewe kukanusha?

Chama
Gongo la mboto DSM

hahahaha hahahahah umenifurahisha mkuu.
Asante sana, ninachukua ushauri wako.
 
Wazo la leo: Tanzania haiitaji Rais kijana... kwani tunapeleka Ikulu mbeba vyuma au mtunisha misuli au atakuwa na kazi ya kupiga push ups ofisini? Na hatuwezi kumkataa mtu kwa sababu ni mzee kwani anaenda kubebeshwa viroba vya mchele au kukimbia marathon? Tena hata hatuhitaji Rais msomi wa kivile! Mwaka 2015 Watanzania wanahitaji Rais ambaye atavunjilia mbali sera zilizoshindwa za CCM, kuifumua mifumo mibovu ya kiutawala iliyodumu kwa miaka karibu hamsini sasa na kutupa uongozi wa kutufanya tujiamini kuwa tunaweza na akatuongoza katika kujenga taifa la kisasa lenye kujali utu wa watu na siyo vitu vya watu.

Tunahitaji rais na pamoja naye viongozi wenye UWEZO wa kufikiri kwa usahihi, kuamua kwa usahihi na kutenda kwa usahihi wakitambua dhamana ya uongozi ambao taifa linawapa. RAIS ajaye wa Tanzania ni lazima awe na UWEZO; UMRI wake usihusishwe kabisa na uwezo huo.

Kiongozi ajaye basi ni lazima we ni MTU WA WATU; ambaye amejitofuatisha katika mambo makubwa yafuatayo: Wazo hili litaendelea...

FACEBOOK YANGU

Huo uwezo tutaupimaje, kwa maneno jukwaani au kwa rekodi ya mtu kiutendaji? Kumbuka hata JK tulimjaribu bila rekodi yoyote na matokeo yake tumeyaona.

Mzee mwenzangu, nina wasiwasi unampigia ndogo ndogo EL kiaina?
 
hahahaha hahahahah umenifurahisha mkuu.
Asante sana, ninachukua ushauri wako.

Bob Lee Swagger
Mimi nakubaliana na wewe 100%; uliachoandika kipo wazi na hakina mjadala ila mwanakijiji ameandika riwaya na ndio sababu hawezi kukanusha

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Unafikiri alikuwa anaitwa "haambiliki" kwa sababu ya uzee? Unajua Nyerere aliacha Urais akiwa na miaka mingapi? Kukupa taarifa tu alikuwa na miaka 63. Michael Sata wa Zambia ana miaka 74, Mwai Kibaki 80, Truman alipoapishwa alikuwa 60 na Regan 69!!! think about it.. Rais kijana Marekani kuapishwa alikuwa ni T. Roosevelt akiwa na miaka 42 na mzee zaidi akiwa ni Regan! Marekani kwa miaka yote na marais 44 imewahi kuwa na marais 2 waliokuwa chini ya miaka 45!! And its doing just fine.

Umri wa watu wa kizazi cha Nyerere ni vigumu sana kuutaja kwa uhakika, wengi wao walikuwa wanakadiria tu, kama baba/ mama yangu aliniambia nilizaliwa wakati mjerumani anajenga reli ya kati imefika hapa zuzu. Au wakati wa mafuriko fulani au njaa fulani iliyoweka record zama hizo. Anyway tukiachana na hilo mbona awali watu walimpa Mwl majina kama musa, mchonga n.k lakini mwisho wa siku akaishia kuitwa haambiliki na kwa maneno yake mwenyewe haya majina mengine aliyakubali tena kwa kutoa sababu za kuyakubali. Lakini hili la haambiliki hili akasema nitamfunga mtu. So ubishi na kutokushaurika vilikuwa ni sifa za Nyerere alipo fikia umri wa uzeeni. Narudi palepale, kama kilivyo kigezo cha umri wa ruksa ya mwanzo wa kugombea lazima na umri wa ukomo wa kugombea urais wa tz uweke kikatiba.Kama sisi ni taifa la watu makini.

Naona umetoa mifano ya umri wa marais wa usa, zambia, kenya, mimi sioni tatizo kama tutaweka kigezo cha ukomo wa umri wa kugombea halfu hawa nao wakaja kujifunza kwetu, tunatakiwa kujiami tu imekuwa ni kasumba sasa kuwa kila jambo lazima kwanza tuangalie wazungu wamefanya nini tunaiga hata yanayohitaji kutumia busra zetu, tena busara kidogo tu.
 
Nimeipenda sana hii hoja, kikubwa ni uwezo!. Endeleeni kuweka vigezo tena with elimination strategies, at the end of the day, tutarudi kule kule kwa the "good ones" who are capable, piga ua galagaza, mwisho wa siku tutagota mule mule!.

Huwezi kuzuia upepo!. Mgombea wetu ni magma ya moto, saa hizi imeanza kutokota kidogo tuu, watu wanaweweseka!, jee itakapo chemka ni nini kitafuatia... ni eruption tuu!, nothing more, nothing less!, 2015 rais wa ukweli tunae na ni ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

Tumechoka na wagombea urais wa mazoea na ahadi, sasa tunataka mgombea sio tuu mwenye uwezo, bali pia mwenye mission na vision anataka kulitoa taifa letu hapa lilipo, atatupeleka wapi na strategies za kuimplement hiyo mission ili kuifikia hiyo vision in reality na sio ahadi hewa!. Mtu wa namna hii tunaye its only the matter of time!.

Afande hapo bolded and red, mbona hizo ukitaka kama vigezo utapewa sana tu, tena wasanii na matapele wa kisiasa ndio watakumaliza nazo kabisa tatizo la watz ni kuwa wasahaulifu sana si juzi tu hapa tulizisikia vision na mission tena kwa mbwembwe zote kiko wapi sasa?
 
Unafikiri hawa wazee waliibuka tu wakiwa na mvi? unawaona wazee waliingia na kupewa nafasi mbalimbali wakiwa vijana!! Wote unaowaita wazee leo ukirudi kati ya 1964-1972 walipoingizwa kwenye utumishi wa umma wengi walikuwa ndio "vijana" wa wakati huo!!! Kwanini unafikiri vijana wa "sasa" watakuwa na tofauti?
Easy,
Mazingira waliyokulia wazee wetu si sawa na mazingira waliyokulia vijana wa sasa hivi.
 
Ndugu zangu watanzania, hii tabia ya kuchagua watu ili mradi tu kujaza nafasi tuhakikishe haijirudii tena 2015. Hivi kweli watanzania tutaendelea kuishi kwa ahadi hewa za "maisha bora kwa kila mtanzania" huku rasrimali zetu zikiporwa na wageni hadi lini? huu wimbo wa nchi yetu ni changa na masikini unachusha! Miaka 50 ya uhuru tuliyosherehekea kwa kuonyeshana zana hafifu za kivita ambazo hatujatengeneza wenyewe huku viongozi wakizuga kwamba wanajipanga, wanajifunza na bado wako kwenye mchakato isiyoisha! Tusifanye tena mzaha 2015.
 
Hii ni kazi yetu wote. Anzia pale ulipo kumwaga elimu ya uraia, umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura. LAKINI UJUE CHAMA CHA MABWE NI JANGA LA TAIFA. Kwa pamoja tutafika.
 
Back
Top Bottom