Jambo linalonishangaza ni kwamba more than 70 ya population ya Tanzania walizaliwa baada ya uhuru, wamezaliwa na kukulia kwenye mazingira ambayo (naamini) udini, ukabila, umri havikuwa issue hasa kwenye siasa. Sasa haya maneno ya u-mkoa, ukabila, udini wametoa wapi? Na kwanini? Tanzania tunakwenda mbele au tunarudi nyuma?Nitegemea hao wanaobudu siasa za ujana wawe wanahubiri kuhusu kutengeneza rocket, kujenga our own silicon Valley, lakini day in day out we are being subjected to this medieval politics! Inaudhi.
Ahsante kwa hoja zako nzuri. Tatizo lililopo limeanzishwa na wanasiasa na viongozi wa dini.
Hawa wametumia udhaifu wa kuelewa wa asilimia 70 kupenyeza udini na ukabila. Lakini isingekuwa tatizo kama kungekuwa na busara kwa wale waliopewa dhamana.Udini na ukabila vilikuwepo hata zamani,uzuri ni kwamba kila vilipojitokeza vilikemewa sana na kwa nguvu zote. Siku hizi mamlaka zote zinaogopa kukemea! sababu ni kuwa viongozi waliopo hawakuingia madarakani kwa hoja bali ulaghai huo huo wa ukabila na udini.
Tuna makundi matatu ya wananchi, la kwanza ni la wale wanaoelewa na kujielewa.
Kundi la pili ni wale waisoelewa lakini wanategeme busara zao.
Kundi kubwa ni hili lililopo la asilimia 70 ambalo wengi wamepikwa wakaiva nusu'half baked'. Hawa wanajua kusoma kwahiyo wanaweza kukupa majina ya viongozi na dini zao tena kwa takwimu hafifu za asilimia 60 ni viongozi wa kabila au dini fulani hata kama viongozi hao ni 5. Simple statistic hakuna analysis wala kuliangalia jambo kwa wider prism.
Hili ndilo kundi hatari sana kwasababu halijui lakini linadhani linajua. Wasi wasi wangu ni kuwa kila kukicha hili kundi la nusu nusu linazidi kuongezeka na linatumika sana na wanasiasa na viongozi wa dini
Kuhusu hoja ya ujana vs uzee,hapa tunapotoka sana. Urais ni taasisi siyo mtu mmoja kama ilivyo kwa viongozi wa kada nyingine.
Manager mzuri ni yule mwenye timu nzuri, na timu nzuri inapatikana kwa busara za manager mzuri.
Mfano, Tonny Blair alikuwa PM akiwa na iaka 45, pengine yeye ndiye alikuwa na elimu ndogo umri mkubwa au mdogo katika timu yake. Kilichomsaidia ni weledi, hekima na busara za ku-organize resorce alizonazo.
Ronald Reagan alikuwa Rais akiwa na umri mkubwa sana. Ni mmoja wa marais wa Marekani wanaotajwa kuwa bora. Kilichomsaidia ni hekima, busara na maono yake katika kutengeneza timu ya uongozi na ku-organize resource alizokuwa nazo
Kiongozi tunayemuhitaji si yule maarufu, msemaji au mwenye umri na jinsia fulani.
Tunahitaji mtu atakaye organize resource zilizopo kututoa point A kwenda B.
Tunahitaji mtu mwenye weledi, busara, hekima na maono(vision).
Mtu mwenye uthubutu wa kufikiri na kutenda, kusikiliza na kusikilizwa, atakayetuunganisha na kusimamia thamani zetu kama taifa. Kiongozi tunayemuhitaji ni yule anayeweza kusimama na kutetea anachokiamini ni sahihi kwa jamii hata kama kufanya hivyo ataudhi watu, lakini pia ni mtu anayeijua jamii anayoiongoza na dunia kwa ujumla.
Ujana au Uzee hautusaidii katika nyakati tulizonazo.