Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,335
- 9,756
Ndugu zangu Watanzania,
Urais ni nafasi nyeti na kipekee sana, ni nafasi inayohitaji mtu mwenye akili kubwa ya kuweza kujuwa, kufahamu na kutambua namna ya kutumia akili kubwa zote nchini katika kuleta matokeo chanya katika maisha ya watu.
Ni nafasi inayohitaji mtu mwenye upeo mkubwa na maono ya mbali, ni nafasi inayohitaji mtu anayeweza kuona umbali wa miaka mia mbele na kuwa na mipango ya karne moja mbele, ni nafasi inayohitaji mtu mtulivu wa akili na mipango au maamuzi yake.
Ni nafasi inayohitaji mtu jasiri katika kufanya maamuzi kwa wakati bila hofu wala uoga, ni nafasi inayohitaji mtu mwenye hekima, busara na mwenye kuchunga ulimi wake.
Urais unahitaji mtu mwenye uwezo wa kuwaunganisha watu wa makundi yote, vyama vyote, rika zote na Dini zote, mtu mwenye uwezo wa kuvumilia na kuweza kukaa meza moja na mpinzani wake, mtu mwenye uwezo wa kusikiliza na kuthamini sauti zote, mtu mwenye uwezo wa kutoa haki kwa wengi na kuwasikiliza wachache.
Ndio maana mtu anaweza kuongoza vizuri wizara lakini akawa hana sifa hata kidogo ya kupewa Urais wa nchi kwa kuwa Urais unahitaji mtu mwenye akili, uwezo na macho ya kuzitazama wizara zote kwa usawa, inahitaji mtu ambaye makundi yote, Taasisi zote kuanzia viongozi wa Dini, wananchi, wanasiasa, vyombo vya ulinzi na usalama, n.k watajiona wana nafasi sawa na muhimu katika uongozi wako, watajiona hawatengwi na wana fursa sawa katika Taifa lao.
Urais unahitaji mtu anayejuwa kuwa akishapita anakuwa Rais wa wote kwa walio mchagua na ambao hawajamchagua, kwa wanao mpenda na wasio mpenda kwa maslahi yao, unahitaji mtu mwenye kifua kikubwa, mwenye kujua uongozi ni Jalala ambapo kila kitu utatupiwa wewe.
Unahitaji mtu shupavu, jasiri na madhubuti katika kukabiliana na mishale kutoka kila upande na kuweza kuhimili vishindo vyake na kubaki katika muelekeo wake na Dira yake pasipo kuyumba wala kuyumbishwa.
Urais hauhitaji mtu wa Hasira au visasi au chuki juu ya Wale waliokuwa wana mpinga kabla au waliomuumiza kabla, unahitaji mtu mwenye moyo wa kuachilia na kusamehe, unahitaji kujuwa nguvu yake ni kubwa kikatiba na kisheria inayohitaji busara katika kuitumia kwa watu. Inahitaji mtu mwenye hofu ya Mungu ili asitese watu hovyo, kuua watu hovyo, kuumiza watu hovyo na kububujisha watu machozi.
Sasa ukiangalia CHADEMA haina mtu mwenye sifa hizo, haina mtu mwenye uwezo wa kuwaunganisha Watanzania wa makundi yote na vyama vyote, haina mtu ambaye anaweza kutumainiwa na kutazamwa na watanzania kama mtu anayeweza akawahakikishia usalama na kuwatumikia pasipo visasi au chuki dhidi ya chama kingine au anayeweza kuwapa fursa sawa masikioni pake, CHADEMA haina mtu anayeweza akaviongoza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kama Amiri jeshi mkuu.
Haina mtu anayeweza akatazamwa na watu wa Dini zote na makabila yote na makundi yote kama kiongozi wao na wakawa huru kuonana naye na kufanya naye mazungumzo, CHADEMA haina mtu anayeweza akawafanya watu wa makundi yote wakajiona kuwa wana nafasi sawa katika utawala wake.
CHADEMA haina mtu mwenye ulimi wa kujenga umoja wa Kitaifa na hili linathibitishwa kupitia majukwaa yao kwa namna wanavyotoa lugha za ubaguzi na uchochezi na chuki dhidi ya wale wote wanaokuwa kinyume nao au kutowaunga mkono kama walivyofanya kwa walimu, police N.k.
Ukija kwa Upande wa Rais samia unaona ni mtu na nusu,ni kiongozi aliye kamilika, ni kiongozi mwenye kipawa na Karama ya uongozi ,ni kiongozi mwenye upeo, maono na akili kubwa, ni kiongozi mwenye kifua, uvumilivu na utulivu wa hali ya juu sana, ni kiongozi mwenye ulimi wa kulinganisha Taifa na uliojenga umoja wa kitaifa.
Ni kiongozi ambaye makundi yote ndani ya Taifa letu yanajiona yana nafasi sawa na fursa sawa katika uongozi wake, ni kiongozi mwenye uwezo wa kusikiliza sauti zote masikioni mwake, pamoja na kuweza kukaa mezani na yeyote katika kutafuta suluhu, lakini pia ni kiongozi mwenye kifua kikubwa na chenye kuhimili vishindo pasipo kupoteza Dira au kupandwa na jazba.
Hii ndio maana kwa uwezo wake huo wa kiuongozi tangia Ameingia madarakani amerudisha utaratibu wa mikutano ya kisiasa ili watu wazungumze ya moyoni, japo sasa watu Hasa CHADEMA wanatumia uhuru huo kutukana matusi na kupandikiza mbegu za ubaguzi kwa misingi ya Udini , ukabila, ukanda na jinsia.
Amekaa na makundi na viongozi mbalimbali katika kujadili Masuala mbalimbali katika ustawi wa Taifa letu, amekaa na viongozi wa Dini,wa vyama na hata kwa mtu mmoja mmoja. Ni Rais anaye mtizama kila mtu kwa jicho la usawa na haki.
Hii ndio maana Rais Samia Anaendelea kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania, hii ndio sababu ya upinzani kutokuwa na mtu wa kuweza kumshindanisha na Rais samia, hii ndio sababu kwa sasa upinzani umeishiwa hoja na kuishia kutoa Viroja na vihoja tu majukwaani kwa kuwa hoja za msingi zimefanyiwa kazi na serikali ya Rais Samia.
Ni busara kwa CHADEMA kuachana na wazo la kusimamisha mgombea Urais uchaguzi ujao ili kujiepusha kupoteza fedha zinazoweza kuwasaidia hata kujenga ofisi zao za chama au kufungua hata kituo cha TV kwa ajili ya kurusha matukio yao katika kuwafikia watu wengi sana kama ilivyo kwa chama makini cha CCM.
Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.