17 wajeruhiwa katika shambulizi la hospitali ya kujifungua Ukraine - maafisa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
1646911996476.png

Takriban watu 17 wamejeruhiwa na shambulizi la angani la Urusi kwenye hospitali ya Mariupol, kulingana na utawala wa kijeshi wa Ukraine katika eneo la mashariki la Donetsk.

Wafanyikazi na wanawake walio katika harakati za kijifungua walikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa, maafisa walisema.

Pavlo Kyrylenko, mkuu wa utawala wa kijeshi wa Ukraine katika eneo la Donetsk, alisema idadi ya watoto waliojeruhiwa "ni sifuri, namshukuru Mungu, na ninatumai itasalia kuwa hivyo".

BBC Swahili
 
Russia baada ya kuona mambo hayaendi kama walivyokuwa wakifikiria hapo awali matokeo yake wamekuwa desperate hadi sasa wanaua hadi mbwa na paka wanaokutana nao nchini Ukraine.

Wamebanwa sana kwenye vita vya ardhini na sasa wanatumia zaidi makombora ya masafa marefu kuua watu na kuharibu miundombinu.

Nasikia kwamba wamewarejesha nyumbani wale vijana wa JKT kufuatia malalamiko ya wananchi na pia ukweli kwamba hao vijana ndio wamekufa wengi baada ya kuwekwa mstari wa mbele wa mapigano.
 
Mnamo tarehe 7/03/2022, Majeshi ya Urusi yaligundua kuwa majeshi ya Ukraine yameibadilishia matumishi iliyokuwa hospitali ya wajawazito na watoto na kuifanya maficho ya wanajeshi wa Ukraine ambapo walikuwa wanashambulia kutokea hapo.

Tangu siku hiyo Urusi ilitoa onyo kuwa hospitali hiyo isitumiwe na majeshi ya Ukraine vinginevyo ingeshambuliwa. Ukraine waliendelea kuitumia hospotali hiyo kijeshi na kutokea humo kuendeshaashambulizi.

Kilichowatokea kila mmoja amekisikia na kelele ni kila kona!! Hizi picha wanazoonesha za watoto na wajawazito wakiwa majeruhi zilikuwa zimeandaliwa kabla!

Propaganda Kali inaendeshwa ili tu kuonesha Urusi inafanya unyama!
 
Mnamo tarehe 7/03/2022, Majeshi ya Urusi yaligundua kuwa majeshi ya Ukraine yameibadilishia matumishi iliyokuwa hospitali ya wajawazito na watoto na kuifanya maficho...
Ambaye hajui historia ya Russians wakiwa vitani ndio anaweza akapinga madai hayo. Nikikumbuka vile vita vya warusi kule Chechnya katikati ya miaka ya tisini na Georgia mwaka 2008 siwezi kupinga warusi ni jamii ya watu makatili sana.
 
Takriban watu 17 wamejeruhiwa na shambulizi la angani la Urusi kwenye hospitali ya Mariupol, kulingana na utawala wa kijeshi wa Ukraine katika eneo la mashariki la Donetsk...
Wajawazito na watoto waliondolewa hospotalini hapo na hospitali hiyo ikawa kama maficho ya wanajeshi was Ukraine na kwa kustukiza kutokea hapo.

Tarehe 07/03/2022, urusi iligundua hilo na kuonya, lakini hawakusikia matokeo yake moto umewawakia!! Hizo picha zinazooneshwa ni usanii na ziliandaliwa kabla!!
 
Ambaye hajui historia ya Russians wakiwa vitani ndio anaweza akapinga madai hayo. Nikikumbuka vile vita vya warusi kule Chechnya katikati ya miaka ya tisini na Georgia mwaka 2008 siwezi kupinga warusi ni jamii ya watu makatili sana.
Hivi ulilisikia onyo la urusi alilotoa tarehe 7 mwezi huu au unafuatilia habari za upande mmoja?

Ni kawaida kwenye vita upande ulioelemewa kujificha kwenye nyumba za raia na kuendesha mapambao.

Kuhusu ukatili hakuna taifa katili kama marekani kwenye historian ya dunia. Unajua alichokifanya hukoHiroshima Japan baada ya kuona mjapan anaendelea kuwanyanyasa kivita na hana mpango was kusarenda?

Aliipiga Japan kwa Bomu LA nyuklia! Malaki ya watu walikufa hapo hapo na wanyama na mimea na wadudu na kila kilicho hai kwenye eneo linalozunguka Hiroshima! Hakuna ukatili mkubwa kuliko huu!!
 
Wajawazito na watoto waliondolewa hospotalini hapo na hospitali hiyo ikawa kama maficho ya wanajeshi was Ukraine na kwa kustukiza kutokea hapo. Tarehe 17/03/2022, urusi iligundua hilo na kuonya, lakini hawakusikia matokeo yake moto umewawakia!! Hizo picha zinazooneshwa ni usanii na ziliandaliwa kabla!!
7/3/2022
 
Ambaye hajui historia ya Russians wakiwa vitani ndio anaweza akapinga madai hayo. Nikikumbuka vile vita vya warusi kule Chechnya katikati ya miaka ya tisini na Georgia mwaka 2008 siwezi kupinga warusi ni jamii ya watu makatili sana.
Wewe uliona wapi askari aliye vitani asiwe mkatili? Kwa waliopita depo watanielewa.
Jeshi maana yake ufe wew au afe adui? Kutakuwa na kuchekeana hapo mtu unaona kifo mbele yako?
Mkiambiwa ombeeni amani ya Tanzania, ombeeni vizuri.
 
Russia baada ya kuona mambo hayaendi kama walivyokuwa wakifikiria hapo awali matokeo yake wamekuwa desperate hadi sasa wanaua hadi mbwa na paka wanaokutana nao nchini Ukraine.

Wamebanwa sana kwenye vita vya ardhini na sasa wanatumia zaidi makombora ya masafa marefu kuua watu na kuharibu miundombinu.

Nasikia kwamba wamewarejesha nyumbani wale vijana wa JKT kufuatia malalamiko ya wananchi na pia ukweli kwamba hao vijana ndio wamekufa wengi baada ya kuwekwa mstari wa mbele wa mapigano.
Kila nikikumbuka zile tambo za hapa JF kwa ule uzi wa LIVE za Pro Russia na hali halisi ilivyo sasa nabaki kujisemea siku zote tuwe na akiba ya maneno.
 
Mnamo tarehe 7/03/2022, Majeshi ya Urusi yaligundua kuwa majeshi ya Ukraine yameibadilishia matumishi iliyokuwa hospitali ya wajawazito na watoto na kuifanya maficho ya wanajeshi wa Ukraine ambapo walikuwa wanashambulia kutokea hapo.

Tangu siku hiyo Urusi ilitoa onyo kuwa hospitali hiyo isitumiwe na majeshi ya Ukraine vinginevyo ingeshambuliwa. Ukraine waliendelea kuitumia hospotali hiyo kijeshi na kutokea humo kuendeshaashambulizi.

Kilichowatokea kila mmoja amekisikia na kelele ni kila kona!! Hizi picha wanazoonesha za watoto na wajawazito wakiwa majeruhi zilikuwa zimeandaliwa kabla!

Propaganda Kali inaendeshwa ili tu kuonesha Urusi inafanya unyama!
Umeandika utoto Askari wa Ukraine wana uhuru wa kukaa popote wako nchini mwao huwezi wapangia wakae wapi

Wao ni Raia halali wa Ukraine waweza kaa kambini ,hospitalini,wodini au vyuoni au popote wako ndani ya nchi yao utawapangiaje kuwa wakae wapi.

Unaungana na huo ujinga wa warusi? Wao kukaa hata hospitali sawa tu si wanalinda hospitali zao kosa lao nini kukaa kulinda majengo yao zikiwemo hospitali?

Eti unawaambia tokeni hapo hospitali malipo mnapolinda majengo vyenu ya hospitali na kulinda madaktari na manesi wasidhuriwe tokeni.Watoke ili uvurunishe makombora uue madaktari ,manesi,wagonjwa nk

Askari wa Ukraine walikuwa sahihi kuweka wanajeshi kulinda hospitali zao

Alichofanya Russia hapo ni uhalifu wa kivita dhidi ya majengo ya kiraia
 
Sawa ila wakipigwa wasilalamike kuwa wamepiga mabomu wajawazito!!
 
Back
Top Bottom