Mashambulizi ya Urusi yaua watu 8 na kujeruhi wengine zaidi ya 20 nchini Ukraine

HERY HERNHO

Member
Mar 4, 2022
70
313
20230415_12_1243577_L.jpg

Mashambulizi ya Urusi huko mashariki mwa Ukraine yamesababisha vifo vya watu wanane na kuwajeruhi wengine zaidi ya 20.

Mkuu wa Majeshi ya Ukraine amesema mashambulizi makali yanayofanywa na vikosi vya Urusi yaliendelea jana Ijumaa katika eneo la Sloviansk na maeneo mengine ya Donetsk, mashariki mwa nchi hiyo.

Gavana wa Donetsk, Pavlo Kyrylenko, amesema kupitia mitandao ya kijamii kuwa watu waliouawa kwenye mashambulizi hayo ni pamoja na mtoto mmoja mwenye umri wa miaka miwili.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amelaani mashambulizi hayo. Ameitaja Urusi kama taifa ovu, na kusema kuwa Ukraine haitaacha kumwadhibu adui yeyote.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu wa Ukraine, Denys Shmyhal, amesema nchi yake inajiandaa kufanya mashambulizi ya jibizo ikisaidiwa na mataifa ya magharibi. Shmyhal kwa sasa yupo nchini Marekani na alizungumza na wanahabari juzi Alhamisi.
 
Nilijua tu lazima watasema mtoto. Hao ni mamluki wamekutana na kitu kizito.
 
Back
Top Bottom