Katika utulivu wa usiku, peke yako, kabla hujalala, kuna sauti ile ya ndani inayokuuliza:
“Ningekuwa nani kama singezaliwa hivi nilivyo?”
Sauti hii haijibu kwa haraka, haipigi kelele, lakini huacha mdundo fulani moyoni—wa tafakuri, wa uchungu, wa kukiri kimya kuwa maisha hayakuwahi kuwa meza...