uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Tunahitaji uchaguzi huru au uchunguzi huru?

    Serikali imekuja na gea ya kutaka maridhiano. Je, tunaanzaje wakati walioumiza wenzao ndiyo wamejipa mamlaka ya kusamehe? Nani anamsamehe nani bila kujua nani alifanya nini na kwanini?
  2. TEC na Wakristo na Waislam Safi hakuna Kurudi Nyuma : Tuliposema Maridhiano kabla ya Uchaguzi, walitubagaza, Wamepora Uchaguzi wataka Maridhiano!

    Hakuna Hakuna Hakuna MARIDHIANO baada ya Mauaji ya Halaiki, HAKUNA HAKUNA !!.
  3. PostGE2025 BAKWATA mkoa wa Morogoro yaunga mkono kufanyika kwa uchunguzi vifo vya Oktoba 29

    Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Morogoro limeunga mkono agizo la Serikali ya Awamu ya Sita kutaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza vifo vilivyotokea baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29. . Sheikh wa Mkoa huo, Twaha Kilango, amesema uchunguzi wa haraka unahitajika ili...
  4. PostGE2025 KKKT: Tumehuzunishwa na kusikitishwa na matukio yalitokea Oktoba 29 yaliyokosa UTU, HESHIMA na TAMANI ya binadamu

    Nchi yetu imefanya uchaguzi Mkuu wa Taifa tarehe 29 Oktoba 2025. Sote tunakumbuka kuwa siku hiyo na siku zilizofuata, nchi yetu imepitia hali ngumu ambayo haijawahi kutokea katika historia yake. Palitokea vurugu zilizababisha upotevu wa maisha, ulemavu na uharibifu wa mali za umma na binafsi...
  5. #D9 Naomba baadhi ya vijana tuelekee kwenye ofisi za wizara ya afya kwa unyama waliotufanyia wenzetu yani kama tulivyopita vituo vya uchaguzi

    #D9 Naomba baadhi ya vijana tuelekee kwenye ofisi za wizara ya afya kwa unyama waliotufanyia wenzetu yani kama tulivyopita vituo vya uchaguzi. Ili ushenzi wote uishe lazima tukakinukishe kwenye ofisi zao hatuwezi kukubali unyama huu uachwe kwenye nchi yetu. Kuna watu mpaka hivi sasa hawajapata...
  6. PostGE2025 Jaribio la kuhatarisha usalama wa taifa lilianza uchaguzi mkuu 2020 idara na mamlaka wakajiona washindi sasa tunavuna matokeo

    Hii idara huenda haipo huwa tunadanganywa kama taifa, inawezekana vipi idara ilishindwa kuona hatari iliyopo wakati wa Uchaguzi Mkuu 2020, then 2024 serikali za mitaa na mwaka huu wakapuuza security alert iliyokuwa imeshaonekana mapema? Hii idara ivunjwe kama ipo kweli maana naona mambo mengine...
  7. PostGE2025 Wizara ya Afya yazidi kuuthibitishia ulimwengu kuhusu Serikali ya Samia kuficha ukweli wa Mauaji ya kutisha yaliyofanywa kipindi cha Uchaguzi

    Anguko Kuu la CCM na Serikali yake halitotokana na jambo lingine lolote lile zaidi ya kukosa akili. Kukosa kwao akili ndo kumesababisha wawapuuze Wananchi na madai yao ya ukweli kisha kukimbilia kuwateka, kuwaua na kuwapoteza hali iliyopelekea hasira za Wananchi kupanda na kufikia kikomo na...
  8. M

    PostGE2025 Shura ya Maimamu: Tunalaani mauaji ya watu wasio na hatia wakati wa uchaguzi mkuu. Tunakataa kupongeza uchaguzi mkuu uliofanyika

    SHURA YA MAIMAMU TANZANIA KAMATI KUU YA SIASA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2025 Imetolewa Tarehe 15/11/2025 Utangulizi Taifa letu la Tanzania lilifanya uchaguzi wa viongozi wa kitaifa Rais, Wabunge na Madiwani Tarehe 29 Oktoba 2025. Katika uchaguzi huo Shura ya Maimamu Tanzania ilikua...
  9. Wale mnaosikia juujuu tu kwamba mauaji ya maelfu Watanganyika wakati wa uchaguzi ni kisasa, kujeni niwa-brief kidogo

    Uchaguzi mkuu Oct.29 Mwaka 2000 Mkapa akiwa anatetea mhula wa pili wa urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, zanzibar ccm walimsimamisha Aman Abeid Karume akichuana na Maalim Seif wa CUF wakati huo. Seif alitia upinzani mkubwa sana kwa Karume. Na kulikuwa na kila dalili ya CUF kushinda...
  10. PostGE2025 Rais Samia: Nitaunda Tume ya Maridhiano na Upatanishi ‘baada ya kujua kiini cha vurugu’

    Rais Samia amesema ataunda tume ya maridhiano na upatanishi na kuanza mchakato wa mabadiliko ya Katiba baada ya kujua kiini cha vurugu kwenye uchaguzi mkuu.
  11. PostGE2025 Kuiba uchaguzi ilianza mdogo mdogo kudokoa hawakuanza tu kuua watu kwa siku moja pia na hii ni baada ya kuona vyombo vya usalama ni dhaifu

    Kuiba uchaguzi ilianza mdogo mdogo kudokoa hawakuanza tu kuuwa watu kwa siku moja pia na hii ni baada ya kuona vyombo vya usalama ni dhaifu. Mtu kwasasa anafanya mapinduzi ya nchi kwa kuiba uchaguzi alafu vyombo vya usalama vinajioa akili na kumpigia saluti kuwa ni rais. Wananchi tutachukua...
  12. Kwenye malumbano ya hoja ITV kuna kijana anasema siku ya uchaguzi mkuu wa Bara alikuwa Zanzibar

    Ni nani huyu? Zanzibar alienda kufanya nini? Kwani hakupiga kura? Au ndio resource mobilization? Alisema anaona mitandaoni kuhusu habari ya D09, na kama ikitokea waachiwe wao (kijana) wadili na hao waandamanaji...
  13. A

    Balozi za nchi za Nordic (Denmark, Sweden, Norway na Finland) zatuma ujumbe kuhusu mauaji katika uchaguzi

    Balozi za nchi za Nordic zimetuma jumbe tofauti kwenye kurasa zao za Instagram kuhusu mauaji yaliyofanyika katika uchaguzi wa tarehe 29. Ubalozi wa Finland unatoa rambirambi zake za dhati kwa wote waliopoteza wapendwa wao na kwa wale walioathiriwa na matukio ya hivi karibuni baada ya uchaguzi...
  14. R

    PostGE2025 Uchaguzi wa 2025 Tanzania imeng'ara kwenye magazeti kama nchi ya mauaji na isiyo na demokrasia

    Historia ya Tanzania imebadilika ghafla kutokana na udikteta wa Rais Samia, Taifa lililosifika ulimwenguni kwa amani na ukarimu wa raia wake, sasa imekuwa nchi inayozungumzwa kama nchi iliyojaa mauaji, ukandamizaji na udikteta Vyombo vyetu vya habari vilipuuza sana kuripoti habari za matukio ya...
  15. H

    PostGE2025 Kinachoitwa Maridhiano Ni Uhuni wa Watawala na CCM, Maridhiano Yalistahili Kabla ya Uchaguzi

    Mmesikia kelele za watawala, baada ya kupoka madaraka kwa nguvu kupitia uchaguzi bandia, baada ya kuwaua watanzania wengi waliokuwa wakipinga uchaguzi haramu, baada ya kuteka, kuwaua na kuwapoteza watanzania wengi, kwa unafiki mkubwa, sahizi wanaimba maridhiano. Kabla ya uchaguzi, watanzania...
  16. B

    Ulisema uchaguzi umekwisha, basi ondoa mapicha yako mitaani, pleaseee!

    Kama uchaguzi umekwisha ondoa hii mipicha mitaani, please! Watu walizichoma walizoweza, hawataki kuziona Si kila kitu lazima ushindane na matakwa ya wananchi
  17. Shukrani: Nawashukuru kwa kunichagua. Uchaguzi ulikuwa huru na haki

    Nawashukuru sana kwa kunichagua. Uchaguzi ulikuwa huru na haki
  18. GE2025 Rais Ruto: Sisemi Tanzania hakuna demokrasia, lakini Kenya huwezi kushinda Uchaguzi kwa asilimia 96

    Hapa Ruto ni kama ametupa jiwe gizani hivi Yaani kapiga kwenye mshono alafu kajitetea
  19. M

    PostGE2025 ACT Wazalendo: Mchakato wa uchaguzi uliharibiwa na tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC). Tutakwenda mahakamani

    Chama cha ACT Wazalendo kimesema kimejipanga kuchukua hatua za Kisheria kwa kile wanachodai kuwa ni kudai haki ya ushindi walioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Kauli hiyo imetolewa na Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Profesa Omar Fakih, wakati...
  20. Ijengwe minara kuwaenzi waliouawa kipindi cha uchaguzi mkuu 2025

    Hakuna namna nyingine sahihi sana ya kuwaenzi hawa zaidi ya kuwajengea minara katika mikoa husika. Mnara mkuu utawekwa Dar Es salaam. Utaitwa mnara wa pili wa mashujaa. Kisha kila mkoa ambao.palitokea mauaji ya halaiki pajengwe mnara kisha majina yote ya waliouawa yawekwe hapo. Kadhalika picha...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…