uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Just Pray

    PostGE2025 Padre Kitima akumbushia matukio ya Oktoba 29 asema 'kesi za uvunjaji wa haki za binadamu hazifutiki'

    Padre Charles Kitima anasema aliyetumwa, aliyetoa mamlaka kupiga risasi akijua kabisa ni kinyume cha sheria atawajibishwa tu ni suala la wakati. Anasema masuala ya kesi za kibinadamu hayafutiki!! Soma Pia: PostGE2025 Padre Kitima: Nilishauriwa na watu nisiende kumzika Jenista
  2. M

    Upinzani waitaka IEBC iachane na teknolojia ya Smartmatic kabla ya uchaguzi wa mwaka 2027

    Viongozi wa Upinzani Wote wametaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) iachane kabisa na teknolojia ya Smartmatic kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Viongozi hao, wakiwemo Kalonzo Musyoka wa Wiper Patriotic Front, Justin Muturi wa DP, na Eugene Wamalwa wa DAP-K, pia waliwaomba Mahakama...
  3. K

    Bila kupatikana kwa katiba mpya ya wananchi tume huru ya uchaguzi Nchi haitakuja kutawalika tena

    Kwa heshima ujengwe mnara mkubwa wa makumbusho ya kumbukumbu ya kuwa kumbuka kila mwaka wahanga wetu wote. Walioteswa Waliopotezwa ama kuuwawa na CCM kabla na baada ya mauwaji ya uchaguzi wa October 29,2025 kwa kuyaandika majina yao wote kama Mashujaa wa Taifa.
  4. Nyani Ngabu

    Kim Jong Un ashinda uchaguzi kwa asilimia 99.93!

    Vichekesho! Hatimaye Samia [ambaye si rais] apata mpinzani. Kim Jong Un ameshinda uchaguzi uliofanyika tarehe 15 mwezi Machi mwaka huu. Kim kampiku Samia 😂. Samia asije kuona wivu. ============ Kim Jong Un amepata ushindi mwingine mkubwa wa uchaguzi, baada ya chama chake cha Workers' Party...
  5. Yoda

    2015 ndio ilikuwa mara ya mwisho Tanzania kuwa na uchaguzi, tusichanganyikiwe

    Tutaongea yote ila mara ya mwisho Tanzania kuwa na uchaguzi mkuu au serikali za mitaa ni mwaka 2015. Kumuhusudu na kumkubali aliyesababisha hali hii yote ya sasa huku unamlaani na kumkosoa mrithi na mwanafunzi wake ni sawa na kuchanganyikiwa na kuwa bumunda.
  6. Dalton elijah

    Uchaguzi Mkuu Jamhuri ya Kongo: Mtandao wa Intaneti wazimwa!

    Wakati uchaguzi wa uraisi unaendelea jamhuri ya kongo mtandao wa NetBlocks umetangaza kukatika kwa intaneti karibu nchi nzima. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa NetBlocks, Alp Toker, kiwango cha muunganisho wa intaneti kimeshuka hadi karibu asilimia 3 ya kiwango cha kawaida, hali inayoweza kupunguza...
  7. Parabolic

    Tanzania yaiangalia Tume ya Uchunguzi wa Vurugu za Uchaguzi 2025 kama kipimo cha uwajibikaji

    Geneva, Uswisi. Tanzania imeangazia juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, katika kuimarisha uwajibikaji, maridhiano na kuendelea kuzijenga taasisi za umma kupitia kuundwa kwa Tume Huru ya Uchunguzi kuhusu vurugu zilizohusishwa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Hayo yaliwasilishwa katika tukio...
  8. M

    Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu imesema kila jambo la tume ya uchaguzi ni lazima lihojiwe mahakamani!

    Anaandika Jebra Kambole AfCHPR imesema ibara ya 74 (12) Ya Katiba ya Tz na Ibara ya 119(13) ya Katiba ya Zanz zinakiuka ibara ya 3(2) na 7(1)(a) ya Mkataba wa ACHPR kwa sababu ibara hizo zinakataza kufungua kesi ya kupinga ujinga wa INEC na ZEC. Tunashukuru kuwa kwenye Timu ya Mawakili wa kesi...
  9. M

    Mahakama ya Afrika yatupilia mbali shauri la kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2020

    Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imetoa uamuzi wake uliosubiriwa kwa muda mrefu kuhusu shauri lililopinga uhalali wa uchaguzi mkuu wa Tanzania wa mwaka 2020. Katika hukumu yake, mahakama hiyo imetupilia mbali kesi hiyo kwa kukosa mashiko ya kisheria na ushahidi thabiti. Wapinga...
  10. Mhaya

    Trump Ataka Kupitishwa kwa “Save America Act” Ili Kulinda Mfumo wa Uchaguzi na Sera za Kijamii

    Kumekuwa na mjadala mkubwa nchini United States kufuatia wito wa kupitishwa kwa sheria mpya inayojulikana kama “Save America Act.” Sheria hii inapendekezwa na Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, ambaye amesisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha uadilifu wa uchaguzi pamoja na kulinda...
  11. Dalton elijah

    Wadau wajadili hasara kuzimwa intaneti wakati wa uchaguzi

    KUZIMWA kwa intaneti wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kumelisababishia Taifa hasara ya dola za Marekani milioni 238, sawa na takribani Sh. bilioni 560, kwa mujibu wa ripoti mpya ya utawala wa kidijitali. Takwimu hizo zimetolewa na Ofisa Sera na Teknolojia wa Tech, Media Convergency (TMC)...
  12. Kijukuu cha Tanzania

    PostGE2025 Uchaguzi Mkuu wa 2025 ulivyoonesha vazi la Demokrasi la Tanzania linavyochakaa kupitia INEC, Vyama vya Upinzani

    Tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyamavingi Mwaka 1992, Tanzania imejengwajuu ya msingi wa kikatiba unaotambuademokrasia, utawala wa sheria na heshimakwa haki za binadamu. Katiba ya Jamhuri ya Muungano inawekawazi haki za msingi, ikiwemo uhuru wakukusanyika na kujiunga na vyama vyasiasa, uhuru wa...
  13. Roving Journalist

    Ngulangwa: Inawezekana CUF kutotambua Uchaguzi wa Oktoba 29 imesababisha Msajili aone Uchaguzi wetu ulikuwa batili

    Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imetangaza kuwa matokeo ya Uchaguzi wa Viongozi wa Kitaifa wa Chama cha Wananchi (CUF) wa Desemba 2024 ni batili na kuelekeza chama hicho kurudia uchaguzi wa nafasi za juu za uongozi mara moja. Hoja ya awali hii hapa ~ Msajili amtaka Profesa Lipumba na...
  14. Parabolic

    Msajili amtaka Profesa Lipumba na wenzake warudie uchaguzi CUF

    Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imetangaza kuwa matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa kitaifa wa Chama cha Wananchi (CUF) uliofanyika Desemba 2024 ni batili na kuelekeza chama hicho kurudia uchaguzi wa nafasi za juu za uongozi mara moja. Kwa mujibu wa Jambo TV, barua ya Februari 13...
  15. Genius Man

    Suala la Msajiri kutengua uwenyekiti wa Lipumba hana hayo mamlaka na umekaa kisiasa kwanini ametengua baada ya kukosoa uchaguzi achunge sana huyo mzee

    Suala la Msajiri kutengua uwenyekiti wa Lipumba hana hayo mamlaka na umekaa kisiasa kwanini ametengua baada ya kukosoa uchaguzi achunge sana huyo mzee. Hakuna mtu mwenye nguvu kuliko umma hakuna mpumbavu ambaye tutamuacha salama kwenye fagio linalokuja msajiri ni mpumbavu anatumika kuhujumu...
  16. Genius Man

    Kesi ya Lissu: Shahidi anasema hajui kama kuzuia uchaguzi, kuandamana ni kosa sasa mtu kama huyu ameendaje mwenyewe polisi kushtaki kosa?

    Kesi ya Lissu: Shahidi anasema hajui kama kuzuia uchaguzi, kuandamana ni kosa sasa mtu kama huyu ameendaje mwenyewe polisi kushtaki kosa? Kuna upumbavu mwingi sana kwenye jeshi la polisi lazima wahusika wa upumbavu huu watawajibishwa. kijana ameshinikizwa na polisi kuja kuongea vitu asivyo...
  17. Roving Journalist

    Kesi za kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2025 Zanzibar, zakutana na kikwazo Mahakamani

    https://www.youtube.com/watch?v=VvgEZ6hch6A Kwa mara nyingine tena, kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar wa Oktoba 29 mwaka jana zimeambatana na kikwazo baada ya upande wa Jamhuri kuhoji uhalali wa viapo vilivyoandaliwa katika kesi hiyo. Hoja hiyo imewasilishwa mbele ya Jaji Salma...
  18. A

    KERO Dar inazidi kuwa na mazingira yasio na mpangilio. Viongozi wana hofu au wanaogopa Wananchi baada ya Uchaguzi wa 2025?

    Tunatambua tangu matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi 2025 yamesababisha usimamizi wa usafi na mazingira kuzorota, hofu ikiwa kwa Wanasiasa kuogopa lawama za Wananchi. Hii imesababisha mji kuwa mchafu sana, tunajenga barabara nzuri lakini mabanda kila mahali, ukienda Mbezi Mwisho...
  19. Genius Man

    Lissu akiachiliwa hiyo tarehe 9 sasa ndipo uchaguzi utarudiwa kwa nguvu zote za wananchi kwa sasa bado hatujafanya uchaguzi wowote

    Lissu akiachiliwa hiyo tarehe 9 sasa ndipo uchaguzi utarudiwa kwa nguvu zote za wananchi kwa sasa bado hatujafanya uchaguzi wowote. Je watamtoa chuma tarehe 9 au wataanza visingizio sijui shahidi anaumwa tumbo hajafika tuhairishe kesi.
  20. PAYE

    Rais samia: Nampongeza Museveni kwa ushindi mkubwa wa Uchaguzi

Back
Top Bottom