tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. D

    JamiiForums Tanzania Serikali (NEMC na TCRA) kuna pesa za bure hapa wala msijiulize mara mbili

    Kila idara ya serikali siku hizi ina vyanzo vya mapato! Ndungu zangu NEMC naona bado wamelala usingizi wa pono wakati kuna pesa kibao za kuokota! 1. Sheria na kanuni za mazingira ziko wazi kabisa! Hivyo basi! Nashauri NEMC ianze kutoza kodi ya spika na miziki mikubwa katika kumbi na taasisi...
  2. JanguKamaJangu

    JamiiForums Tanzania TCRA: Tumia simu vizuri, ukimdhalilisha mwanamke mtandaoni jela inakuhusu

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaonya watu wanaofanya vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake mitandaoni, ikisema kufanya hivyo ni kosa la kihalifu kwa mujibu wa sheria za nchi na kunaweza kumpelekea mtu kutozwa faini, kufungwa jela au vyote kwa pamoja. Wito huo umetolewa hivi...
  3. MNEKI

    JamiiForums Tanzania TCRA /COSOTA au Mamlaka zinazohusika hamuoni tamthilia ya BONDITA Azam two unavyoharibu watoto kwa kuhamasishwa ndoa za utotoni.?

    -Hao waigizaji wakuu Bondita na mumewe mbona wanatofautiana sana umri. -Watoto wanajifunza nini wakiona mtoto mwenzao analiita baba zima ''mumewangu'' -watoto wadogo wanawaza kuolewa kuliko hata homework -Na Mamlaka zinazohusika mpo tu,, sasa mna msaada gani kama tatizo kama hili hamulioni? -Ee...
  4. Mwanga Lutila

    JamiiForums Tanzania TCRA, Vodacom wanatukata 200 kila tuongezapo salio za nini?

    Hii sasa kwangu ni mara ya tatu, Sijawahi kopa Ila nashangaa kila nikiweka salio. Sina huduma yoyote ambayo nimejiunga. Huu ni wizi.
  5. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania TCRA: Kasi ya internet inasababisha kifurushi kuisha haraka

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaja vitu vitatu vinavyosababisha kuisha kwa bando haraka ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kasi ya internet, uwezo wa simu janja na kuwa na application nyingi kwenye simu. Pia imesema gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine nchini...
  6. Risk manager

    JamiiForums Tanzania TCRA hivi mpo kwa ajili yetu ama? Waziri wa Mawasiliwano tusaidie hili

    Habari zenu wanajukwaa. Ninaomba hili suala limfikie mwenye dhamana na haya Mambo yanaboa Sana. Unanunua kifurushi wanakupangia muda wa kutumia. Mfano hapa nimeshajiunga sms za shs1500 kwa Airtel sms 9000. Shida mpaka napangiwa sms za kutuma kwa siku hivi kweli hii ni uungwana ama wao...
  7. BUMIJA

    JamiiForums Tanzania Naomba Msaada wa kutoa taarifa ya utapeli

    Hii namba kapiga huyu jamaa akijifanya ni Airtel Customer Care na kuniambia amekosea kutuma hela laki moja. Huku akaunti yangu haina hiyo hela. Naomba mnisaidie kumripoti TCRA mnaojua, kanitukana sana nlipomgundua.Namba za Tapeli ni 0683595613
  8. John Haramba

    JamiiForums Tanzania Picha aliyoposti Makonda siku moja baada ya Mahakama kutoa kibali cha kuchapisha Gazetini wito wa kumuita Mahakamani

    Siku moja tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kutoa kibali cha kuchapisha Gazetini wito wa kumuita Mahakamani aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda na kuubandika wito huo katika Makazi yake ya Dar na Kijijini kwao Koromije, Makonda amepost picha kwenye ukurasa wake ikimuonyesha akiwa...
  9. B

    JamiiForums Tanzania Waziri Nape, kuhusu vifurushi vya simu tatizo lipo TCRA

    NDUGU NAPE, KUHUSU VIFURUSHI VYA SIMU Bashir Yakub, WAKILI. +255714047241. Ndugu yangu Nape tatizo liko hapo TCRA. Haya makampuni ya simu yanafanya biashara na hivyo yanaweza fanya lolote yasipopata usimamizi. Tunahitaji Kanuni za vifurushi kama vifurushi kutoka hapo TCRA ili zitusaidie...
  10. beth

    JamiiForums Tanzania TCRA yasimamisha kipindi cha EFATHA cha Nabii Josephat Elias Mwingira kwa miezi mitatu, Star TV yapewa onyo

    Kamati ya Maadili ya TCRA imesema Kituo cha Star Tv kimeonesha uzembe na udhaifu katika kusimamia kipindi cha EFATHA Ministries ambacho hurushwa kwa matangazo ya moja kwa moja, kwa kuruhusu maudhui yenye ukakasi ambayo ni kinyume na Kanuni za Mawasiliano TCRA ikimnukuu Askofu Josephat Mwingira...
  11. GENTAMYCINE

    JamiiForums Tanzania Nape acha 'Kukurupuka' hili la 'TCRA' laweza 'Kukuharibia'. 'Boss' wako 99% anategemea hizo 'Tozo' ili nchi iende

    Umeanza kwa Pupa sana Kamarada ( Comrade ) sijui bado 'appointment hangover' inakusumbua pamoja na Ujana ulionao? Jeuri ya Boss wako ( Mama ) ipo katika hizi Tozo mbalimbali sasa leo hii unavyotaka TCRA ipunguze kwa kutafuta Kwako Sifa kwa Watanzania huku ukimkosesha Mama Mapato ya Kuongezea...
  12. Chachu Ombara

    JamiiForums Tanzania Waziri Nape Nnauye aitaka TCRA kuyaagiza Makampuni ya Mawasiliano kusitisha upandishaji wa bei ya Vifurushi

    Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nnauye ameiagiza TCRA kuyaagiza makampuni ya simu kusitisha upandishaji wa bei ya Vifurushi mpaka hapo watakapokaa na Serikali kuzungumza kuhusu jambo hilo. Chanzo: DarMpya Pia soma - Gharama za vifurushi vya intaneti zapandishwa tena kimya...
  13. NostradamusEstrademe

    JamiiForums Tanzania TCRA Naomba fuatilieni hii kitu hawa watu wanatapeli watu sana

    Leo nimetumiwa message kutoka kwenye namba +255733326905 kuwa nimeshinda Biko ya milioni 5 waliniona mimi ni zuzu wa kuona milioni tano nitahaha. Wakanipa maelekezo nipige kwenye namba hii 0719254427 Nawaomba cyber polisi na TCRA fuatelieni nyendo za hizi namba mishowe mtamkamata huyu mtu. +
  14. MR.NOMA

    JamiiForums Tanzania Matapeli wa Simu wanazidi, licha ya simu kusajiliwa! Nani alaumiwe, Makampuni ya simu, TCRA, Polisi au Raia?

    Wakuu hizi sms Mzee flani ni mganga maarufu, atakupa utajiri wa freemason, mara utajiri wa ndagu nk. sasa zimetawala sana, na hizi zingine za umeshinda milioni 700000000, piga Simu 0000 ili upate zawadi zako. Au unapigiwa simu na litapeli likisema Kuna Hela imetumwa kwako kimakosa. Simu zote...
  15. Inside10

    JamiiForums Tanzania TCRA waipa onyo wasafi Tv kwa kukashifu dini ya kikristo.

    Kamati ya Maudhui ya TCRA, leo Jumatano imeipa onyo Wasafi Televisheni, pamoja na kuitaka iombe radhi mara tatu kwa siku, kuanzia kesho Alhamisi hadi Jumamosi, huku ikiiamuru ilipe faini ya Sh. 2 Mil., baada ya kukutwa na hatia katika kosa la kurusha maudhui yenye kukashifu dini ya Kikristo...
  16. Naipendatz

    JamiiForums Tanzania Balozi Kagasheki: TCRA Mnachekesha

    Anaandika Balozi Khamis Sued Kagasheki kupitia ukurasa wake wa Twitter na ninamnukuu; Humphrey siyo rafiki yangu. Pia siyo adui yangu. Sikuwahi kuketi popote na yeye kwa maongezi. Mara moja tu niliongea nae kwa simu kuhusu jambo lililo mhusu mwanachama mwenzetu na Boss wake (Bashiru) alikuwa...
  17. Poppy Hatonn

    JamiiForums Tanzania TCRA haina malaika ya kuzuia Darasa la Uongozi.S

    Siyo kila mtu anayesema ana mamlaka ya kufanya jambo anayo mamlaka hayo. Kile kipindi cha phone-in. Watu walikuwa wanapiga kutoa maoni yao kuhusu kile kipindi. TCRA iliwasikiliza watu wale? Wale watu walikuwa na shukrani sana kwa Polepole. Polepole alikuwa anaongea maneno kama vile ," Mwajibishe...
  18. Niache Nteseke

    JamiiForums Tanzania TCRA Yamfungia Polepole, Mwenyewe Asema "Kusema Ukweli ni Sehemu ni Safari Ndefu."

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kwa muda usiojulikana kipindi cha Shule ya Uongozi kinachomilikiwa na Mbunge, Humphrey Polepole kwa makosa matatu likiwemo la kutoa taarifa ya upotoshaji kuhusu chanjo ya Uviko 19.
  19. Pascal Mayalla

    JamiiForums Tanzania Hongera TCRA kusisitiza Professionalism kwenye habari! Acheni double standards, acheni uonevu. Tendeni haki kwa Watanzania!

    Wanabodi, Naomba kuanza uzi huu kwa declaration of interest. Mimi ni mdau mkubwa sana wa TCRA, nawakubali sana, na hadi vipindi vyao nafanya Ila TCRA ilichomfanyia Humphrey Polepole na shule yake ya uongozi sio sawa, sio haki, ni kumuonea na TCRA kufanya maamuzi kwa double standards...
  20. R

    JamiiForums Tanzania Naipongeza TCRA kwa kumkomesha Polepole and the Likes: Massage sent!

    Ktk vitu ambavyo intelijensia haijachukulia mzaha ni pamoja na swala la Polepole. Hata kama mlichelewa kumfumba mdomo lakini atleast mmejaribu. Huyu Polepole tungemchekea mwisho wa siku tungevuna mabua Waswahili husema ukimchekea sana Mbwa itakuja siku atakufata msikitini. Haiwezekani mtu...
Back
Top Bottom