tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. Mateso chakubanga

    JamiiForums Tanzania TCRA fuatilieni matapeli wa mtandao wanaojiita" Digital Master"

    Kumeibuka kikundi cha watu wanaojiita Digital Master kikiongozwa na mtu anaejiita Saidi Mbondela jijini Daresalaam ambao kazi yao ni kutangaza wana uwezo wa kutengeneza programme katika simu kwaajili ya kufuatilia message, na simu za watu,aidha mtu huyo mwenye namba 0757039596 anakuhitaji...
  2. Z

    JamiiForums Tanzania TCRA tuambieni nani alimshitaki Polep[ole? Kuna matatizo makubwa ya maamuzi.

    TCRA imemshitaki Polepole, Polepole akajitetea kwa TCRA, halafu TCRA ikamhukumu! That is no right! Kuna tatizo kubwa sana. Muhusika amesoma kwa maringo sana juu ya mwenendo mzima wa maamuzi ya TCRA lakini mwishoni mtu unaona ni kama upuuzi wa aina fulani vile. Haijulikani makosa yameanzia kwa...
  3. chiembe

    JamiiForums Tanzania Humphrey, ulikuwa unapeleka majina yetu TCRA na Polisi kwa Makosa ya Mitandao, Sasa upanga unakukata upande wa pili

    Humphrey na kundi lake la Wana ccm mtandaoni walikuwa wanapeana posho kusaka wanaomkosoa JP na serikali yake, watu wengi waliokamatwa na kushitakiwa ni kazi ya Humphrey na kikosi kazi chake, na aliomba fungu maalum, Leo walewale aliokuwaa awapelekea majina ndio wanamla N.B: alitishia ma RPC na...
  4. Jidu La Mabambasi

    JamiiForums Tanzania TCRA: Kipindi cha Shule ya Uongozi cha Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji

    Kamati ya Maudhui ya TCRA imesema kipindi cha Shule ya Uongozi cha Mbunge Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji. Kamati imeongeza kuwa maudhui ya kipindi ni ya upotoshaji na yanayoweza kusababisha taharuki kwa wananchi. Sasa kiki ya...
  5. The Dictator

    JamiiForums Tanzania TCRA: Polepole Tv ina mapungufu ya kutokuwa na wafanyakazi wenye taaluma ya uandishi na utangazaji habari

    "Humphrey Polepole Online Television ina mapungufu ya kutokuwa na wafanyakazi wenye taaluma ya uandishi na utangazaji wa habari, jambo linalowapelekea kukiuka sheria, kanuni, misingi na maadili ya uandishi na utangazaji wa habari katika kazi zao." Kamati ya Maudhui ya TCRA imesema kipindi cha...
  6. At Calvary

    JamiiForums Tanzania Humphrey Polepole: Sihami CCM labda Wanitupe nje!, Nimeitwa TCRA nijieleze. Hoja haipigwi rungu bali inajibiwa

    Hi guys. Hope mnado poa. Kuna page imeandika kuwa bwana Polepole atajitoa chamani wakishirikina na taasisi 2. Hii ni nyepesi nyepesi. At Calvary. ==== Taarifa kwa Vyombo vya Habari. Jumamosi tarehe 11, Disemba 2021 saa 5:00 Asubuhi nitazungumza na Wanahabari pamoja na Mambo mengine...
  7. GUSSIE

    JamiiForums Tanzania Tulishiriki kutunga Sheria za TCRA, Humprey Polepole kwanini Unalia kuitwa na TCRA?

    Humprey Polepole na Mimi wote tulikuwa wapiga tarumbeta, Vinanda na vinubi wakati wa JPM Utofauti wetu ndani ya chama na sisi Yeye Humprey Polepole aliendekeza dharau kwa kuwa ni mtu wa kuja chamani, Sisi wengine na waomba msamaha wote kama Nape tuliogopa usalama wetu na Matumbo yetu JPM...
  8. K

    JamiiForums Tanzania Kwanini TCRA wanawaachia hawa matapeli wanatumia majina ya watu vibaya?

    Nimepokea huu ujumbe kwa mtu anaejifanya mganga anajifanya eti kakosea number na mimi mambo hayo sio muumini wake kabisa.
  9. idoyo

    JamiiForums Tanzania Athari za Tozo: TCRA “wakacha” kutoa ripoti ya robo ya 3 (R3) ya mwaka 2021

    .
  10. SULEIMAN ABEID

    JamiiForums Tanzania TCRA wanashindwa kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaoposti habari za uongo?

    Inashangaza sana kuona TCRA wanashindwa kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaopost habari za uongo kwenye mitandao kwa lengo la kupata viewers wengi. ANGALIA HII HABARI!
  11. YEHODAYA

    JamiiForums Tanzania TCRA mchukulieni hatua huyu Nabii Tito, channel yake ya YouTube inamdhihaki Yesu

    TCRA na vyombo husika mchukulieni hatua huyu nabii Tito channel yake youtube kaandika YESU ni shetani Hii ni hatari kwa jamii oneni wenyewe
  12. J

    JamiiForums Tanzania TCRA: Imekutana na Wawakilishi wa Umoja wa Watoa Huduma za Matangazo kwa njia ya Waya

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekutana na Wawakilishi wa Umoja wa Watoa Huduma za Matangazo kwa njia ya Waya (Cable Operators - TACOL), Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) na Baraza la Mashauriano la Watumiaji la TCRA (TCRA -CCC) katika kikao cha...
  13. C

    JamiiForums Tanzania Inachekesha: Afisa wa TCRA naye analalamikia speed ya internet

    Mojawapo ya Top guns wa mamlaka ya mawasiliano naye analalamika kuhusu speed ya internet aitwaye Inncoent Mungi kama sikosei ni afisa mawasiliano na mmewe mtangazaji susan Mungi naye analalamika. Dah ila imekuwaje hii nchi Internet inachukuliwa kama anasa? ukiwasha redio kuna speech Rais samia...
  14. Huihui2

    JamiiForums Tanzania Hatari ya ushoga kwa watoto wa Tanzania; Serikali itunge Sheria kuzuia vikaragosi vya Superman

    Sahau Tozo, sahau machinga, sahau COVID-19Hatari mpya inayowakabili watoto na wajukuu wetu ni Superman mpya ambaye ni shoga. Ushaur; Serikali yetu ingetunga Sheria mathubuti za kuzuia vikaragosi hivyo visionyeshwe wala kufanya mijadala kama hiyo. Maana wazung wanaweza sema ni haki ila ni kwao...
  15. PendoLyimo

    JamiiForums Tanzania Mkurugenzi Mkuu TCRA Dkt. Jabiri Bakar asisitiza Postal code ni suluhisho la utoaji huduma kwa wananchi

    "POSTAL CODE" NI SULUHISHO LA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefanya semina kwa watoa huduma za Posta leo oktoba 7, Jijini Dodoma katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Posta duniani. Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya...
  16. Travis 1

    JamiiForums Tanzania WhatsApp, Facebook na Instagram zatoweka hewani Oktaba 4, 2021

    Au tatizo hili ninalo mimi tu? ---Update---
  17. Mtini

    JamiiForums Tanzania Watendaji wa TCRA na makampuni ya simu yanashirikiana na matapeli kutuibia wananchi?

    TCRA walituambia baada ya usajiri wa alama za vidole utapeli wa tuma fedha kwenye namba hii utaisha kwani watu hao itakuwa rahisi kuwatambua. Kitu za kushangaza hili suala bado linaendelea, TCRA na makampuni ya simu yanashindwa nini kuzifunga hizi line ikiwa ni pamoja na kuwakamata hawa jamaa...
  18. N'yadikwa

    JamiiForums Tanzania TCRA yatoa onyo kali kwa Kampuni za Mabasi kuhusu usafirishaji vipeto. Wapewa muda kujisajili

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa Kampuni za Mabasi ambazo zimekuwa zikisafirisha vipeto bila kuwa na Leseni. Wamepewa muda hadi Oktoba wawe wamejisajili la sivyo kitanuka.
  19. Red Giant

    JamiiForums Tanzania Mpesa inakataa kutuma pesa tigo pesa, TCRA waangalieni hawa voda.

    Siku nyingi. Nikijaribu kutuma pesa kutoka Mpesa kwenda Tigopesa inakataa. Inarudiarudia kusema niweke namba ya siri hata mara kumi. Nahisi Voda wanafanya hili makusudi, labda wana bifu na Tigo. Maana hata kununua airtime tigo kwa kutumia Mpesa haiwezekani. Kama wana bifu, basi linatukwamisha...
  20. J

    JamiiForums Tanzania Dkt. Ndugulile: Kuanzia sasa ni namba 100 pekee itatumika kwa mawasiliano kati ya Kampuni ya simu na Mteja wake

    Waziri wa Tehama Dkt. Ndugulile amesema kuanzia sasa ni namba 100 pekee itatumika kwa mawasiliano ya kampuni ya simu na mteja wake. Hii ni katika lengo la kuondoa utapeli na wizi na kwa maana hiyo namby za kawaida haziruhusiwi kutumika.
Back
Top Bottom