Habari wakuu,
Inasikitisha na kutia hasira kuona tumefikia huku na tunasema kila siku jeshi letu ni kiboko. Kweli Panya Road ndiyo wameshindikana kiasi hiki mpaka kufikia mtu anapoteza uhai na nyie mpo?!
Ama huu ni mchongo wa mtu unaoibuliwa kila akitaka kupata maslahi yake anayoyajua...
Wakuu kwema,
Kuna habari sina uhakika kama ni ya kweli au ni uzushi tu, kwamba kuna Panya Road eti kuna eneo mjini kati walivamia tena na kufanya uhalifu na kuua! Sidhani!
Nashauri IGP aanze safisha safisha ya wahuni wote kwenye vijiwe vya wavuta bangi, tena ikibidi wenye records za uhalifu...
Assalaam Alaikum.
Wadau naskitika kuwa jirani yangu maeneo ya Tabata Bima mtaa wa Madukani jana alivamiwa na Panya Road na kumjeruhi vibaya.
Walivyofanya hivyo hawakutosheka wakawajeruhi na wengine wa 4. Majeruhi wamepelekwa Amana hospitali usiku ule ule.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea...
Wakazi wa mtaa wa Kabaga Kinyerezi yamewakuta.
Ilikuwa ana kwa ana na panya road usiku wa manane. Kwa takribani masaa 2 ikivunjwa nyumba moja baada ya nyingine. Wakazi hao macho pima walikuwa wakichungulia madirishani, wakiwa wameufyata vilivyo mmoja baada mwingine akisubiria zamu yake...
Alisikika kamanda mkuu wa kanda ya kipolisi ya dar es salaam mwezi wa tano mwaka huu wa 2022 akisema wamefanikiwa kuwakamata vijana wasiopungua thelathini na moja 31 katika operesheni ya kuwasaka panya road iliyofanyika maeneo yote ya mkoa wa dar es salaam ambayo ilianza takribani tarehe...
Wamerudi maeneo ya Tabata na hawa madogo wanapovamia hujinasibu kua hakuna wa kuwafanya kitu na huahidi kurudi eneo la tukio tena baada ya mda.
Hawa watu hushirikiana na Polisi hasa kugawana vitu wanavyo pora baada ya kuviuza hakuna mtu anaweza sema hili kwa sababu linagusa watu nyeti pia walio...
Jumatatu iliyopita vijana wahalifu maarufu kama panya road wamevamia watu, wawaibia kisha kuwajeruhi kwa mapanga.
Mmoja wao kapigwa mapanga kichwani na kupoteza damu nyingi nusura apoteze maisha. Baada ya kujeruhiwa kaporwa simu na PESA nyingi.
Mwingine kaporwa simu, PESA na passport na...
Katika pilika pilika nyingi tunaweza kusahau plight ya hawa vijana. Kuna mtu yeyote anaweza kufahamu jambo gani limewafika?
Labda Ustawi wa Jamii wanafuatilia mambo haya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Amos Makalla amesema kuwa Operesheni ya kutokomeza Panya Road ni endelevu na bado inaendelea.
RC Makalla amesema hayo wakati akizungumza kwenye kikao Maalum na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ambapo amewatoa hofu Wananchi kuwa mji uko salama.
"Kwa Panya road...
Kundi lingine la wahalifu 25 ambao wengi wao ni Vijana maarufu kwa jina la ‘Panya Road’ waliokamatwa wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Kinyerezi Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za unyang'anyi wa kutumia silaha ikiwemo mapanga.
Watuhumiwa hao walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa...
Kundi la watuhumiwa wa uhalifu ambao wengi wao ni vijana maarufu kwa jina la ''Panya Road'' wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Kinyerezi Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za unyang'anyi wa kutumia silaha (mapanga).
Mtuhumiwa wa kwanza Daud Abdallah, 22, Mkazi wa Tungini pamoja na...
Maisha na mali ya wananchi wa halmashauri ya Mlimba kata ya Mngeta na Mchombe yako hatarini kutokana na kuimbuka kwa kundi hatari la panya road maarufu kwa jina la Mungu moshi yaani bangi ndiyo Mungu wao. Vijana hawa kati ya miaka 15 mpaka 25 wanajihusisha na uporaji kwa kutumia mapanga, visu na...
JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LINAWASHIKILIA BAADA YA KUWAKAMATA WATUHUMIWA 23 KWA TUHUMA MBALIMBALI ZA KIHALIFU
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeendelea kuisimamia oparesheni maalum kali ya mtaa kwa mtaa, Kata kwa Kata dhidi ya makundi ya wahalifu ambao wengi...
Nikiwa Kama Kijana Mzalendo Hapa Tanzania Nimeamua Kujitolea Kupambana na Hawa Vijana Wapuuzi Wanao Tishia Maisha Ya Watanzania Wenzangu
Nimepitia Mafunzo Ya Ugambo mwaka 2001 nikajiunga Na jeshi Mwaka 2004.
Mwaka 2011 nikapelekwa Somalia kupambana na Vikosi vya ugaidi Mwaka 2016 nikaingia...
Mie si mshari, mchokozi na wala sina hasira.
Lakini toka majuzi panya rodi walipotetemesha hadi Kunduchi nikaona sasa wacha mbwai iwe mbwai.
Wanaume wa kanda Maalum Musoma wamezidi kutucheka.
Panya rodi mkiniona na subaru ya bluu na nakunywa mitaa ya Kunduchi njooni mnisalimie.
Nina salaam zenu.
Habari!
Panya road (vibaka) wanaudhi
Wezi wa kura (wapotosha haki) wanaudhi.
Je, kati ya makundi hayo mawili juu ni kundi lipi linaweza kuleta matatizo makubwa zaidi katika nchi kuliko jingine?
Ni kundi lipi lina afadhali?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.