Maisha na mali ya wananchi wa halmashauri ya Mlimba kata ya Mngeta na Mchombe yako hatarini kutokana na kuimbuka kwa kundi hatari la panya road maarufu kwa jina la Mungu moshi yaani bangi ndiyo Mungu wao. Vijana hawa kati ya miaka 15 mpaka 25 wanajihusisha na uporaji kwa kutumia mapanga, visu na nondo nyakati za jioni na usiku hasa siku za sikukuu. Inasadikika mmoja wao ambaye ndiye kiongozi wao anamiliki bastola ambayo ameiba kutoka kwa baba yake mstaafu wa usalama wa taifa.
Siku ya Idd Mosi mwaka huu kundi hili lilijeruhi watu kwa mapanga na visu eneno la Johnson bar na kupora vitu mbalilmbali. Vijana takribani 50 walikamatwa na kituo kidogo cha polisi Mngeta lakini siku 3 baadaye wote waliachiwa kwa kutoa pesa bila kuchukuliwa hatua yeyote.
Tofauti na panya road wa jiji la Dar, hawa wanafahamika kwa majina na makazi yao. Vijana hawa makazi yao yako Mngeta centre, mara kwa mara hukamatwa na polisi wanapofanya tukio na kuachiwa baadaye. Kwa kifupi polisi pia wanawafahamu kwa majina na makazi yao ila wamegeuza kitegauchumi chao!
Wito kwa wenye mamlaka, Mkuu wa wilaya, Mkuu wa mkoa na RPC kuchukua hatua haraka iwezekanavyo ili kunusuru mali na maisha ya wakazi wa halmashauri ya Mlimba. Pia polisi wa kituo cha Mngeta ambao wengi wao ni walevi na wanajihusisha na rushwa wazi wazi wachukuliwe hatua.