chanjo

Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.

Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini.

Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.

Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio, pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili

Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya. Kinga ni bora kuliko tiba.
  1. Sema Kimeumana

    #COVID19 Chanjo ya UVIKO-19: Wasiotaka kuchanjwa wafunguliwe kesi ya kutaka kujiua

    Wadau, Dunia sasa linaingia katika wimbi la nne (fourth wave) ya maambukizi ya korona, kama tunavyosikia na kuona kupitia vyombo vya habari vya kimataifa, Ujerumani maambukizi yamefikia takriban 52,000+ ndani ya masaa 24 ambacho ni kiwango kikubwa ukilinganisha na waves zilizopita huko nyuma...
  2. J

    #COVID19 Chanjo ya COVID-19 ni salama kwa wagonjwa wa Saratani

    Je, hupaswi kupata chanjo ya COVID-19 ikiwa kwa sasa unapokea matibabu ya saratani? Jibu: Baada ya kukagua kwa uangalifu chanjo hizi, wataalam wa matibabu wa MD Anderson katika Chuo Kikuu cha Texas wameamua kuwa chanjo za COVID-19 ni salama na zinapendekezwa kwa wagonjwa wa saratani. Wataalam...
  3. J

    #COVID19 Prof. Makubi: Wanasayansi Wazalendo wanakaribia kutengeneza Chanjo ya Corona ya Kitanzania

    Katibu mkuu wa wizara ya afya Prof. Makubi amesema kama taifa tunakaribia kupata chanjo yetu ya Corona. Prof Makubi amesema wanasayansi wazalendo hawajalala katika utafiti na wako mbioni kutupatia chanjo ya Corona ambayo itakuwa ni ya kwetu wenyewe. Source: ITV habari ============= Katibu...
  4. J

    #COVID19 Chanjo ya COVID-19 haiathiri nguvu za kiume

    Wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa nadharia zote zinazozihusisha Chanjo za #Coronavirus na kupunguza nguvu za kiume na mfumo wa uzazi kwa mwanaume sio za kweli. Aidha kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa juu ya suala hili Wataalamu wanabainisha kuwa Chanjo za corona zimetengenezwa ili...
  5. J

    #COVID19 Mchakato wa kupata Chanjo ya COVID-19 hauchukui muda mrefu

    Watu wengi wanauliza shughuli nyingi sana kupata chanjo; je, ni lazima mchakato kuchukua muda mrefu? Wataalamu wa Afya kutoka Chuo Kikuu cha Augusta huko Georgia Nchini Marekani wanasema ingawa chanjo za Pfizer-BioNTech na Moderna huchomwa kwa awamu mbili, mchakato huwa ni wa haraka na...
  6. J

    #COVID19 Chanjo hazina viambata hatari na sumu

    Je, chanjo zina viambato hatari na sumu? Hapana. Ingawa viambata vilivyo kwenye lebo za chanjo vinaweza kutisha, (k.m. zebaki, alumini, na formaldehyde) kwa kawaida hupatikana katika mwili, chakula tunachokula na mazingira yanayotuzunguka - kwa mfano, katika tuna. Kiasi katika chanjo ni kidogo...
  7. J

    #COVID19 Mwenye mzio wa chanjo (Allergic reaction) amueleze mtaalamu wa Afya kabla ya kuchanjwa Covid-19

    Inaelezwa kuwa wapo baadhi ya watu ambao wana historia ya kupata matokeo mabaya (Severe Allergic Reaction) kutokana na chanjo wanazochanjwa kipindi cha nyuma. Shirika la Afya duniani linawashauri watu ambao wana historia ya kuwa na mzio wa chanjo nyingine kuwaona Wataalamu wa Afya na kuwaeleza...
  8. J

    #COVID19 Chanjo za COVID-19 hazisababishi mimba kuharibika

    Kituo cha Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC) kinahimiza wajawazito wote, wanaofikiria kuwa wajawazito na wale wanaonyonyesha kupata chanjo ili kujikinga na #COVID19. Utafiti umegundua kiwango cha kuharibika kwa mimba baada ya chanjo ya #COVID19 ni sawa na kiwango cha kuharibika kwa mimba...
  9. hazard Don

    #COVID19 Nimekosa huduma ya afya kwakuwa sijapata chanjo. Je, chanjo ya COVID-19 ni lazima nchini Tanzania?

    Kwa mwenye kufahamu juu ya Hil naomba anifahamishe. Nimekosa huduma moja ya kituo Cha Afya hapa nchini ,sababu sijachoma Chanjo ya COVID-19. Je, hawa watoa huduma wamepata wapi jeuri ya kupinga kauli ya Mh. Rais Ile kauli ya kuwa Chanjo sio Lazima.
  10. Komeo Lachuma

    #COVID19 Je, Chanjo ya COVID-19 ilikuwa ni ya kupatia Mkopo? Sisikii tena

    Dr. John Pombe Magufuli was right. Inachukiza na kuumiza kuongea maneno haya sababu sikuwa na upendo kwake. But Ukweli ni kuwa He was Right. COVID-19 (Wabunge wa CDM waliopo Bungeni) ilikuwa ni biashara na itaendelea kuwa biashara. Watu ni kweli wapo waliofariki kwa ugonjwa huo. Sikatai but ni...
  11. L

    #COVID19 Marekani yaruhusu watu waliopewa chanjo za Sinopharm na Sinovac

    Marekani imetangaza kuwa kuanzia tarehe 8 Novemba watu waliopata chanjo kwa ukamilifu kutoka nchi zote duniani wataruhusiwa kuingia nchini Marekani kwa ajili ya utalii. Uamuzi huu umetangazwa kwa njia ya Twitter na naibu msemaji wa Ikulu ya Marekani Bw. Kevin Munoz. Uamuzi huu unafuatia marufuku...
  12. J

    #COVID19 Chanjo za COVID-19 zenye virusi hai (viral vector vaccines) hazisababishi mtu kupata CoronaVirus

    Kituo cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) kimesema chanjo zenye viambata vya virusi hai (viral vector vaccines) havisababishi mtu kupata #coronavirus Chanjo hizi hutumia virusi visivyo na madhara ili kuchochea mfumo wa kinga ili kupambana na kile inachodhani ni maambukizi Karaha...
  13. J

    #COVID19 Chanjo za COVID-19 hazizuii kuchangia au kuchangiwa damu

    Kumekuwapo maswali mbalimbali ya wanajamii wanaojaribu kujiuliza uhusiano uliopo kati ya kuchangia damu ya chanjo ya Covid-19. Watu waliochanjwa wanajiuliza kama endapo wanaweza kuambukizwa corona wanapochangiwa damu na watu ambao hawajachanjwa na wengine wanajiuliza endapo kama hujachanjwa...
  14. J

    #COVID19 Chanjo za COVID-19 haziathiri DNA kwa namna yoyote

    Kumekuwa na mining'ono kuhusu chanjo za COVID-19 kuathiri DNA. Lakini je, hili lina ukweli wowote? Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), hakuna chanjo ya COVID-19 inayoathiri au kuingiliana na DNA kwa namna yoyote ile UNICEF inaeleza kuwa chanjo hufunza seli...
  15. J

    #COVID19 Chanjo za COVID-19 hazisababishi kuibuka kwa aina (variants) mpya za Coronavirus

    Kumekuwa na taarifa nyingi za kupotosha kuhusu chanjo za COVID-19. Mojawapo ni uvumi kuwa chanjo za COVID-19 zinasababisaha kuibuka aina (variants) nyingine za coronavirus. Lakini je, ni kweli? Kwa mujibu wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC), Chanjo za COVID-19 hazitengenezi au...
  16. J

    #COVID19 Chanjo ya COVID-19 haisababishi usumaku mwilini

    CHANJO YA COVID19 HAISABABISHI USUMAKU MWILINI Kituo cha CDC kinasema chanjo ya COVID19 haisababishi mwili au sehemu ya mwili iliyochomwa sindano kutengeneza nguvu ya usumaku Chanjo hizo hazina viambata vyovyote vyenye asili ya chuma ====== Can receiving a COVID-19 vaccine cause you to be...
  17. J

    #COVID19 CDC: Chanjo za COVID-19 hazitumiki kufuatilia mienendo ya watu

    Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) kinasema Chanjo za COVID-19 zimetengenezwa ili kupambana na magonjwa na hazijapandikizwa ‘microchips’ ili kufuatilia mienendo ya watu Chanjo hufanya kazi ya kuchochea mfumo wa kuzalisha kingamwili, kama ambavyo mwili hufanya pindi unapopata maradhi...
  18. beth

    #COVID19 Marekani yaidhinisha Chanjo ya Pfizer kwa Watoto wa miaka mitano hadi 11

    Taifa hilo limeidhinisha Chanjo dhidi ya COVID19 ya Pfizer/BioNtech kwa Watoto walio na umri wa miaka 5 - 11, ikielezwa Wataalamu wamebaini ina ufanisi wa 91% katika kuzuia Ugonjwa huo kwa Watoto Kwa mujibu wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC) Marekani imerekodi maambukizi takriban...
  19. L

    #COVID19 Ni wakati kwa Marekani kuelekeza nguvu kupunguza pengo la chanjo

    Hivi karibuni, shirika la ujasusi la Marekani lilitoa ripoti kamili kuhusu chanzo cha virusi vya Corona, ambayo ilishindwa kujibu swali kuwa ni jinsi gani virusi hivyo vya ugonjwa wa COVID-19 vilimwambukiza mtu wa kwanza. Baada ya kupoteza nusu mwaka ambao ni fursa muhimu kwa dunia nzima...
  20. beth

    #COVID19 Mkuu wa WHO atoa wito kwa G20 kumaliza mzozo wa chanjo

    Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa Kundi la mataifa 20 yaliostawi na yanayoinukia kiuchumi G20 yana uwezo wa kuzuia janga la virusi vya corona kuenea zaidi na kuzuia majanga ya siku zijazo. Akizungumza wakati wa mazungumzo kuhusu afya hapo jana kwenye...
Back
Top Bottom