Guterres: Hatutakiwi kuyasahau hata maisha ya mtu mmoja aliyetutoka

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Vifo vinavyotokana na maabukizi ya virusi vya corona vimezidi watu milioni moja, kwa mujibu wa takwimu za Chuo Kikuu cha John Hopkins, huku Shirika la Afya Duniani likionya kuwa idadi hiyo inaweza kuwa ndogo zaidi ikilinganishwa na uhalisia kutokana na changamoto katika upatikanaji wa takwimu sahihi.

Mataifa yaliyopoteza idadi kubwa zaidi ya watu duniani ni Marekani, iliyotipoti vifo zaidi ya 205,000 ikifuatiwa na Brazil iliyoripoti vifo 142,000, kisha India yenye vifo 95,500, Mexico yenye vifo 76,000 na Uingereza yanye vifo 42,000.

Brazil May 14 2020.png


Katika taarifa yake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema kuwa dunia haitakiwi kuyasahau hata maisha ya mtu mmoja aliyepoteza maisha kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

"Dunia yetu imefikia hatua inayoumiza sana: kupotea kwa maisha ya watu milioni moja kutokana na maambukizi ya virusi vya corona. Lakini hatutakiwi kuyasahau hata maisha ya mtu mmoja aliyetutoka," alisema Guterres.

"Walikuwa wababa na wamama, wake na waume, kaka na dada, ndugu na marafiki. Maumivu tuliyonayo yameongezwa maradufu na athari za ugonjwa huu. Hatari ya maambukizi ilifanya familia zisiwe karibu na ndugu zao waliokuwa wagonjwa na haikuwa rahisi kuomboleza. Unawezaje kusema kwaheri bila kumshika mkono au kumbusu, au kumkumbatia na kumnong'onezea kwa mara ya mwisho "Nakupenda"? Na bado hatuoni hatima ya kusambaa kwa virusi hivi, kupoteza ajira, kuharibiwa kwa elimu na maisha yetu," alisema Guterez.



Idadi ya maambukizi imefikia visa zaidi ya milioni 33, Marekani ikiwa ndilo taifa lenye visa vingi zaidi, ikiwa na visa milioni 7 vya maambukizi, ikifuatiwa kwa ukaribu na India yenye visa milioni 6 vya maambukizi.

Unawezaje kusema kwaheri bila kumshika mkono au kumbusu, au kumkumbatia na kumnong'onezea kwa mara ya mwisho "Nakupenda"?
-Antonio Guterres

Wakati dunia ikiendelea kutafuta chanjo ya virusi hivyo, Guterres amewataka viongozi duniani kufanya kazi kwa pamoja ili kuvishinda virusi hivyo. Shirika la Afya Duniani lilitangaza siku ya Jumatatu kuwa itatoa vifaa zaidi ya milioni 120 kwa ajili ya kurahisisha upimaji wa virusi hivyo, vipimo vinavyoweza kutoa majibu sahihi ndani ya muda wa dakika 15 tu, ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo.
 
Kweli kabisa hapa kwetu tokea tulipofikia maambukizi 509 na vifo 21,tuliambiwa kuwa sisi imeisha. Ila kuna familia nyingi sana zimepoteza wapendwa wao lakini record haijawekwa sawa. Wako wengi walougua na kupona lakini record haijawekwa sawa. Kwa hiyo hata hiyo record ya WHO haiko sawa sababu ya nchi nyingi kutoweka idadi sawa.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom