Chanjo ya Virusi vya Corona kuuzwa kwa bei nafuu kwa nchi masikini

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Shirika la UNICEF limetangaza kuhusu mkakati wake wa kusambaza chanjo ya Covid-19 kwa Kenya na nchi nyingine zinazoendelea, limeripoti gazeti la daily Nation nchini Kenya.

Chanjo zote zitakazonunuliwa kupitia Covax zitauzwa kwa shilingi 300 za Kenya (takriban dola 3) kwa nchi zinazoendelea.

Shirika hilo la watoto duniani linasema kuwa limefanya mkataba na zaidi ya ndege 350 na makampuni mengine ya safari za anga kwa ajili ya kusambaza sindano bilioni billion na chanjo.

Takriban sindano milioni 500 za chanjo zitaletwa mwaka ujao. Shirika hilo Jumatatu lilisema kuwa hii itakuwa ni operesheni kubwa na ya haraka ya aina yake kuwahi kufanywa na shirika hilo.

Wataalamu wa Kenya wanatarajia kupokea chanjo za Covid-19 kwa asilimia 20 kwa ajili ya Wakenya. Wahudumu wa afya watakuwa wa kwanza kunufaika kwa kuchanjwa, wakifuatiwa na makundi yaliyomo katika hatari zaidi kama vile wazee.

Likiwa ni mnunuzi mkubwa wa chanjo duniani, Unicef kwa kawaida hununua zaidi ya dozi zaidi ya bilioni mbili kwa mwaka kwa ajili ya chanjo ya kawaida na kwa ajili ya milipuko ya magonjwa kwa niaba ya karibu nusu ya nchi 100.

Jumatatu, Chuo kikuu chaOxford na Astrazeneca pia walitangaza matokeo ya hatua ya tatu ya uchunguzi wa chanjo zao. Hii ndio chanjo ambayo inafanyiwa majaribio katika eneo la Kilifi, lakini matokeo yaliyotangazwa hayajumuishi data kutoka Kenya.
 
Attachments

  • 1606206301680.gif
    1606206301680.gif
    42 bytes · Views: 1
Chanjo itafanya kazi kwa mtu ambaye alisha athirika na huo ugonjwa na mwili ukatengeneza chanjo yake?
 
Wapewe Kenya tu, sisi miili yetu imeishatengeneza kinga ya "asili" dhidi ya corona, nina uhakika 80 hadi 90% ya watanzania tumishaugua ugonjwa huu!
Mabeberu wameijiandaa kupia hela za chanjo na dawa alafu utamuona member wa JF anaseama "mabeberu hoyee"
 
Nakuhakikishia hapa kuwa Magufuli ataikataa na kudai kuwa maombi yalishaiondosha Corona Tanzania!
Hawezi kuikataa.
Meko kwenye majukwaa anaoayuka kuwa c-19 imeisha ila nyuma ya pazia anawatuma mawaziri wake waombe mkopo wakidaipesa ya covid
 
Nakuhakikishia hapa kuwa Magufuli ataikataa na kudai kuwa maombi yalishaiondosha Corona Tanzania!
Kuna mashirika ya Ndege yameshaanza kusema mtu asipokua amechanjwa hio chanjo hataruhusiwa kupanda kwny ndege zao,so tunakoelekea ni kwamba ambao hawana hio chanjo hawatapata huduma.
 
Duh... Luna kitu si bure... yani ugonjwa umekuwa maarufu kwa siku chache na chanjo tayar na wanataka Walter Africa na policy za usafir zimeanza kulazimisha kuchanjwa... something fishy
Na isitoshe Biden ndio next Fishy master mkuu, Trump kaangushwa kwa kusudi kabisa wait and see
 
Dunia imefika ukingoni ndugu yangu. Mungu atusaidie tu kwa kweli
 
Duh... Luna kitu si bure... yani ugonjwa umekuwa maarufu kwa siku chache na chanjo tayar na wanataka Walter Africa na policy za usafir zimeanza kulazimisha kuchanjwa... something fishy
Na isitoshe Biden ndio next Fishy master mkuu, Trump kaangushwa kwa kusudi kabisa wait and see
Kuna mkakati mahususi ktk jambo hili la korona na chanjo. Hakika walisema magwiji wa fikra wa dunia kuwa kuna jambo linaandaliwa. Kuangushwa kwa Trump ni majanga kwa nchi za Africa.
 
Back
Top Bottom