#COVID19 Urusi yaidhinishwa chanjo ya kwanza ya CoronaVirus duniani

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais Vladimir Putin ametangaza kuwa Urusi imeidhinisha rasmi chanjo ya COVID19 iliyotengenezwa na Taasisi ya Galameya iliyopo Mji Mkuu wa nchi hiyo, Moscow

Akizungumza na Mawaziri kupitia mtandao, Rais Putin (67) amesema hii ni mara ya kwanza kwa chanjo dhidi ya CoronaVirus kuidhinishwa duniani

Ameongeza kuwa, chanjo hiyo imepitia hatua zote muhimu na kwamba binti yake aliyekuwa na homa ameitumia na anaendelea vizuri kwa sasa

Hata hivyo, Urusi haijatoa taarifa zozote za kisayansi kuhusiana na chanjo hiyo

===

1597139083770.png

Russia has officially registered a coronavirus vaccine developed by the Moscow-based Gamaleya Institute, President Vladimir Putin said on Russian state TV on Tuesday.

Speaking in a live teleconference with his cabinet ministers, Putin said the vaccine had gone through all the necessary checks.

The Russian President said one of his daughters has taken the vaccine; he said she had a slightly higher temperature, but that she now feels better.

Reports about Russia's vaccine have come amid concerns about its safety, effectiveness and allegations that the country has cut essential corners in its development.

Russian officials told CNN previously that crucial Phase III trials would take place after state registration of the vaccine.

Russia has released no scientific data on its vaccine testing and CNN is unable to verify its claimed safety or effectiveness.

Critics say the country's push for a vaccine comes amid political pressure from the Kremlin, which is keen to portray Russia as a global scientific force.

Source: CNN
 
Habari wakuu.

Rais wa Urusi ametangaza kupatikana kwa chanjo ya covid19 leo akiwahutubia mawaziri wake kwa njia ya video.

Amesema chanjo ni ya uhakika kwa kuwa imekuwa ikifanyiwa majaribio takribani miezi 2 sasa na kwamba moja ya walijaribiwa chanjo hiyo ni binti yake.

Taarifa zaidi zinafuata, chanzo ni shirika la utangazaji la Ujerumani DW

====
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kwamba chanjo iliyotengenezwa ndani ya Urusi kwa ajili ya ugonjwa wa Covid-19 imeidhinishwa kwa matumizi baada ya kufanyiwa majaribio kwa binadamu chini ya miezi miwili.

Bwana Putin amesema kwamba chanjo hiyo imepita vigezo vyote vilivyowekwa na kuongeza kwamba binti yake tayari amepatiwa.

Maafisa wamesema kuwa wanampango wa kuanza kutoa chanjo hiyo kwa umma kuanzia Oktoba.

Wataalamu wameonesha wasiwasi wao kuhusu kasi ya kazi ya Urusi na kusema kuwa watafiti huenda wametumia njia za mkato.

Huku wasiwasi ukiendelea kuhusu uwezekano wa usalama kuingiliwa wiki iliyopita Shirika la Afya Duniani (WHO) liliitaka Urusi kufuata miongozo ya kimataifa ya kutengeneza chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Chanjo iliyotengenzwa na Urusi sio miongoni mwa orodha ya zile za WHO ambazo zimefika awamu ya tatu ya majaribio kunakohusisha majaribio kwa watu wengi zaidi.

Akiitaja chanjo hiyo kuwa ya kwanza Duniani, Rais Putin amesema chanjo iliyotengenezwa na taasisi ya Moscow ya Gamaleya, inatoa "kinga endelevu" dhidi ya virusi vya corona.

Waziri wa Afya Mikhail Murashko amesema chanjo hiyo imethibitisha kuwa salama na yenye ufanisi", na kupongeza kwamba ni hatua kubwa kuelekea ushindi kwa mwanadamu dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.

Wiki iliyopita, Serikali ya Urusi ilitangaza kwamba inajitayarisha kuanza kutoa chanjo hiyo kwa umma baada ya majaribio yake kufanikiwa.

Zaidi ya chanjo 100 kote duniani zinaendelea huku baadhi zikifanyiwa majaribio.

Licha ya maendeleo hayo yaliyopigwa kwa haraka, wataalam wengi wanafikiria kwamba chanjo hiyo haitakuwa inapatikana kwa wingi hadi katikati ya 2021.

"Baadhi ya watafiti binafsi wanadai wamebaini kitu, na bila shaka ni habari njema,"Msemaji wa WHO Christian Lindmeier amezungumza na wanahabari Agosti 4 August.

"Lakini katikati ya utafiti au kuwa na fununu ya kupata chanjo inayofanyakazi, na kupitia hatua zote, hatua kubwa imepigwa."

1597149856143.png
 
Screenshot_20200811-152112.jpg
 
Urusi haijawahi kuwa na sayansi ya hivyo! Kama wameshindwa kurekebisha Antonov, wataweza hili la nano tch!
 
Back
Top Bottom